Makamu wa Rais wa Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, akimkaribisha Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam Makamu wa Rais wa Cuba Mheshimiwa Eseban Lazo Hernandez wakati alipomtembelea leo.
Bwana Hernandez ambaye amefuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rodriguez Costa aliwasili nchini jana usiku na kupokelewa na Makamu wa Rais. Katika ziara hiyo ya siku tano anatarajiwa pia kwenda Zanzibar kesho ambako atakaa kwa siku mbili.
Atarejea Dar es Salaam Ijumaa jioni kuendelea na ratiba yake ambapo Jumapili ijayo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete na baadae jioni ataondoka kwenda Ethiopia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. loh...kibonge hicho!hata wakomunisti mavazi kuiga tuuu...bora Castro na kombat suit!!!

    ReplyDelete
  2. Dah!
    BODIGADI wake mwanamke!
    Kudadadek walaI!
    Kwa hiyo anakuwa nae "kila pahala" anapokwenda!
    Natamani mie ndo ningekuwa huyo Makamu wa Rais!

    ReplyDelete
  3. Da!Mjomba ngoma ngumu kishenzi, je kama kina Guivala wangekuwa hai leo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...