
Salamu za rambirambi zinazidi kumiminika kufuatia kifo cha Mzee wetu Kanyama Chiume huko New York, Marekani. tovuti maalum ya rambirambi iko wazi kwa kubofya hapa
Tafadhali saidia kufikisha ujumbe kwa ndugu na jamaa wengine. Ahsanteni sana kwa mshikamano na upendo wenu katika wakati huu wa huzuni.
- Familia ya Chiume.
Title: KLH News Episode: Buriani mzee Kanyama Chiume...
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2007-11-23T10_20_20-08_00


Kuna msemo wa kichina kwamba mtoto ni kama kipande cha karatasi na kila mtu anaweka alama yake kwa huyo mtoto.
ReplyDeleteWakati nikiwa mtoto miaka ya mwanzo ya themanini huko kijijini kwetu Mnazi kando ya milima ya usambara km 65 toka Mkomazi ndani kweli kweli, nilifungua gazeti la uhuru siku moja (nakala kama ya mwezi hivi) nikaona makala ya Mzee Kanyama nikaisoma na tangu hapo sikurudi nyuma.
Alikuwa link yangu na ulimwengu nje ya Mnazi, nilikuwa nasoma makala zake kila wiki japo magazeti yalikuwa ni ya zamani.
Hakujua alikuwa amepata msomaji darasa la tano kaskazini ya wilaya ya Lushoto? Na hii ni changamoto kwa wasomi na wote wanaoandika makala au vitabu.
Kupitia Mzee Chiume na wengine kama Nizar Visram, Haroub Hosman na baadaye Jenerali Ulimwengu nimeilewa nchi yangu, Africa na dunia kwa mapana yake. Ameacha ALAMA kubwa ndani ya ubongo wangu.
Kwa wafiwa wakumbuke msiba huu si wao pekee ni wetu sote na Africa imempoteza mwanawake mtiifu. MZEE KANYAMA CHIUME MWILI UMEKUFA FIKRA ZAKO ZITAISHI MILELE.
H.S. Mpunga. London