Michuzi,
Kuna mdau anatafuta makala, magazeti/majarida yenye habari za Lance Spearman ambaye alikuwa muhusika wa makala/tamthiliya za picha (photo novel/photo play/photo comic) zilizochapishwa kati ya miaka ya 1960 na 1970 na magazeti ya Afrika Kusini "Drum Publications Ltd".


Mhusika huyu pia alikuwa anajulikana kama "The Spear" au "Spia"Pia kwa Afrika Mashariki kuna magazeti yaliyochapishwa Kenya yanayoitwa "Film" au "African Film" yaliyokuwa na mhusika huyu kama hilo analosoma mdau pichani.
Pia kuna wahusika wengine kama "Fearless Fang", an African "Tarzan" na wengineo pia kama kuna mtu mwenye kumbukumbu zozote hizo pia zinahitajikaMdau huyu yuko tayari kununua nakala hizo zilizotumika zitakazopatikana kwa ajili ya kuweka kumbukumbu katika maktaba.


Kulingana na ubora na idadi mdau yuko tayari kulipa Euro 5 mpaka 20 Kwa watu wanaofahamu jarida/gazeti linaloitwa "Film Tanzania" na kama kuna mtu analijua na upatikanaji wake mdau anaomba amfahamishe kupitia vicensiashule@hotmail.com


shukran kibao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Film Tanzania? Nipe muda nikapekue masanduku ya baba kabla ya kukupa mail yangu, anayo mengi karibu yote. Stori za Faraji Katalambula, zile mfanyakazi anatumwa kupost barua kumbe mama kazichanganya ya kule kapeleka huku na ya huku kule.

    ReplyDelete
  2. Michu,
    Huyu mdau aliyekutumia ujumbe huu naye ni msanii. Awe wazi tu kuwa anazitaka kwa masuala yake ya kiusanii.
    Mbona malipo yake pia ni kidogo sana wakati kipato chake ni kikubwa na anaweza kulipa zaidi ya Euro hizo. Asituzengue.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  3. Nikusaidie mdau, gazeti la yule Bwana mwenye maguvu mpanda Tembo linaitwa "BOOM" (dRU dACHI)

    ReplyDelete
  4. Film Tanzaniam huh? Wakati Kenya walikuwa na Lance Spearman sisi TZ tulikuwa na mnyalukolo Fred Sengo, complete na nembo yake kama mkuki wa Spear yeye alikuwa na "inyengo" au "imundu" kama waHehe tunavyoiita. Fred Sengo alikuwa mpelelezi fulani hivi kama Spear.

    Aliyecheza kama Spear nasikia alikuja kuwa mwizi wa magari na nadhani alishawahi kupigwa shaba na mapolisi na kulazwa hospitali ya Huruma, Mkuu, Rombo, enzi zile nipo Kili Boys.

    ReplyDelete
  5. Simu ya kifo ! na Faraji Katalambula.Aweza ibuka Mzee wa watu na magazeti yake.

    Mzushi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...