HOME COMING PARTY FOR BIG BROTHER 2007 RICHARD (PICTURED ABOVE WITH MULTICHOICE TANZANIA STAFF) WILL BE HELD AT THE PEACOCK MILLENIUM HOTEL AT KIJITONYAMA, DAR ES SALAAM, POOLSIDE ON NOVEMBER 23, 2007 FROM 21h00.
ENTRANCE FEE WILL BE 20,000/- OR YOU CAN BUY YOUR TICKET IN ADVANCE AT PRIME TIME OFFICES LOCATED AT NIC INVESTMENT HOUSE BUILDING ON THE 5TH FLOOR


Kaka Michuzi
ReplyDeletewaama hadi sasa nimechoka na nina hasira na huyu Richard kwa hasa watz kwa ufahamu wao mdogo wanaomuheshimu huyu jamaa kama shujaa aliyetutoa kimasomaso
Huo ni ufinyu wa mawazo,,ukweli ni kuwa huyu Richard alitudhalilisha sana sisi watz kwa sababu tu ya tuhela huto,alifikia hatua hata ya kuonyesha uume wake hadharani kwenye TV ili tu ashinde!
Akafanya ngono hadharani na yule dada wa Angola hadharani kitu ambacho ni kinyume sana na mila za watz
Kibaya zaidi jamaa huyu kaoa na ana familia,alikuwa anatudhalilisha sana hasa sisi wenye familia hasa kwa kitendo chake cha kumdhalilisha dada yule wa Angola kw akuingiza vidole vyake mbele ya TV kwenye uuke wa dada yule
Kuna shirika moja la kutetea haki za wanawake nchini UK imemuelezea jamaa huyu Richard kama MTZ asiye na akili,na ni mbumbumbu wa utunza maadili,,sasa sisi tunamshagilia sana kwa lipi hapo?
Michu,wewe ni mzazi na hata mwanao/wanao tunawajua,,iweje huyu jamaa ashagiliwe sana ili hali alitudhalilisha>?je magazeti ya nje ya tz yanayompaka na kuonyesha picha zake za utupu yanamsingizia?au kaka Michu hujaona"combo pics"za jamaa huyu akipozi kakaa uchi wa mnyama?
Sasa hiyo party watu waje kuona tena utupu wake au?No mater what,we have to preserve our tradition,dont mimic it only because of money!!Richard Go T o Hell@@
na nyie ya Richard yashapita hebu kaeni mfnye kazi..eeh mwataka umaarufu kupitia migongo ya wenzenu!! wabongongo bwana.
ReplyDeleteHeri mimi sijasema. Richard, Richard ...., Naona tujaribu kuangalia nini cha kushabikia na wala si matusi aliyoyaonyesha richard.
ReplyDeletehuyo anony wa kwanza nakupongeza kwani yote niliyotaka kuyasema umeyamaliza wewe!hivi tunakwenda kutoa20,000 za nini amefanya nini kama sio ujinga, upumbavu na ubaradhuli?tunaenda wapi kwa style hii?ujinga kabisa
ReplyDeleteWhat??????????? 20,000/= yaani wabongo bwana wameishageuza dili eti kumuona kiingilio na hawa lazima watakuwa clouds(prime time promotions) maana hizo ndio kazi ambazo zinazowaweka mjini utafikiri sijui wameambiwa ni nani mimi nawashangaa sana
ReplyDeleteAsante sana Anonymous apo juu wa kwanza kabisa ata ww wa pili,2mechoka na picha za Richard pesa ameshapata ss atulie na mkewe na familia yake kwa ujumla,ss hayo mengine ya kurudiana na mkewe ayatuhusu magazeti mengi sana yanamuandika haswa ya udaku tayari tumeshamuona na muacheni ss azifaidi hizo pesa alizoenda kujizalilisha uko BBA,na kama anashukrani au fadhira atamtafuta Tatiana na kumpa kifungu kidogo cha izo pesa alizozipata,sababu yy hawezi kujua ss watazamaji ndio tulikuwa tunamuona kila siku na yule binti wa Angola alivyokuwa anamtetea na alivyokuwa anamfanya awe na mvuto zaidi ndani ya Jumba ata anadiliki kuvaa bendera ya TZ,kusema ukweli Richard au kwa yyte ataye isoma hii comm akamueleze au kama unaisoma ww Ricahrd hii comm Utakuwa hujamtendea haki Tatiana kwa kumnyima hata senti moja ni dhambi sana ukiwa kama mkristu mwenye moyo safi,kwanza katubu pili peleka zaka na kingine plz nenda kwa tati au mtumie au aje achukue ata kidogo utapata baraka kwa mungu.Ni hayo tu.reen_minja@yahoo.com
ReplyDeleteNilikua nina mpango wa kwenda kwenye hiyo party, lakini kama mambo yenyewe ni ya kwenda kuona utupu kwa kiingilio cha elfu ishirini. I say noooooooooooo nina wangu ninaona kila siku.
