DEGE LA KWANZA KATI YA MATATU YATAYOPELEKA MAHUJAJI WETU KUHIJI BAADA YA KUKWAMA UWANJANI KWA SIKU KADHAA LIMESHATUA EAPOTI KAMA ILIVYOKUWA IMEAHIDIWA MILANGO YA SAA MOJA NA USHEE.
DEGE HILO LINATARAJIWA KUONDOKA MNAMO SAA TATU USIKU HUU, PANAPO MAJAALIWA.
DEGE LA PILI LINATARAJIWA KUTUA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA NA LIMEPANGWA KUPAA SAA SABA USIKU NA KUNDI LA PILI. KUNDI LA TATU LINATARAJIWA KUONDOKA MAPEMA KESHO ASUBUHI.
PAMOJA NA KADHIA HIYO YA KUCHELEWA SAFARI HALI YA UTULIVU IMETAWALA UWANJANI HAPO NA VICHEKO NA TABASAMU VINAONEKANA...


mungu atawafikisha salama
ReplyDeleteSwali..je izo ticket walinunua au walipewa bure, maana ku deal namswahili , halafu unamkosesha safari wakati ni ya bure , hapo ni mara mia una mzidishia usongo ,licha ya usembe wa Air TZ ,kuchelewesha safari.
ReplyDeleteMichuzi!
ReplyDeleteShukran kwa kutupa hizi taarifa, angalau sasa nasi nafsi zetu zitapumua maana wako mama zetu humo, ndugu na jamaa mbalimbali wanaosafiri kwa kweli hata sie tulio mbali tulikuwa stressed na hiyo hali ya kutokujua nini kinaendelea.
Shukrani Mungu akujaalie kila la kheri na baraka.
Wewe mdau wa pili ulishawahi kupewa ticket ya bure na ya ATC au shirika lolote la ndege ili usafiri, hebu acheni dharau zenu za kijinga kwa kuwa ni waislam basi ni waswahili masikini wapewa vya bure na kupenda kupiga kelele sio?
ReplyDeleteMagazeti yote yametaja mpaka na kiasi cha pesa walizolipa kwa ajili ya safari kuwa ni kuanzai dola za kimarekani 2400.
Au mnataka humu kwenye blogu tuwakumbushe historia? Nyerere alikuja Mzizima akakuta wazee wetu na chama chao na harakati zao za kudai uhuru (TAA) walivyokibadilisha kuwa TANU ndio wakasema ngoja tumpe uwenyekiti huyu kijana msomi.
Sitaki kuingia huko lakini usifikiri kuwa waislamu ni masikini wa kusubiri vya dezo, tena uache tabia za prejudice! Jielimishe ili uelimike mtu yoyote aliye na prejudice hata kama amesoma mpaka wapi bado hajaelimika hata kidogo na ustaarabu umempa kisogo.
Wewe anon wa 8.29 acha ushamba unafikiri wewe ulivyopewa tiketi ya bure ya kwenda ulaya kwa skolaship basi watu wote hupewa tiketi za bure.
ReplyDeleteHebu piga simu ATC au KLM au KQ au ET wakupe basi tiketi ya bure ukasalimie kwenu krismas hii. Zipo kama walivyopewa hao waislamu na wewe ukipiga simu taja jina lako watakutumia E-ticket kwenye email yako!! Umesikia Zoba!!
Inshallah m'mungu awafikishe salama maana safari kama hizi huwa hazitaki mizengwe na waajalie hija zao ziwe za kheri.
ReplyDeleteKwa mtizamo wangu ninaona itabidi ATC wawarudishie pesa zao kwani kwa sasa safari hii imetokana na msaada tuu kutoka kwa nchi rafike hapo hamna biashara.
ReplyDeleteSasa na wao inabidi wadai hizo pesa kutoka kwa huyo tapeli wa kiarabu na sio mdomo hivi kwali michuzo siasa zitaisha lini bongo kila kitu uongo tuu
halafu sababu zenyewe wanazotoa ni uongo mtupu mtu huitaji hata kuwa form four.
1. Wanadai wamekosa slot hii bwana si big deal kabisa kwani ngambo kuna air tax sasa kama ao wanaweza kupata within six hours sasa mbona ATC wanaongopa vile vile kungekuwa hamna haja ya kuwa na private jet kama pa kutua ni issue.
2. Wanadai ndege imekataliwa ethiopia na sudani huo ndio uongo mkubwa kabisa kwani kwenye Aviation law kuna kitu kinaitwa International Airspace hiyo huitaji permission from anywhere
sasa huu si utoto
3. Michuzi usinibanie kwani ni juhudi za kuondoa ubabaishaji na kama kweli una mapenzi na nchi weka ili wajue kwamba watu sio mafala kama zamani.
