MAHUJAJI WALIOKWAMA UWANJA WA NDEGE WA DAR BADO WANAENDELEA KUSOTA HAPO UWANJANI HADI DAKIKA HII NA HAIJULIKANI SAFARI KAMA ITAKUWEPO AMA LA. UCHUNGUZI WANGU UMEBAINI KWAMBA KUNA DEGE LA AIRBUS LINATARAJIWA KUTUA SAA KUMI JIONI LEO LAKINI UHAKIKA WA KAMA SAFARI ITAKUWEPO AMA LA NI HADI HAPO BAADAYE. NA HII SAFARI ITAWEZEKANA ENDAPO ATC ITAKUWA IMEPATA TENA 'FLOAT' AMA NAFASI YA KUTUA NA KURUKA UWANJA WA NDEGE WA MADINA BAADA YA KUIPOTEZA ILE YA AWALI ILIYOPEWA NDEGE YA KUKODI. LAKINI PENYE SUBIRA HUWA HERI, NA TUMUOMEB JALALI AWAJAALIE MAHUJAJI KIASI CHGA 1,000 WALIOKWAMA SAFARI HIYO MUHIMU - AMINA
MSTARI MFU KWA MAHUJAJI KUTUA MADINA NI ALHAMISI.
WAKATI HUO HUO MAHUJAJI WALIOKWAMA UWANJA WA NDEGE WANATARAJIA KUANDAMANA KUPINGA KUTOSAFIRI KWAO KWENDA KUHIJI. HAIJAJULIKANA MAANDAMANO HAYO YATAANZA SAA NGAPI NA YATAISHIA WAPI ILA VIONGOZI WA MAHUJAJI HAO AKIWEMO SHEKHE ISSA PONDA WAMENUKULIWA NA REDIO TANZANIA KATIKA TAARIFA YA HABARI YA SAA SABA KWAMBA WANAPANGA KUANDAMANA.


Bongo tambarare.Hali hii inatokea Bongo tu lazima tuwe unique duniani.Kweli sisi wala vumbi lazima tutambe kwamba tumevunja rekodi.Kwa mahujaji poleni kuweni na subira Mwenyezi Mungu atawajalia safari salama Inshallah.
ReplyDeleteMimi kama Sheikh na Alhaji naomba nimshauri Ponda na wenziwe kuwa Kabla kuandamana ni vizuri wajihoji kama wako swafi mbele ya Allah.
ReplyDeleteSababu kama hawako swafi yawezekana ndiyo maana safari yao inakuwa na nuksi na mikosi kibao.Allah anaweza akawa hataki watu hao wende hija.ATC wataionea bure.
Kwenda hija si lelemama.Waweza lazimisha kwenda yakawakumba mabaya zaidi wakti wa hija au baada ya hija.
Kwa uzoefu wangu wa Hija wale walo takata mioyo na kumlingania vizuri Allah safari zao huwa hazina mambo kama hayo.Allah huwaepushia mbali yale wayajuayo na wasoyajua yalojificha katika shimo la shwaitani.
Allah akuepushieni madhara makubwa ya dhambi nyepesi na zile nzito nzito mzijuazo ama msozijua.
Asalaam Aleikum jamiya.
Mi nafikiri ndugu zangu mahujaji kwa sababu tulikuwa tunakwenda kwa Mungu(kuhiji ni kutimiza moja ya nguzo za uislamu) na nikizingatia ushauri wa Mh.Mtutura hiyo ni mitihani ya Mwenyezi Mungu muhimu ni kuwa nia mlikuwa nayo hivyo kiroho mmehiji.
ReplyDeleteSi vyema kuandamana ni sawa na kukataa mitihani ya Muumba,maana wengine walipenda kufanya kama ninyi lakini kifo tu kiliwalazimisha wasitimize hiyo nguzo ni kumshukuru kwani kwa rehema zake mmefika hadi airport.
Inawezekana Mungu hakupenda mkahiji wakati huu ila wakati mwingine.
Nafikiri badala ya kuandamana tuongeze swala inshlaah Mungu atatusikia na atatufanyia kadri anavyopenda yeye.
