Miss Earth Tanzania 2007 Angel Kileo jana alijumuika na warembo wenzake katika kuwania taji la kipaji (Talent). Mrembo Angel alionyesha ngoma ya kipekee ambapo alicheza na moto akiwa amevalia nguo asilia ya kaniki. Angel Kileo alifundishwa ngoma hii ya kipekee na Kikundi cha sanaa cha Makumbusho na alifanya mazoezi mazito ili kuweza kumudu ngoma hii. Kutokana na utumiaji wa moto, warembo wenzake wengi pamoja na watazamaji waliogopa moto ule, hata hivyo mrembo huyu alikuwa kati ya wachache waliosifiwa kwa kuonesha vipaji tofauti zaidi ya kucheza ngoma za kiasili au kuimba pekee. Mshindi wa talent atatangazwa tarehe 11 novemba.
Home
Unlabelled
vipaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Go girl!Go..!Sisi tuko na wewe sambamba kukushangilia na kukupa moyo kuiwakilisha NCHI YETU!!!
ReplyDeleteMiss ka' mganga wa kienyeji. Kama maisha yamekushinda nenda kalime. Mdau
ReplyDeletenywele mbona za kidhungu,angepiga afro hapo kiafrica.Kuiga jamani.
ReplyDeleteBro Michuzi. Hayo yalikuwa mashindano ya wachawi au waganga wa jadi? Tufahamishe kaka.
ReplyDelete