pailoti wa treni ya kwanza kuondoka dar kwenda bara baada ya kusitishwa kwa takriban mwaka mmoja akiaga

gogo likiondoka taratiiiiibu

baadhi ya abiria leo

kaimu stesheni masta wa dar akipunga bendera akiwa na vingunge wengine wa kampuni mpya ya reli kuashiria mwanzo wa safari ya kwanza ya treni ya reli ya kati leo

lainzimeni wa stesheni ya reli ya dar akiwa na furaha isiyo kipimo wakati akiruhusu treni la kwanza la abiria kutoka dar kwenda mwanza na kigoma kuanza safari leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. I hope wamewaeleza watu wanaoishi hizo sehemu zinazopita hii train kuwa leo ni leo....waondoke humo njiani na Ng'ombe zao. Nakumbuka tukiwa wadogo ilikua kila siku ni nusura ya Mwenyenzi Mungu. Kila wakati linapita tu puuuuuu na tulikua tunacheza kwenye rails muda sio mrefu. Mungu huyu ...basi tu ...ila ikawa tabia sijui six senses tulikua kila ikikaribia saa 11 au 12 jioni kila mtoto au mtu anaondoka karibu na hizo sehemu lakini ukweli hamna cha mtu wa kuwaambia kuwa tahadhari au train inapita au inakuja lihorn linaaanza tu puuu mara limefika. Mambo yote ni kwa pekecha pekecha tu.....hehehehehe...


    Hongera zao walioliarudisha hilo train ...Litasaidia usafiri kwa watu wasioweza kulipa mihela ya mabasi au ndege.

    ReplyDelete
  2. Hayo mabehewa si yalikaa sana pale stesheni unattended?!
    Wameyaangalia vizuri usalama wake kweli? Upepo wa chumvi huu wa karibu na bahari isije ikawa mabosi na sakafu vyote vimepata miKUTU, mtu anwenda chooni anakanyaga ndo anatumbukia moja kwa moja mpaka kwenye reli, na ndinga ndo liko kwenye mwendo.
    Patamu hapo!

    ReplyDelete
  3. MASKINI WATANZANIA WANAFURAHIA HAKI YAO!!!!! HII NI HAKI YAO LAKINI WAO WANASHUKURU KAMA VILE WAMEPEWA MSAADA!!!

    ReplyDelete
  4. Hongerani kwa kuwezesha treni kufanya kazi tena baada ya kusimama kwa muda mrefu.

    Nasikia kuna upungufu wa mabehewa, kweli amini usiamini tulivyo na viongozi wasio na mwelekeo, yatakuja yaliyotumika huko Bombay wanatafuta pa kutupa, na serikali itayapokea kwa shangwe. Wasafiri wa kanda hiyo na wafanyakazi shirika hilo wanaoipenda Tanzania mkiona unyama huo toeni taarifa

    ReplyDelete
  5. Kuna siku mtindo huu wa kuayahujumu mashirika yetu kwa kuyafanya hayajiwezi kwa muda fulani kupata sababu ya kuuza kwa hawa tunaowaita wawekezaji utang'amuliwa na kuumbuliwa kama walivyoumbuka wezi wa BOT. Hii technic ya uhujumu wenzetu wa Kenya waliing'amua na kuwatimua "wawekezaji" wa Uchumi Ltd. Serikali inapaswa irejee ule mkakati wa 1982-83 wa walanguzi na wahujumu uchumi ili kuubaini uhujumu huu.

    Inauma sana tena mno. Huu ni uhujumu. Ni hujuma. Tuna jihujumu kwa kwa faida ya nani?

    ReplyDelete
  6. je, Vyoo visafi?

    ReplyDelete
  7. Ndio uzuri wa biashara za kidosi,hamna cha usalama,ubora,uimara wala usafi.Na wanajua kweli wapi PAKUJIFANYA WANAWEKEZA.
    Mmmh!Yetu macho,manake wakisha chota wanachotaka tuko palepale.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...