Rais Jakaya Kikwete akimwapisha balozi Alex Masinda kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Asia katika Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ikulu dar jioni ya leo.
Jk akimwapisha balozi Anthony Itatiro kuwa Mkurugenzi wa Itifaki ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo. Itatiro anachukua nafasi ya balozi Cisco Mtiro aliyeteuliwa kuwa balozi wetu huko Malaysia. jk ameondoka usiku huu kuelekewa washington dc ambako keshokutwa desembe 13 atakuwa na hafla ya mfuko wa leon h. sullivan ambapo atatumia fursa hiyo kuwaalika rasmi wafanyabiashara na wadau wengine kuhudhuria mkutano wa sullivan utaofanyika mwanzoni mwa mwezin juni mwakani huko arusha na kuhudhuriwa na wamarekani weusi wafanyabiashara na wadau wengine wapatao 3,000

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Itatiro mzee wa Itifaki safi sana. Masinde kumbe alisharudi bongo. Hongereni!!

    ReplyDelete
  2. Michu, kweli huyo ni kikwete kweli? naomba uanaglie vizuri au macho yangu.

    ReplyDelete
  3. KILA LA KHERI JK a.k.a VASCO DAGAMA!!

    ReplyDelete
  4. bongo bwana idara kibao na mambo bado hayaeleweki,ukiuliza hapo wanalipwa kiasi gani utakimbia wakati shule vijijini hazina madawati.

    ReplyDelete
  5. Wadau naomba niulize, Hivi kila Mkurugenzi wa idara ya serikali huwa wanaapishwa Ikulu? Maana naona ikiwa ndo hivyo kiutaratibu basi Rais wetu ana kazi, kutokana na wakurugenzi kuwa wanateuliwa kila siku, hivyo Mh. Rais anakuwa na muda mdogo wa kuwajibika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na sera bora kuinua maisha ya watanzania.
    Ni bora wakurugenzi 'wateuliwa' kukubali madaraka na wajibu wa cheo chake kwa kujibu barua ya uteuzi na sio kuingia ikulu kuapa.
    Mdau
    SeniorJunior.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...