hatimaye safari za treni toka dar kwenda mwanza na kigoma zimeanza rasmi leo jioni toka stesheni ya dar baada ya kusitishwa kwa takriban mwaka mmoja. ratiba inaonesha kwa kuanzia safari hizo zitafanyika mara mbili kwa wiki badala ya tano za awali ambapo jumapili na jumanne itakuwa safari ya dar/mwanza/kigoma na jumanne na alhamisi ni mwanza/kigoma/dar. bofya hapa kumjua mwekezaji mpya wa shirika la reli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kumradhi kwa wenzangu wa bongo; lakini Mzee Michu hebu niambie ni kitu gani cha kujivunia kuona hilo pipa bovu lenye kutu na chafu hivyo likishangiliwa na wananchi namna hii? tutafika kweli? ubinafsishaji gani huu ambao maendeleo yake ni kulifanya treni liweze kwenda mbele na nyuma badala ya kufanya "overhaul" ya mabehewa hayo. Daaaamn!!!
    Wameshindwa nini hao wawekezaji kupaka rangi mpya na kuweka viti safi kwenye hayo mabehewa? Kulikoni.

    Mdau wa Newala.

    ReplyDelete
  2. KWANZA KABISA HONGERA SANA KWA WAWEKEZAJI KUTOKA INDIA.MNATUOKOA SANA SISI WASUKUMA,WAGOGO NA WAVINZA.MAKE BILA HIVYO MAPUMZIKO YA DAR TUNAYASIKIA TUU.MABASI YA KUPITIA ARUSHA >KENYA >MWANZA YALIKUWA YANAPANDISHA BEI KILA SIKU.SASA MMETUOKOA,MUNGU AWAZIDISHIE.

    VIJANA WAKITANZANIA WENGI NA WAZEE WALIOIBA SERIKALINI HAWATAKI KUWEKEZA NYUMBANI??INASIKITISHA SANA SISI WADOGO ZENU,TUNAKOSA WATU WA KUIGA.

    VIJANA WENGI NA WAZEE WENGI TANZANIA WAMEKUA NI WASHABIKI WA POMBE NA WANAWAKE WASIOKUWA NA MISIMAMO.

    GOGO LILISIMAMA KWA SABABU LILIKUWA LIKIENDESHWA KWA HASARA KUBWA SANA BILA FAIDA.HII NI KWA SABABU YA VIONGOZI WENGI PALE RAILWAY NI WASANII NA WALEVI KWELIKWELI.

    WANASAFIRISHA MABEHEWA YA MIZIGO TOKA MWANZA MPAKA DAR,BILA KUWALIPISHA WAFANYABIASHARA,KISHA WANAPOKEA HONGO KUTOKA KWA WAFANYABIASHARA HAO.

    NDIO MAANA MABOSI WENGI WA RAILWAY WANANYUMBA ZENYE THAMANI KUANZIA
    TSH/50,000,000 MPAKA 200,000,000.
    KWA MISHAHARA YA RAILWAY HUWEZI KUEZEKA NYUMBA HIZO.

    WAWEKEZAJI WA KIHINDI NI LAZIMA WAWE MACHO BILA HIVYO ITAKUWA HADITHI ILE ILE.

    UKITAKA KUONA KWAMBA WENGI WALIIBA ANGALIA HIYO INGINI YA MABEHEWA HAYO,ZOTE ZIMECHOKEANA,NA NILAZIMA UWE NAZO MBILI KWA WAKATI MMOJA ILI UWEZE KUVUTA MABEHEWA KUMI.
    HAWATAKI KUKUSANYA PESA ILI KUNUNUA VICHWA VINGINE???

    KUNA KAMPUNI MOJA YA MABASI MWANZA.ILIANZA VIZURI SANA.INAITWA TANGANYIKA BUS SERVICE PAMOJA NA TRANS BUS SERVICE.
    SINGASINGA HAWA WANAPIGA KAZI BILA MCHEZO ,LAKINI MSWAHILI ALIPOPEWA KAZI HAPO WALIKUWA WANATIA HASARA YA MAMILIONI.
    MASINGASINGA WALICHANGANYIKIWA KABISA IKABIDI WANUNUE MAGARI MADOGO AINA YA NISSAN TROPPERS.ILI WAWEZE KUPAMBANA NA WASWAHILI.
    KILA BASI LIKIONDOKA SINGASINGA WANALIFUATA BASI KINYEMELA-LIKIFIKA POLINI KAMA KILOMETA 100
    WANALISIMAMISHA BASI KISHA WANAITISHA TIKETI KWA KILA ABIRIA.
    KULIKUWA NA ABIRIA ZAIDI YA ISHIRINI WASIO NA TIKETI NA WOTE WANADAI WAMELIPA.SINGASINGA WANAPINGA SACHI KONDAKITA WANAKUTA ANAPESA ZAIDI YA ZA TIKETI.