ReplyDeleteKuna watoa maoni hawana habari kuwa Michuzi ni'promota' wa Richard.
ReplyDeleteYeye (Michuzi) kazi yake ni kumpigia debe Richard na mpaka ameshinda Big Brother yao -sio mchezo!
Kwa hiyo Michuzi hawezi kusema lolote baya kuhusu Richard (fanyeni utafiti kuhusu matukio yoote mabaya yaliyotokea Michuzi hajaripoti hata moja!!!!)
Bila shaka kamisheni ya Michuzi ni 10% au zaidi ya bulungutu la Richard!
Nilikataa toka mwanzoni kuwa BBA ni mning'inio wa kikoloni toka BBE na haitufundishi chochote cha maana zaidi ya kutafuta Mwafrika ambaye yuko tayari kuwaza,kusema au kutenda hadharani kama mwehu na muhuni asiyejali kupitia Kamera zianikazo uozo huo dunia nzima.
ReplyDeleteKwamba Mwafrika mshiriki awe tayari pasipo aibu kufanya ambayo kwa kawaida asingeyafanya mbele ya macho ya watu isipokuwa kwa ahadi ya hisabati za yamkini(probability calculations) ya kupata fedha za kibahati nasibu kupitia kura za washabiki.
Kwamba hata wanawake/wasichana wengi wanaoingia ndani ya jumba wanakuwa na mahesabu ya kuwa tayari kupozi maongezi, viungo na mitembeo yao kama ulimbo kunasa mwanaume na ikiwezekana hata kuwachanganya. Na kwamba wanaweza kujitongozesha kwa wanaume waliomo Jumbani ili tu walambane na kuamshana hisia za kingono na hata kufanya ngono salama au sisizo salama ili mradi vituko vyake vinaishia kueleza kile Washabiki wakiitacho 'anatufurahisha sana tunaomba aendelee kuwemo ndani ili aendeleze kutupa vituko mpaka mwisho!!!'.
Hivyo sikupiga kura yeyote, sikushangilia ushindi wa kutudhalilisha, sikwenda Airport ng'o na wala simfagilii Richard hasilani na wala sitoi hata senti tano eti kwa ajili ya welcome home party ya kipumbavu (samahani kwa kuandika tusi ni hasira nilizo nazo juu ya suala hili linalovuka hata ufahamu wa wasomi na makampuni yenye maadili kama Multchoice ambayo sasa italegea na kuwa Polychoice).
Kama mnafikiri sisi ni washamba au tuna wivu basi ninyi Multchoice tumieni kasehemu tu ka fedha mlizonazo kulaghibisha (facilitate)kwa kutangaza tu 'A Conference on BBA; Challenges & Realities'. Karibisheni wachokozi wa mada na paper zao toka jamii za Wasomi, Wanadini, Wanaharakati wa masuala ya Kijamii, Wanasheria, Wafanyabiashara, Waandishi wa habari, Wasanii na hata Wanasiasa muone mlivyochemka!