Nyie mnaomshambulia huyo aliyesema tiketi za bure muwe mnasoma vizuri, sio kukurupuka tu. Hata kma maudhui ni mabaya lakini maana yake haikuwa hiyo munayoisema nyinyi.
ReplyDeleteHakumaanisha kupewa tiketi bure na ATC au Shirika la ndege lolote.
Alichokuwa anamaanisha ni mtu kufadhiliwa/kulipiwa safari na mtu mwingine au Taasisi, as opposed to mtu kutoa pesa yake mwenyewe kutoka mfukoni mwake.
Nyie vipi?
CLASS A Airspace
ReplyDelete"Class A Airspace is the airspace from 24,500 feet to UNLIMITED vertically. All pilots flying in Class A airspace shall file an Instrument Flight Rules (IFR) flight plan and receive an appropriate air traffic control (ATC) clearance."
THERE IS NO SUCH THING AS AN 'INTERNATIONAL AIRSPACE'...SIKU HIZI KILA AIRSPACE IKO CHINI YA SOME AUTHORITY...HIZO UNAZOSEMA ZILIKUWEPO BAHARINI, NOT THERE ANYMORE.
Kuna kitu kinaitwa OVERFLIGHT PERMITS.
Kila nchi unayovuka border yake you need to have PRIOR authorization with a PERMIT NUMBER ambayo sometimes wanauliza.
Hiyo class A airspace ndiyo ALL Airlines fly within.
LAZIMA KUWA NA MAWASILIANO NA KILA NCHI UNAYO OVERFLY.
Mipango huwa inafanywa IN ADVANCE by respective Airline dispatchers.
Ukikurupuka na dege la kukodi, inabidi kuanza ku process OVERFLIGHT PERMITS za nchi utakazo overfly.
Nchi nyingine huwa ziko slow in responding/issuing permits.
SLOT is another complex affair when it comes to busy airports during busy times, ukiikosa yako uliyosema utafika na ukapewa inabidi kusubiri ingine depending on traffic.
Private jets pia zinafuata hizi taratibu.
wewe wa Wednesday, December 12, 2007 8:01:00 AM EAT
ReplyDeletehebu acha kumtetea mjinga huyo, unataka kuniambia hakuna Waislam wanaoweza kujilipia mfukoni, bado katema ujinga tu. Hebu sit down and think.
Kabla hujasema jambo lolote lazima ulifikiri kwa kina, sembuse kuandika kwenye Kijiji kama hiki ambacho ni kiini cha habari kwa watu wengi hivi sasa.
ReplyDeleteHuyo mtu aliyezungumzia Bure tukubaliane wote mwanzo wa wazo lake ni dharau na kama mtu hapo juu alipotumia neno la kigeni (Prejudice) kuelezea ugonjwa mkubwa alionao mtu huyo.
Hijja katika uislamu ni moja ya Nguzo kuu. Na miongoni mwa Sharti lake ni KWA YULE MWENYE UWEZO. ilifahamika kwamba kwenda hijja itakua ghali na inaweza kwakwaza baadhi ya waumini si ndio maana khabari ya mwenye Uwezo ikawekwa hapo.Na kwa kusaidia zaidi ili mtu aende Hijja Sharti jingine ni kwmaba lazima ahakikishe Familia yake anaiacha ikiwa na hali bora na wala sio ya kujibana ati kwa sababu labda baba ameenda Hijja
Anaweza kupata tiketi ya Bure, je vipi kuhusu haya masharti mengine? (Tafadhali tafakari hilo)
Uisilamu haujamzuia kama Dini nyingine haujamzuia mtu kujielemisha kuhusu dini husika.Kuna vitabu vingi ambavyo vinaelezea mambo yanayompasa mtu kufanya Kabla ya Hijja.
Ninakushauri uvisome kwa makini badala ya kudharau kutokana na kupata taarifa kwa redio mbao au vijiweni.
Ishaalah Mwenyezi mungu atakufunulia mwanga wa Elimu na siku moja utataka kujua ukweli badala ya kukurupukia mambo.
All in all acheni dharau, wala hakuna mtu anayejua yupi kasaidiwa kusafiri yupi katoa mwenyewe pesa mfukoni kwa sababu kwa taratibu za kiislam mkono wa kulia ukitoa basi mkono wa kushoto haupaswi kujua kilichotelewa. Taratibu hizi ziliwekwa ili kuepuka tabia kama za huyo mdau huko juu na kujionyesha au riya.
ReplyDeleteWote hapo walipo na huko wanakokwenda ni sawa mbele za Mungu. Tuache kashfa na dharau hata kama una uwezo.