LILE DEGE LILILOKUWA LICHUKUE MAHUJAJI KUPELEKA HIJJA JANA USIKU LIMESHINDWA KUONDOKA BAADA YA KILE KINACHOSADIKIWA KUKOSEKANA KWA 'SLOT' AMA NAFASI YA KUTUA HUKO SAUDIA.
HABARI ZINASEMA KUNDI LA KWANZA LA MAHUJAJI LILIISHAINGIA NDEGENI LAKINI SAFARI HAIKUWEZA KUANZA KUTOKANA NA TATIZO LA 'SLOT' AMBAYO MAHUJAJI WETU WALIIPOTEZA BAADA YA NDEGE YA AWALI KUSHINDWA KWENDA KULE KWA MUDA UNAOTAKIWA. HUKO NYUMA GLOBU YENU HII YA JAMII ILITAHADHARISHA KUHUSU HILO...
MSTARI MFU WA MAHUJAJI KUTUA HUKO SAUDIA NI USIKU WA MANANE AMA SAA SITA USIKU LEO. DEGE HILO AMBALO LILIPANGIWA LIPIGE TRIPU TATU KUCHUKUA MAHUJAJI HAO WAPATAO 1,000 LINA UWEZO WA KUBEBA ABIRIA TAKRIBAN 357 HIVI...


Kwani si angerirusha tu na kuenda kutua kwenye other nearest aiport nyingine halafu wakasafirishwa kwa mabasi au treni kwenda huko wanakotaka?
ReplyDeleteHuyo Rubani vipi huyo?
LENA nini?
Serikali imejitahidi kutoa ndege kupeleka mahujaji kusali.
ReplyDeleteswali ni Je ni halali kutumia pesa za walipa kodi kwa masuala ya kidini kama kupeleka watu kwenda hija wakati serikali haina din
sasa ndugu zetu waislam watamulaumu nani tena kwa hili. sababu adui wa mafanikio ya waislam wa tanzania ni wakristu na hao ndio walio laumiwa miaka yote. Mustafa kawa mkristu?
ReplyDeleteMhmmm usitudanganye mwanzoni ulionya juu ya 'float' sio 'slot' sawa? na sisi tulikuangalia tu tukanyamaza kwa hiyo cha kufanya rekebisha mtu mzima.
ReplyDeleteJamani tuache kuangalia hili swala kwa mtazamo wa kidini. Ni kweli kuna watu (waislam na wakristo) ambao wanapenda kuingiza udini katika kila jambo inapowezekana.
ReplyDeleteHapa ni kwamba kuna uzembe somewhere na kuna watu wanakwepa lawama kwa uzembe wao ndio maana inatolewa story mpya kila saa.
Naona kuna mtu au watu wamepewa madaraka makubwa ya kuamua mambo ya ATC lakini hawana ujuzi wa kutosha kutoa maamuzi sahihi. Sasa wameshavurunda wanajaribu kudanganya umma.
Kwamba dhahama ya uzembe huo imewakumba abiria wanaokwenda Hijja isiyumbishe uwezo wetu wa kupembua mambo kwa uyakinifu tukaanaza kuingiza udini. Hii itatufanya tuteleze kidogo katika kuwachambua na kuwaadhibu walioboronga.
MUCHI ASANTE KWA HABARI MAHUJAJI, SASA ZINATOSHA, TUENDELEE NA MAMBO MENGINE......