    KWA HIYO WAHINDI HAWA WA RAILWAY WAWE MAKINI SANA AMA SIVYO FAIDA YOTE ITAKUWA NDIO INAENDESHA BIASHARA.MAKE WASANII NI WENGI.

    WATU WANAKAA BAA NA MATUMIZI MPAKA WANAISHIWA MFUKONI WAKIJADIRI MIKAKATI YA KUIBA.

    MUNGU ANIEPUSHE NA POMBE.

    WATANZANIA WENGI WANAJIFANYA WANAJUA MENGI ,KUMBE NI HASARA TUU.
    SERIKALI IMESHIDWA KUTOA ELIMU ZA KUJIENDELEZA KWA VIJANA NA VIJANA WENGI WAMEKUWA NI WABISHI.

    ASILIMIA 99.33 YA UCHUMI WA TANZANIA UKO MIKONONI MWA WAGENI.
    WAHINDI NA WAARABU.TAZAMA KARIAKOO
    MAGOROFA YOTE YA WAARABU,BIASHARA ZOTE KUBWA ZA WAHINDI.

    WASWAHILI WEUSI NI ASILIMIA 0.67

    WATANZANIA WEUSI WENGI WANAWEKEZA PESA KWENYE NYUMBA ZA KUISHI WAO WENYEWE. WALIOJITAHIDI NI ASILIMIA 0.67

    MUNGU ANIZIDISHIE UPEO NA NGUVU ILI NIWEZE KUIKOMBOA TANZANIA.Ameni

    ReplyDelete
  3. Michuzi usije ukabania hii...nilizaniaga ni uongo lakini nimeletewa barua kuwa niende nikachukue gari na kusign vyote on Monday. Nilikua kwenye waiting list kwa siz weeks. Though nilizania ni game lakini ...ndio hivyo....

    Mlioko marekani try this ...it will help you around...Good credit and a good valid driver lincense is a must....
    You can drive a free car or you can get paid to drive your car....It is faster and easy for those who live in big cities though but just try ....don't ask me how...I will be driving a free car advertising one catroon show ....who knows ...and I don't care.....

    www.pypes.net

    ReplyDelete
  4. This is $%&*@#....SI mnaliona hilo DUDE linavyofanana....basi hiyo haitoshi.....KWA TAARIFA ZILIZORUSHWA NA VYOMBO VYA HABARI ni kwamba ABIRIA WANAKAA CHINI KWENYE SAKAFU....ila waliobahatika kusatrehe ni wale waliokaa kwenye MBAO CHAKAVU........THIS IS SCANDAL.......LAZIMA AWAJIBIKE MTU....&$%^&*

    ReplyDelete
  5. Mmh......!!! Hayo mabehewa yanatisha kama nini loh!! Inabidi wafanye ukarabati wa kutosha maana,ukisafiri humo hadi ukifika dodoma unanuka kama mbuzi!!

    ReplyDelete
  6. Kuna siku mtindo huu wa kuayahujumu mashirika yetu kwa kuyafanya hayajiwezi kwa muda fulani kupata sababu ya kuuza kwa hawa tunaowaita wawekezaji utang'amuliwa na kuumbuliwa kama walivyoumbuka wezi wa BOT. Hii technic ya uhujumu wenzetu wa Kenya waliing'amua na kuwatimua "wawekezaji" wa Uchumi Ltd. Serikali inapaswa irejee ule mkakati wa 1982-83 wa walanguzi na wahujumu uchumi ili kuubaini uhujumu huu.

    Inauma sana tena mno. Huu ni uhujumu. Ni hujuma. Tuna jihujumu kwa kwa faida ya nani?

    ReplyDelete
  7. Jamani wangeleta mabehewa na Engine mpya. Makosa yanajirudia.Tazama hata notice board ya station tena hapo ni DAR?
    Shame

    ReplyDelete
  8. Hao wawekezaji mmmh,yale yaleee...!Haya,yetu macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...