wadau kibao shoo ya jahazi ya usiku huko lamu

sebene la jahazi usiku huko lamu

mzee yusuf akiwasili kwenye shoo
jahazi wakati wa shoo yao ya mchana lamu
Msanii mahiri wa muziki wa Taarab Mzee Yusuf tarehe 10 Novemba mwezi huu alifanikiwa kukonga nyoyo za wakaazi wa mji wa kihistoria wa Lamu wakatialipoongoza kundi lake la Jahazi Modern Taarab kushiriki katika tamasha lautamaduni la Lamu.
Tamasha hilo ambalo limetimiza miaka 7 huandaliwa nataasisi ya Lamu Cultural Promotion Centre na hushirikisha maonyesho ya Mbioza Punda, Mashindano ya Ngalawa, Ngoma za utamaduni, upakaji wa Hinna,Harusi za Waswahili, makongamano na maonyesho ya picha.
Kundi la Jahazi ambalo ndilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu liliwezakukusanya umati wa watu wake kwa waume wasiopungua 5000. Jahazi lilikuwandiyo kundi pekee kutoka nje ya nchi ya Kenya na wao ndiyo waliotoa burudaniiliyoonekana kukubalika na wakaazi wa mji wa Lamu... Tanzania tuko juu katika sanaa ila basi tu hatujijui.

Habari kutoka CHUZINEWS.
Huyu kijana ni mtambo michuzi...kwa sisi tunaojua taarabu nini...keep it up MZEE YUSUPH, "tulikuona zamani hata ungo hujavunja" una nyodo weweee
ReplyDeleteMichuzi kama utakutana na Mzee Yusuph mwambie kwamba Taarab anaiharibu kwani toka ameanzisha Jahazi taarab yote anataka ifanane na ndombolo yaani inaisha ule utamu wa Taarab, Modern Taarab ilikua ile ya Melody na alipokua Zanzibar stars lakini sasa hilo jahazi litazama kwani hatawezana na ndombolo ya twanga pepeta na wengine, muambie arejee zile style za Zanzibar stars, Jahazi ni copy ya Ndombolo, inauma kuona Taarab tuliokua tunaipenda sasa inakwenda mrama
ReplyDelete