ReplyDeleteVIPI HALI YA HUYU DIDAS MMOJA WA WALE WAGONJWA WALIOCHANGANYIWA TIBA PALE MUHIMBILI, YUKO INDIA NASIKIA HALI MBAYA SANA.......ANAPOTEZA KUMBUKUMBU,,MBONA HAMSEMI MAENDELEO YAKE JAMANI, ANGEKUWA WAZIRI MNGETUWEKEA KILA KUKICHA, ACHENI HIVYO BWANA, HUYU NAYE BINADAMU.....
wewe mtoa maoni wa 12,2007 10.40 hao watu wametoa pesa zao sio pesa za serikari nashilika la atc nimali ya selekali ndio limewakwamisha wakati pesa wamesha chukuwa tena inatakiwa walipwe fidia kucheleweswa hakuna pesa za walipa kodi nipesa zao wenyewe jinga we
ReplyDeleteIna maana wanatumia pesa ya serikali ama pesa ya baraza la waislamu Tanzania? Naomba mnieleweshe ndugu zangu. Kama ni pesa ya serikali then that's hilarious, unethical and a waste !!!!!!!!
ReplyDeleteWakati hiyo ndege inakuja huku kuchukua watu hilo la slot halikuonekana?
ReplyDeleteMwingine nae anamlaumu Mustafa, kwani yeye ndiye alitakiwa kufanya kazi ya kuhakikisha ndege inakuja TZ kwa wakati huyu Mustafa ni Mfanyakazi wa ATC au? Sijaelewa bado maana naona kuna mwingiliano wa mambo.
Kama alivyosema mdau hapo juu other options ilikuwa in kutafuta kutua kwenye viwanja vingine ambavyo ni nje ya hiyo Miji halafu watu wangesafirishwa kwa mabasi. Lazima tufike mahali tuwe tunafikia nje ya box, au tuwe na plan zaidi ya moja incase plan A ikifeli basi tufuate plan B in case nayo ikishindikana tunafuata plan C.
Hizo kazi sasa waachiwe vijana wafanye, wazee wakapumzike wale pension basi.!! Hii ni era nyingine kabisa!!
ebwana samahanini sana wale waaohusisha masuala ya kidini hapa.Jaribu kutazama suala la hao watu yaliowatokea kwanza.maana huwa mnayaanza wenyewe haya halafu mtakuja shindwa nyinyi hapo haya tuu.sisi tunawaangalia tuu speed zenu hizo za kutaka kutafuta visababu.na huyo alieandika kuwa yeye abubakari nina hakika si abubakari bali ni john au joseph.na kwa nini asiache anonymous kama wengine?kipi kimekufanya uandike kuwa wewe abubakari.anyway endeleeni tuu kuchokoza
ReplyDeleteSlot gani nyie watu wa serikali mnaizungumzia pamoja na ATC yenu?
ReplyDeleteHebu tufafanulie vizuri najua slot yao ilikuwa ni kutua katika Uwanja wa Madina siku hizo walizopaswa kusafirisha hao watu. Na hili lidege linaelekea Jeddah na si Madina tena, mbona kizungumkuti, si bora wangetaka kutua huko huko Madina ambako watu wameshatoka wako Makka tayari, wakawasafirisha watu kwa Mabasi kwenda Makka!
Watanzania msiwe wadini!
ReplyDeleteKuna mtu ameuliza kuwa kwanini serikali itumie pesa kuwasafirisha mahujaji na wakati serikali haina dini? Jibu ni kwamba:-
Organaizesheni zinazoandaa safari za hijja wameingia mkataba na shirika la ndege la Tanzania ATC milikiwa wa ATC ni serikali kwa asilimia mia moja 100% serikali inalojukumu kuwatafutia mahujaji usafiri mwingine kama ule wa mwanzo umekwama. Mahujaji wamekuwa wavumilivu kupita maelezo. Kama umehi kusafiri na ndege kuna sheria inasema ukicheleweshwa safari air line inatakiwa ikugharamie hoteli yaani kula na malazi mpaka utakapo pewa usafiri. ATC imefanya hivyo?je Mahujaji wamefanya fujo kudai hiyo haki yao?Tuwe wazalendo kidogo sisi sote ni watanzania wakristo na waislam si tunaishi wote mitaani?hatukai pamoja kwenye nyumba za kupanga?Sisi ni ndugu zenu msitubague na kutukebehi "mustafa kawa mkristu?" hiyo ni kebehi dhidi ya waislamu. Mimi kama mwislamu mzalendo sipotayari kuona mtu anamtukana au kumkebehi mkristu kwani ni kosa kubwa mbele ya macho ya Mungu. Mungu amesisitiza kuoneana huruma ndio maana ametupa utu akatutofautisha na wanyama.
