Salamu za rambirambi zinazidi kumiminika kufuatia kifo cha Mzee wetu Kanyama Chiume huko New York, Marekani. tovuti maalum ya rambirambi iko wazi kwa kubofya hapa

Tafadhali saidia kufikisha ujumbe kwa ndugu na jamaa wengine. Ahsanteni sana kwa mshikamano na upendo wenu katika wakati huu wa huzuni.


- Familia ya Chiume.

Title: KLH News Episode: Buriani mzee Kanyama Chiume...
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2007-11-23T10_20_20-08_00

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kuna msemo wa kichina kwamba mtoto ni kama kipande cha karatasi na kila mtu anaweka alama yake kwa huyo mtoto.

    Wakati nikiwa mtoto miaka ya mwanzo ya themanini huko kijijini kwetu Mnazi kando ya milima ya usambara km 65 toka Mkomazi ndani kweli kweli, nilifungua gazeti la uhuru siku moja (nakala kama ya mwezi hivi) nikaona makala ya Mzee Kanyama nikaisoma na tangu hapo sikurudi nyuma.

    Alikuwa link yangu na ulimwengu nje ya Mnazi, nilikuwa nasoma makala zake kila wiki japo magazeti yalikuwa ni ya zamani.

    Hakujua alikuwa amepata msomaji darasa la tano kaskazini ya wilaya ya Lushoto? Na hii ni changamoto kwa wasomi na wote wanaoandika makala au vitabu.

    Kupitia Mzee Chiume na wengine kama Nizar Visram, Haroub Hosman na baadaye Jenerali Ulimwengu nimeilewa nchi yangu, Africa na dunia kwa mapana yake. Ameacha ALAMA kubwa ndani ya ubongo wangu.

    Kwa wafiwa wakumbuke msiba huu si wao pekee ni wetu sote na Africa imempoteza mwanawake mtiifu. MZEE KANYAMA CHIUME MWILI UMEKUFA FIKRA ZAKO ZITAISHI MILELE.
    H.S. Mpunga. London

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...