Tena hapo niko tayari kutoa Tshs.40,000/= niwasilishe mada yangu kuokoa kizazi kijacho kuliko Tshs. 20,000 kushangilia udhalilishwaji wa Mtanzania mwenzangu, Waafrika wenzangu huku tukimwongezea maumivu mke wa Richard!
KAKA MICHUZI, ILIMCHUKUA MTOTO MDOGO KUSEMA MBONA MFALME YUKO UCHI WAKATI WAZEE WANASHANGILIA KUWA ANA VAZI LISILOKIFANI!
Nanye, Nyakatakule Unyilisya Echalo
Kumshabikia huyu Richadi ni upuuzi, isipokuwa kwa ndugu zake wa karibu.
ReplyDeleteNa pia hakumdhalilisha mtu yoyote (nyie mnaojifanya mmedhalilishwa), kama ni kujidhalilisha kajidhalilisha yeye mwenyewe, na siyo mtanzania mwingine yoyote.
Mbona George Michael alipokutwa anachokolewa chooni hamkusema kawadhalilisha waingereza?
Mbona Bill Clinton alipomtifua monika lewinsky ofosini hamkusema kawadhalilisha wamarekani?
Muacheni Richadi wa watu na upumbavu wake kivyakevyake.
Eti kaingiza vidole na kuonyesha uume, wewe umejuaje hayo kama hukuangalia na ku tegea sehemu ambapo ngono inaonyeshwa?, ulikuwa biggest fan wa Richard sababu ya entertainment yake ndio mana mbaka unajua kila alichofanya .
ReplyDeleteMsijifanye kukemea maadili mabaya wakati ndio wa kwanza kuangalia na kufuatilia ili kuburudika,
Richard rocks
Eti anatudhalilisha... anaharibu 'utamaduni wetu', kwanza unamanisha utamaduni wa nani?
ReplyDeleteKi utamaduni, watanzania si huwa tunaoga mitoni, in public. Sasa Richard alichofanya nje ya utamaduni wa mtanzania au mwafrika kwa kuweka mwili wake wazi ni nini?
Kama walivosema waandaaji, BBA sio shule ya kutufundisha malezi, kwa hiyo kama mtu hupendezwi na yaliyokuwemo, una-switch to other channels. Sasa iweje mtu agande kwenye screen ukimwangalia Rich, kisha uje kusema amekudhalilisha? Tena inaoneka wale wanaolalama ndo wlikuwa hawakosi kuangalia BBA. Inawezekana wengine hamko proud na miili yenu, ndo maana mnamshangaa Richard!
Kabla hamja-generalise kuwa fulani kuharibu utamaduni wetu, kwanza kifunzeni utamaduni ni nini, na utamaduni wa nani!
Watu wangapi wanaibia nchi yetu na kupeleka mamilioni nje? Sasa kati ya mtu anayehangaka kama Richard na kuleta $100K kwenye uchumi, na wale mafisadi wanaoiba na kupeleka nje, ni nani anayetudhalilisha? Mkiweza kujibu hili swali frankly, nadhani tutaacha kumwandama mtoto wa watu Richard.
Yeye ni shujaa, kwa sababu ameleta $100,000 kwenye uchumi wetu, ambazo zitawasaidia WaTZ wengi tuu. Kama kila mtanzania anayeenda nje for 98 days angekuwa anarudi na kiasi hicho cha fedha, mnadhani shilingi yetu ingekuwa hoi kama ilivyo?