Wenu,
Majaliwa
Hivi Michuzi lile dege alilonunua Mkapa wakati wa utawala wake hadi tukaambiwa ikibidi kula nyasi tutakula lakini dege lazima linunuliwe, haliwezi kuwawahisha hao mahujaji huko Mecca fastafasta?
ReplyDeleteATC means "Any Time Cancel". Bisha nione!
ReplyDeleteHii laana ya Mwenyezi mungu.. ingekuwa safari ya burudani na urembo au kandanda usafiri tambarareeee.. hebu wapelekeni msiwakoseshe dhawabu zao jamani safari imepangwa miaka mingi hijja ni majaaliwa .
ReplyDeleteMnyezimungu atawapa safari ya kheri Inshaaallah
Ni jambo la kushangaza na kusikitisha pia, iweje uwanja wa ndege ugeuke makazi ya watu waliokosa usafiri hata kugeuka sehemu ya ibada????
ReplyDeleteInajulikana wazi hata kwa mtoto mdogo, ukikosa usafiri huwezi kukaa kituon kwa ahadi za kuwa eti usafiri utakuwepo baada ya muda fulani!!! ni vema ukarudi nyumbani kwako ukasubiri, siyo kituoni!! hapo ni mahali pa wanaofika na wanaosafiri kwenda tu, hata miundombinu ya hapo imetengenezwa hivyo, vyoo,viti, maji nk
Kwanini watu hawataki kuelewa hivyo??? mkiitwa wakorofi mtasemaje???
Mnafanya hata viongozi wanaingia kwenye kundi kama lenu pasipo kujua au kwa nyie kuwalazimisha kuwahurumia!!!
Hata waandishi wa habari nao ni sifuri tu!!!
Tambarare au uwongo mwanangu.Bongo bwana.
ReplyDeleteKweli unaweza kujiita jina ukawa ni kinyume cahke.Huyu aliyewashauri mahujaji warudi nyumbani kwao ame assume kwamba wote wanatoka Dar.Kama mru anaishi Mwanza au Bukoba arudi???Waliowaahidi safari ya kwenda ndio waliopaswa kulaumiwa sio mahujaji.Walipewa ahadi mara tatu ya kusafirishwa sasa waondoke waende wapi??Watu wengine bwana ubongo makamasi matupu.
ReplyDeleteAnnon. hapo juu,anayemiliki uwanja wa ndege ambako hawa watu wanaleta kero na adha kwa wasafiri wengine si yule aliyewakatia tiketi za kusafiri!! au ndiye aliyewaahidi usafiri wao kwa hizo siku tatu!!
ReplyDeleteTofautisha wamiliki wa kiwanja cha ndege na mashirika ya ndege!! ni vitu viwili tofauti.
Narudia tena ukiachwa au kuchelewa au hata safari kuahirishwa, hutakiwi kukaa uwanja wa ndege au kituoni hadi pale tatizo lako litakapotatuliwa na waliokuahidi usafiri, unapaswa kurudi ulikotoka iwe ni pwani, nkasi au popote bila kujali umbali, hali ukiwasiliana na msafirishaji wako namna ya kutatua tatizo lililojitokeza!!!
Ikibidi ukalaumiane nae kule mlikokubaliana juu ya safari, siyo hapo kituoni!
Tafsiri sahihi ya kukosa ustaarabu ni pale uhuru wa mtu mmoja unapoingilia uhuru wa mtu mwingine!!
Uwanja wa ndege panatakiwa pawe safi, kusiwepo msongamano wa watu na patumike tu kwa wanaofika na kuondoka pasipo kulazimika kusubiri zaidi ya masaa matatu!!!
kinyume cha hivyo ni kuleta kero na bugudha kwa wasafiri wengine, ambao hawahusiki wala hawapaswi kujua tatizo lako la usafiri!!
Acha kutetea mambo ya hovyo! yanayoleta temptation si kwa wamiliki wa uwanja pekee, bali hata kwa viongozi wa nchi, kulazimika kuonyesha huruma hata kwa jambo ambalo ukweli uko wazi!