Tuwaombee mahujaji wapate safari na ni jukumu la serikali kuhakikisha wanapata safari kwani huwezi kutenganisha ATC na Serikali.
Tuwe wazalendo, tupendane na tuipende nchi yetu.
Mungu ibariki Tanzania.
Mohammed
Jamani ndugu zangu waislamu tujalibu kutafakari haya,Hijja ni nguzo muhimu sana kwetu cha maana tujaribu kuangalia tunakwendaje huko?Mimi nadhani haya yote ni ya Allah,nahisi kwenye hilo kundi letu kuna wenzetu ambao si wasafi inavyotakiwa kwa Hijja ndo maana Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehmaa ameamua kutuonyesha,haiwezekani mambo yatuendee kombo namna hii,tujaribu kumrudia Allah kabla hatuja amuua kwenda kukanyaga aridhi takatifu ya Mecca.Ni hayo tu kwa niliowakela itabidi waniwie radhi.
ReplyDeleteNi jambo la kusikitisha sana kwa mahujaji ambao wamepanga safari yao nadhani wengine ni mwaka mzima ili aweze kufika huko kunako hija lakini watu wachache wanafanya mambo ambayo yanakwamisha safari hii ya kiroho,watu wamekaa hapo airport kwa muda mrefu sasa bila mafanikio,na hata baada ya kupata ahueni sasa kuwa wanaondoka na wako ndani ya ndege wanaambiwa mambo si mazuri kwani slots haipo tena sasa hii kali,nadhani vikosi vinavyoshughulika na dharula za huduma ya afya ni vizuri wakawepo hapo masasa 24 ili kuokoa kwa wale ambao si rahisi kuhimili msongo wa mawazo na hata wale wenye shinikizo la damu isije ikawa mambo mengine hapo halafu tukaanza kulaumiana hapo.
ReplyDeletena hata wale wataalam wa saikolojia na nadhani nafasi nzuri ya kufanya kazi ya kuwatuliza watu kisaikoljia kutokana ya yote yaliotekea kuhusu safari hiyo ya Hijja.jamani poleni sana lakini yote ni mitihani ya tu kufikia pepo.Mungu atawasaidia tu mtafika salama.
mlau
We anony wa 2:20 nakupa big up kabisa hata mimi ni islamu nakumbuka nilipokuwa huko nyumbani niliona watu wakienda Hijjah lakini mambo yao mmmmmmmm!Hata mimi nabeba maksi huku kabla ya kurudi home nataka nijiwahi Mecca tujisafishe kabla hatujaamua ndugu zangu kufanya tendo kubwa la kitakatifu kama hili!
ReplyDelete"Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wanawake wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Bibi Aisha Sururu, aliwataka mahujaji hao wasilaumu kwa sababu safari hupangwa na Mungu."JAMANI NAOMBA TUMUUNGE MKONO HUYU MAMA NI KWELI HAYA YOTE NI YA ALLAH!HIVYO HAKUNA CHA ATC WALA NANI HAPA NI ALLAH TU NDIE AJUA.
ReplyDeleteJamani Ndugu zangu waislamu naomba mnisaidie kwa hili. Kwa yeyote mwenye mazo tafadhali
ReplyDeleteIbada ya Hijja kama zilivyoibada nyingine zote nia yake kubwa ni katika kupima imani ya muumin. Kwa kuweka nia ya kufanya jambo fulani la kheri na ukajitahidi kwa Kila uwezo wako kulifanikisha lile zuri ( Ibada) fulani inamaana wewe unalengo kamili la Kuitekeleza Ibada ile.
