Napenda kuwaalika wadau wote kwenye concert kali sana jumapili hii ya 9 December, 2007 ambayo ni siku ya uhuru.


Welcome all to thank God together for the past 12 months and also for our nation!


All are welcome bila kujali religion, race, sex, color or age. (Michuzi please usikose). Hamna kiingilio.


Hafla hii itakuwa City Christian Centre , Upang, opposite Mzumbe University Dar es Salaam campus. Kwa mlio ughaibuni mda unawatosha kudaka pipa na kuja. See you there.


For more info, contact organizing commette by calling 0713 414508

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. teh teh teh teheh bongo kwa ku catch up....Mmeona kila siku party zinawekwa huku basi mkasema lazima nasisi tuonyeshe tunaserebuka uhuru day...heh eheeeeee

    It cool kuiga mazuri wabeba box tunayowaonyesha...

    Uzalendo huuuooooooo

    ReplyDelete
  2. jamani hizi sherehe za uhuru mijini na ughaibuni sijui mnasherekea nini? wakati maisha kwa watanznia wengi ni suluba tuu hususan vijijini!Angalieni kule kwa mjengwa muone!Gharamazote hizi za kujirusha kusherehekea uhuru/au niseme utumwa kwa umasikini mngezikusanya kila mwaka na kusaidia maendeleo angalau kijiji kimoja kila mwaka ingekuwa bomba zaidi.Yaani ni afadhali kila sherehe popote pale iwe na harambee[fund raiser],halafu mapato yalenge kijiji,kituo cha watoto yatima,walemavu au hata angalau vituo vya kusaidia wazee/wastaafu kwa maana wanaoumia na jua kali/vumbi bongo wengi!
    Wenu,

    Mabox wa ughaibuni!

    ReplyDelete
  3. Wadau wa ughaibuni nadhani hamjaelewa, na wala sishangai. Hii ni ni ibada ya Kumsifu na Kumuabudu Mungu itakayofanyika tarehe 9. Sio kujirusha ka wengi wanavofikiri, kama kujirusha ni kujirusha mikononi mwa Mungu!

    Watu wengi wanashangaa kukuta tangazo hili sehemu kama hii, inaonyesha kwamba Mungu anatupenda jinsi tulivyo ingawa hapendi mambo tuyafanyalo, na anatukaribisha kuja kwake kama tulivo, kazi ya kubadilisha ni ya kwake, our part is to make ourselves available to him!

    Mie nitahudhuria.

    ReplyDelete
  4. Kweli hizo hela zinazotumiwa kufanya sherehe sherehe za Uhuru nk na waBongo walio Ughaibuni zingechangwa na kusaidia kuleta maendeleo vijijini!Tatizo ni kuwa hao watakao kabidhiwa hizo fedha hawatazifikisha kwa walengwa bali watazitumia kuvimbisha vitambi vyao na kujifaidisha!!!Maana hatuna upendo na nchi yetu wala na jamii yetu!Ubinafsi tu baaaaas!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...