Na Mgaya Kingoba wa HabariLeo, Dodoma
MANAIBU mawaziri watano, wakuu wa wilaya na viongozikadhaa wa zamani wa chama na serikali na wanasiasawatatu wa upinzani waliohamia Chama Cha Mapinduzi(CCM) hivi karibuni, ni miongoni mwa walioshindwakatika uchaguzi wa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifaya chama hicho (NEC).
Wakati wanasiasa hao wakishindwa kuingia ndani yaNEC, watendaji wakuu wa chama hicho akiwamo KatibuMkuu, Yussuf Makamba na mawaziri kadhaa wakiongozwa naWaziri Mkuu Edward Lowassa, walishinda uchaguzi huouliofanyika juzi wakati wa Mkutano Mkuu wa Taifa waNane wa CCM uliomalizika jana alasiri kwenye Ukumbi wa Kizota hapa.
Manaibu mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nnewalioshindwa ni Rita Mlaki (Ardhi, Nyumba na Maendeleoya Makazi) na Mwantumu Mahiza (Elimu na Mafunzo yaUfundi) walioshindwa kwa kundi la viti 13 WanawakeBara.
Wengine ni Dk. Diodorus Kamala (Ushirikiano waAfrika Mashariki), Dk. David Mathayo (Chakula,Ushirikana Masoko) na William Ngeleja (Nishati na Madini)walioshindwa kupitia kundi la viti 20 Tanzania Bara.
Katika uchaguzi huo, walioanguka wengine waliopitia katika kundi la Wanawake Bara ni aliyewahi kuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Tatu Ntimizi, Katibu Mkuu wa zamani wa UWT, Halima Mamuya, wakuu wa wilaya;Halima Kihemba, Chiku Galawa, Fatma Kimario, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Mrisho, wabunge; EstherNyawazwa, Zainab Vullu, Margaret Mkanga, BeatriceShelukindo na wanahabari Jacqueline Liana na Jane Mihanji, wote wa Uhuru/Mzalendo.
Walioshinda na kura zao katika mabano ni MargaretSitta (1,780), Zakia Meghji (1,207), Pindi Chana(1,203), Anne Makinda (1,146), Diana Chilolo (1,105),Dk. Aisha Kigoda (1,060), Anne Kilango-Malecela (983),Dk. Rehema Nchimbi (887), Shamsa Mwangunga (850),Khadija Kopa (842), Asha Baraka (766), Kate Kamba(706) na Sophia Simba (689).
Katika kundi la Tanzania Bara, mbali na akina Dk.Mathayo, Dk. Kamala na Ngeleja, wengine waliotupwa nje ni wakuu wa mikoa; Dk. James Msekela, Isdori Shirima, Abeid Mwinyimsa, wakuu wa wilaya; Pascal Mabiti, Frank Uhaula, David Holela, Dk. Ibrahim Msengi, waandishi wa habari Lucas Kisasa, Shy-RoseBhanji na Novatus Makunga.
Wengine ni Balozi Emmanuel Mwambulukutu, mawaziri wa zamani Wilson Masilingi, Hassan Ngwilizi, Mwenyekiti wa zamani wa Mkoa wa Mara, Enock Chambiri, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi na wabunge; Profesa Idrisa Mtulia na Job Ndugai na mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Salim Hamis Salim ‘Chicago’.
Katika kundi hilo la ‘kifo’, waliopenya ni Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliyeongoza kwa kura 1,681, Andrew Chenge (1,530), Yussuf Makamba (1,510), Bernard Membe (1,281), Jaka Mwambi (1,239), Profesa Juma Kapuya (1,216), Abdulrahman Kinana (1,204),Christopher Gachuma (1,181), Stephen Wassira (1,107),Aggrey Mwanri (1,068), Milton Mahanga (1,067),Frederick Sumaye (1,065).
Pia wamo John Komba (1,056), Kingunge Ngombale-Mwiru(1,023), John Chiligati (910), Amos Makalla (871),Profesa Samuel Wangwe (817), Profesa David Mwakyusa(754) na Jackson Msome (747).
Wanasiasa waliojiunga na CCM kutoka vyama vyaupinzani; Richard Tambwe Hizza na Thomas Ngawaiya walikwama baada ya kushindwa katika Kundi la Wazazi Bara, huku kiongozi mwingine wa zamani wa upinzani,Salum Msabah Mbarouk akishinda kwa upande wa viti 20 kundi la Tanzania Visiwani.
Mbali na Tambwe na Ngawaiya, wengine walioshindwa kwa Wazazi ni mshairi maarufu Salim Tambalizeni, wakuu wawilaya; Danhi Makanga, Athuman Mfutakamba, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, mbunge Ruth Msafiri(Muleba Kaskazini).
Walioshinda ni Stella Manyanya (948), Zainab Gama(818), Mussa Azzan Zungu (730), Adam Kighoma Malima(698), Mohammed Nondo (679) na Richard Nyaulawa (669).
Kwa upande wa Zanzibar kundi hilo la Wazazi, washindini Dogo Iddi Mbarouk, Fatma Abeid Haji, Mtumwa YussufPeya na Hassa Rajab Khatib.