Kwa waliomiss action please check:
ReplyDeletehttp://youtube.com/watch?v=NEk1B6FfSzs
na
http://youtube.com/watch?v=5qBednRz82Y
(hiyo link ya pili inahitaji usign in kwa kutumia your Youtube au Gmail account)
Yaani wewe anon wa nov 24 12:26 am
ReplyDeletenaakuunga miguu na mikono yote yaani umesema la maana
yaani watu wanajitia utamaduni utamaduni hasa huyo anon wa kwanza kabisa
nyio ndiyo mnaooga mitoni mchana kweupe na hamjali watoto wenu wanapita njiani halafu leo mnajitia utamaduni!!! nyoooo
wewe umeuonea wapi uume wake kama sio na wewe ndio wale watu wakuangalia picha za uchi
tuondokee hapa
mshamba mkubwa wewe
get over it
omg nilikua nasoma tu lakini siye huku nje hatukuona hii. Wow!! This is unspeakable.
ReplyDeleteyeye ni mume wa mtu huyo msichana naye sijui vipi...wote miozo tu.
Threesome kwenye TV???? ilionekana kwenye TV hii bongo?
Well huku tuliko wasingeonyesha hii kabisa...
Hizi show zilikua live au recorded. Si walikua na uwewzo wa kukata mengine yasiyofaa?
Hii sio culture yetu kabisa!!!!!!
Heee, mh!!!! Watanzania bwana? kaazi kweli kweli.
ReplyDeletesasa kama mtu hutaki kwend kulipa 20,000 si ukae nyumbani tu kimya kimya?. Maneno meeeengi, kakudhalilisha, katudhalilisha, utamaduni, blah, blah, blah. Mijitu inaboa kweli.
Wewe anonny wa kwanza na wenzio mnaoongelea utamaduni wa mtanzania, utamaduni gani sasa unaosema? acha walioongelea kuoga mchana mtoni, bora tunaona nini kinafanyika, na sasa mangapi yanafanyika kiuficho hapa Tanzania. Unajua kuwa idadi ya mimba mashuleni inaongezeka? huo ni itamaduni gani, na je prev ya HIV? unajua kwa nini, Kujificha, kufanya maovu gizani, unafiki kama wa kwako. Mnafanya meeengi kuliko aliyofanya Rich mkiwa mmejificha, halafu mnakuwa wa kwanza kuona vibanzi vya wenzenu.
Kama ulitaka kuonesha busara yako, mimi nafikiri haukutumia busara kufikisha busara yako, ee bwana. Tulia, kama huna hela ulale, wenye hela waende, wala usiwaite wajinga kila mtu na namna yake ya kutafuta pesa, ili mradi tu hakuna anayepitisha patrol nyumbani kwako. HUku umebana pua "maactivist huko ulaya wamesema Rich ni mtanzania mpumbavu" weweeeeee, acha hizo, ulaya ulaya, wao wana nini watusemee wa TZ, kwani tabia hizi zote zimeletwa na nani kamasio hao walaya unaowasifia.
Haki za mwanamke!!!! ndio, lakini nani amletee haki kama yeye hahitaji haki, Kwani BBA kulikuwa na wanawake wangapi, na je mbona rich hakufanya hivyo na wote? huyo tatiana alikuwa amekolea, na kama hakutaka kingiziwa vidole angebaki nyumbani, na hata wewe ukijidai kwenda BBA watakufanyia hivyi hivyo, so jiheshimu uheshimike. Kama tatiana angebakwa unafikiri dunia ingekaa kimya, alitaka mwenyewe.
anony wa 1 &2 umeboa sana
we unayesema kafanya ngono hadharani kinyume na maadili ya watz, umelala saa zote nini?
ReplyDeleteWatz wanaongoza kwa ukimwi, je wanaupataje? kwa kutizamana macho na kuongea?
Achane propaganda za chuki kwa vile jamaa kashinda.
Do you!
wow, that is amazing! aisee bongo imeendelea wanaiga kuwapita hata wenyewe wazungu.
ReplyDeletedu noma,
HUU WAZIMU, MULTI CHOICE MANAFANYA BIASHARA YA UTUMWA SASA NA HIZO SH.20,000/ NI ZA NINI PARTY WATU HUALIKWA ZILE DOLA ZINATOSHA KUPOROMOSHA PARTY. MIE SIJI NG'O.
ReplyDelete