Hapa nitatoa mfano wa Hadith moja ambayo siikumbuki vizuri ya Malaika wawili waliokua wakibishana kuhusu bwana Mmoja aliyekua akienda kusilimu. Akiwa katikatin ya safari yake yule bwana Umauti ukamfika. ikawa ubishi yule mtu amekufa katika dini gani. Lakini ufumbuzi baadae ulipokuja ikafaahamika kwamba kwa kuwa mtu yule alidhamiria kusilimu na kwa kua alikua ashaianza safari yake kwa umbali fulani kwa hiyo mtu yule alihesabika amesilimu na akahesabiwa miongoni walioongoka( mtanikumbusha vizuri mnakikumbuka kisa hiki).
Na kwa kuwa sisi kama waislamu tunaamini kwamba kila jambo linamipango ya mungu (Kun fa ya kun)
Mimi nilikua nataka kuamini kwamba huenda mwenyezi mungu amepitisha mtihani wake katika kutupima Subra zetu. Na pia nataka kuamini kwamba kwa kuwa suala hili limefanyika huku sisi binadamu tumefanya kila lilowezekana kwa nguvu zetu huwezi Jua mwenyezi mungu ametuepusha na nini au ametupa ujira gani kwa ile nia tuliyokua nayo (wallahu yaalam)
Kwa Hiyo basi mimi nadhani kwa muislam aliyeshiba imani huu sio wakati wa kumnyooshea kidole mtu yoyote na wala si wakati wa kuwapa faida wanaotaka kuchukua suala hili kuthibitisha yale wanayopigia debe(advocate) kwamba uisilamu ni dini ya vurugu.
Hebu tuthibitishe kuwa hilo sio sahihi, na tuonyeshe ustaarabu kamili wa kiislamu kwa kumshukuru mungu kwa mitihani na yale yote alotuepushia. Yeye ndo aliyetupa uwezo wa kwenda Hijja, Kwake yeye ndio tunaomba salama, na kwake yeye wote tutajibu kwa matendo yetu tuliofanya duniani.
Pia mwisho nataka kuamini watu hawa ni sawa tu na waliokwenda Hijja hata kama hawatajaaliwa tena kwenda kwani Nia ilikuwepo.
Wahaadha Salaam
Moh'd usiwe na jazba, aliye uliza kwamba Mustafa ni Mkristu hakumaanisha ku kebehi, kuna tetesi kwamba huoy Musso ndo kaleta kasheshe hili lote , eti walikuwa wametengeneza cha juu kama kilo 2 kwa kila abiria, kwa kutumia AirTZ. Hebu tafute vyanzo vizuri vya habari utaambiwa, pana jambo hapo? Mbona mahujaji wa waliotumia agent mwingine sas wako hija?! hoja no kwamba wa TZ wasidhani dhuluma huangalia dini, mbona hata hao wakristu wanakamua madili juu ya wakristu wenzao?
ReplyDeleteMie namuunga mkono ndugu yangu aliyesema hapo juu, kwa imani ya kiislamu hapo tayari wanahesabiwa kuwa wako Hijja ndio maana hawafungi hizi siku ambazo sie wengine tunafunga, na Mungu hukulipa pale uliponuia kutenda mema hata kama utakuwa umekwazwa kulitenda hilo jambo. Hiyo ni kudra na mwenye kuamini katika kadri basi hana wasi wasi na hayo yanayotokea.
ReplyDeleteNaomba nimjbu aliyesema kuwa wengine si wasafi, ni kweli na moja ya sababu ya kwenda huko ni kwenda kuomba Toba kwa Mungu ili ukirudi basi umetakasika na hutakiwi tena kurudia kutenda maovu, maana yake ni kwamba hijja ni ibada kama ibada nyingine kama kushahadia, kufunga ramadhani, kusali sala tano na kutoa zaka. Na Toba ni ya kila siku ni Mwenyezi Mungu peke yake ajuaye yaliyo sirini ambayo sisi hatuyajui hivyo hatuna haki ya kusema kuwa wameshindwa kwenda kwa sababu ya madhambi yao. Mitihani mizito huwapata wacha mungu wakweli kweli ambao wanafanya ibada zao kiukamilifu ili Mwenyezi mungu apate kuimairisha zaidi imani zao. Nina hakika asilimia kubwa ya hao mahujaji wanazidi sana kwa ucha mungu ndio maana wamekumbwa na hiyo mitihani.