Walioshinda kwa upande wa Umoja wa Vijana Kundi la Bara ni Zainab Kawawa (1,390), Violet Mzindakaya Mpogolo (1,165), Nape Nnauye (1,056), Jerry Silaa(994), Sarah Ally (935), Beno Malisa (857), EdwinSanda (804) na Lucy Mayenga (770).
Miongoni mwa walioshindwa katika kundi hilo ni mgombea Penias Kaindoa ambaye wakati akiomba kura,aliwasihi wajumbe wamnusuru ili asiwe mkimbizi kwenye nchi yake, akitokea katika Jimbo la Bukoba Mjini lenye upinzani mkali na Chama cha Wananchi (CUF), akidai akirudi bila kuchaguliwa, atakuwa katika wakati mgumu.
Washindi kwa upande wa Vijana Zanzibar ni Hawa SukwaSaidi (930), Hamad Masauni Yussuf (894), Adila HilalVuai (886), Michael Charles Bundala (845), AshuraAbdallah Ismail (808) na Suleiman Muhsin Haji (771).
Washindi kwa upande wa Tanzania Visiwani ni Dk. AliMohamed Shein (1,663), Shamsi Vuai Nahodha (1,525), Dk. Hussein Ali Mwinyi (1,496), Dk. Mohammed GharibBilal (1,366), Saleh Ramadhan Ferouz (1,352), Muhammed Seif Khatib (1,346), Samia Suluhu Hassan (1,281),Kidawa Hamid Saleh (1,212), Msabah (1,151), Khadija Hassan Aboud (1,076), Mansour Yussuf Himid (1,073),Omar Yussuf Mzee (1,022), Balozi Seif Ali Iddi (997),Mohamed Hassan Nassoro Moyo (959), Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (958), Maudline Cyrus Castico (950),Vuai Ali Vuai (943), Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki(936), Thuwayban Edington Kissasi (860) na Dk. Ishau Abdula Khamis (840).
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwa upande wa uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa alipata kura za Ndiyo 1,879, na kura tano za Hapana, kati ya kura halali 1,887, huku kura moja ikiharibika na ushindi wake ni sawa na asilimia 99.78.
Sitta alisema kwa upande wa Makamu Mwenyekiti TanzaniaZanzibar, Rais Amani Abeid Karume alishinda kwa kupatakura 1,886 za Ndiyo, kati ya kura 1,887. Kura moja ilimkataa na ushindi wake ni sawa na asilimia 99.94.
Rais Jakaya Kikwete ambaye tangu Juni 25, mwaka jana alikabidhiwa mikoba ya uenyekiti wa CCM na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, jana alikabidhiwa rasmi kipindi chake cha kwanza kwa kuchaguliwa kwa kura za Ndiyo 1,887, kati ya kura halali 1,892, kura tanozi kimkataa na hivyo ushindi wake ni sawa na asilimia 99.73.
Mwenyekiti huyo mpya wa CCM alitangaza kuwa leo Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho itakutana kwamara ya kwanza na kisha kuteua Kamati Kuu na kuundwakwa Sekretarieti mpya itakayoiongoza CCM kwa miakamitano hadi mwaka 2012.
Kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Nane wa CCMjana kulihitimisha mchakato wa uchaguzi ndani ya chamahicho ulioanza Januari mwaka huu kuanzia ngazi yaShina.


God hata yesu alikuwa akishindwa kwa kura nyingi jamani yaani mnataka kuniambia 99% ameshindwa kwa kura moja au tano where are you guys mmelala hata mitume walikuwa wanapingwa na wafuasi wao sasa hao viongozi wakiritimba watakuwa hapo mpaka lini na wewe kingoba hivi hilo limkutano lenu likikuwa kizota au chimwaga just wanna no niko ughaibuni mimi hivi wadaganyinka na kikwete i swear huyo baba yenu mpya wa taifa atahakikisha amewaaacha wote viwete chao from mexico
ReplyDelete"...NILIPOAMBIWA KUA UYAONE NIKAJUA NIYAONE MAGHOROFA KUME NDIO HAYA YA KUYAONA..."
ReplyDeleteEe bwana Kaka Michuzi, najua kuuliza si ujinga, nami naomba nichukue fursa hiyo. Haya matokeo ya NEC sisi kama walalahoi yanatuhusu nini, na yanasaidia nchi yetu kivipi?
ReplyDeleteDuh Michuzi huyu Pope kanifurahisha sana na Comment yake kuwa alidhani akue ayaone maghorofa... duh watu wengine wanafikiriaga nini sijui.....hahahaha Big Up Pope
ReplyDeletejamani mimi nakuomba kama unaweza kunisaidia maoni yangu kuwa ni kwamba mtu kama kinhunge gombale mwiru ni kama hivi wht jamani bado anachaguliwa anapaswa astaafu huyu mtu jamani kwanza ameshazeeka saana embu apumzike kidogo alianza na mzee marehu nyerere sasa atakua anasinzia bungeni wekeni damu moto vijana mbona mnaweka watu wazee na mambo yao yatakua nia kizee halafu kw heshima ange stafu au mnaonaje watanzania wenzangu???
ReplyDelete