baadhi ya majengo ya kale yaliyojengwa na mwasisi wa jiji la dar sultani seyyid majid wa zanzibar sio tu yangali yanadunda bali pia yamekarabatiwa vizuri na kubeba ofisi kadhaa. hili hapa sasa ni makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya ilala, lile la mbele ni ofisi za habari za umoja wa mataifa na pia makao makuu ya tume ya taifa ya ukimwi

Majengo kama hayo mengi yamekwishabomolewa. Bora wakarabati zilizobaki. Hayo majengo ndo yalikuwa malandmark ya Dar es Salaam.
ReplyDeletewewe muhidin tuondolee udanganyifu wako hapa. Dar ilikuwepo na wa-darisalama waliishi hapa kabla huyo sultani wako hata hajazaliwa. Mambo gani haya mnataka kutuletea hapa.
ReplyDeleteAnon wa pili nashukuru kwa kuliona hilo. Hata mimi nilitaka kumuuliza Michuzi kuwa Je hakukuwa na watu wanaishi hapa Dar es Salaam kabla ya Sultani kufika?
ReplyDeleteIsije ikawa yale yale ya kusema mzungu ndio amegundua Mlima Kilimanjaro wakati Wachaga walikuwepo pale miaka mingi tu kabla ya huyo mzungu.
huu ni UHARIBIFU mkubwa sana wa historia yetu.
ReplyDeleteNilibahatika kwenda Rome-Italy.
Wenzetu huko wana Old Rome na new Rome. Old Rome ni mjini ambako kuna yale majengo ya zamani enzi za wafalme wa kirumi ambayo ni kifutio kikubwa cha Utalii.
Ukiwa mpangaji kwenye majengo hayo unaruhusiwa kuyakarabati KWA NDANI TU kwa namna yoyote unavyotaka lakini SIO KWA NJE. Kwa nje yanabaki hivyohivyo milele.
Majengo mapya na ya kisasa badala ya kubomoa hayo ya zamani, ndio wamejenga huko pembeni mwa mji wa Rome, ndio huko new Rome.
Hivi hatuwezi kuiga mfano huo tuka yapreserve hii historia yetu na ku-avoid Mji kuulundika sehemu moja tu?
Naona Zenji wamejaribu kidogo kuu-preserve ule mji Mkongwe
Acheni ujinga nyie..sasa michuzi amekosea nini? hayo majengo yalijengwa wakati wa sultan majjid hao wazaramo wenu hatukatai walikuwepo ila walikuwa wanaishi nyumba za nyasi !!!!
ReplyDeletemhhh makubwa
ReplyDelete