Tumshukuruni Mungu kwa yote kama hayo kuna mtu aliyakusudia basi malipo yake atayakuta huko huko hakuna haja ya kuandamana wala kufanya vurugu yote ni kumwachia Muumba mweza wa yote.
Wakijaaliwa kusafiri yote ni Mungu pia.
Wabillah Taufik.
Habari nilizozipata punde ni kuwa Oganaizesheni hazikuingia mkataba directly na ATC kilichofanyika ni kama lile sakata la radar wakubwa wa ATC wamewadirect waandaaji wa Hijja ( oganaizesheni ) waingie mkataba na Mdosi mmoja anaefahamika kwa jina la Rajan na Rajan yeye ndie ametiliana saini mkataba wa kusafirisha mahujaji zaidi ya 1000 na shirika letu la ndege ATC. Hapa kuna mambo ya 30% za radar kama si 10% namna hii Bongo hatutaendelea maana kila deal muhindi lazma awekwe hivi hii mpka lini?watu hawa wanaoenda kuhiji mwaka huu haijulikani kama mwakani watakuwa hai!wamekuwa wakitunga safari kama mtu atungavyo ushanga for years and years! leo wanadhalilika!wanalala sakafuni wanashindishwa njaa! watu hawa wameacha majumba yao wameacha wake zao wameacha waume zao wameacha misosi yao ya nguvu mnawalaza chini?kweli ATC ilaaniwe. Kina nyang'anyi ni wanyang'anyi kweli kweli!
ReplyDeleteWatanzania wote wakristo kwa waislamu wake kwa waume tulani mambo ya 10% kwa nguvu zote mambo haya yanaigharimu serikali.
Ona sasa kwakua ATC ni mali ya serikali wale jamaa pale wakishitaki wataifilisi ATC na serikali kina Mustafa Nyang'anyi wamesha kula chao raha mustarehe! Hala jamani huyu jamaa wanamngangania tu huyu alikikuwa waziri wakati fulani akanunua kivuko cha pale magogoni kilikuwa kibovu HAKIWAKI! akatolewa u minister akapigwa ubalozi nchi kadhaa amerudi wabongo wamesahau mambo ya kivuko kapewa keki ya taifa na yeye amege. Sio kama hakuna watu ila tumezoe na tutaenedelea kuzoe kuziona sura zile zile leo waziri kesho balozi kesho kutwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi. Kina mwapachu, mungai, zakia, kingunge, kila siku watakuwa mawaziri mtakufa lakini vizazi vyao vitaendelea kuwa kwenye uongozi hawa ni watu wanaojua kuongoza nyie hamjui! wewe unaesoma hii comment unajua kuongoza wewe?acha utani kachunge mbuzi kwenu kijijini waachie wenyewe wenye nchi waongoze nchi yao tena uwache siasa zako za uchochezi!
Nakuja na mpya kuhusu watoto wa vigogo mwanawane kuridhishwa utawala hawa kwa lugha ya mama wanaitwa "ruling clan" kama sio "Royal family"
Tchao
Mohammed
Waislam bwana! Sasa wanataka kichwa cha Mustafa Nyang'anyi, Jasba tu vurugu tu, ni bahati sana Mungu amewaonyesha tena Ndugu zetu waislam kwamba adui wao si mkristu hata kidogo ni wao wenyewe na shule kidogo kichwani. Mungu atazidi kuwaangazieni mpaka kuna siku mtajua tu kweli ni nani hasa alikuwa adui yenu.
ReplyDeletetatizo la waislamu ni shule. period
ReplyDelete