ngoma toka kusini aina ya mganda huenda ndio yenye wachezaji wasafi kuliko zote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi,
    Hii ngoma ya wanyasa ni moja kati ya ngoma za kitanashati hapa nyumbani. Huwa ni burudani tosha uwakutapo wakitumbuiza mahala kwa jinsi wanavyopiga step na mavazi yao meupe na viatu ving'aavyo. Nafikiri ni moja ya vitu vya kujivunia kama waafrika.

    ReplyDelete
  2. Sio wasafi bali ni waNADHIFU.
    Usafi ni dhana pana.
    Kama hapo walipo wananuka vikwapa utasaemaje ni wasafi?
    We vipi wewe!?!

    ReplyDelete
  3. Kama hamelewi mambo jamani muulize kwa wale wanao elewa. Siyo kuzuka tu na maneno yasiyo na maana. Rangi kuwa nyeupe si alama ya nguo kuwa safi. Je unataka kuniambia wanao cheza na maleba meusi (kaniki) si wasafi. Unauhakika gani kama wachezaji hawa wameoga. Naomba usichanganye mabo kwa kuchanganya rangi na usafi. Mimi kama mcheza ngoma huwa navaa maleba yenye rangi kama gunia la katani, lakini ni safi bali kwa mtizamo wako utaniita mimi mchafu. Hiyo ni kasumba ya kikoloni ya kwamba kila kitu cheupe ni safi, ni kitakatifu na cheusi au rangi dhaifu si safi.
    Mtoa maoni!!!

    ReplyDelete
  4. napenda kujua asili ya ngoma hii imekuanzia wapi mpaka wakavaa tofauti na uvaaji wa ngoma za tamaduni nyingi za tz mana naona thokisi na mambuti matai na makalamu hamuna lubega hapo mwanawane.

    ReplyDelete
  5. Ngoma ya kiafrika katika protokol zetu huwa haichezwi hata na viatu, never mind tai shingoni. pumbaf

    ReplyDelete
  6. Hiyo ni ngoma yetu, MUGANDA aka. NGOMA YA BILA JASHO!

    ReplyDelete
  7. Hii ngoma pamoja nakua na utanashati basi hii ngoma haina historia ndefu, kwani kabla ya wamishionari afrika, waafrika walikua hawavai hivyo.

    ReplyDelete
  8. Brother mithupu si mchezo hiyo ngoma yetu kwa watu wenye asili ya kule Mbamba Bay mkoani Ruvuma.... ndugu zangu wanyasa mithupu leo katurudisha nyumbani mambo ya utanashati hakuna kutumia maguvu wala kuchafuka na mavumbi hapo. Mdau UK

    ReplyDelete
  9. Nangombo hoye hoye.Tena babu yangu ndio kihongonzi wa mganda pale nangombo.bila jasho sitepu one sitep two her kamoni.wacha bwana mombo.Vijana wa songea tulio majuu tukumbuke kujenga Ruvuma yetu jamani balabala pale mjini.

    ReplyDelete
  10. MICHUZI WAULIZE WENYE KABILA, KABLA YA WAKOLONI WALIKUWA WANAVAA NINI?

    ReplyDelete
  11. Duh...kombinesheni hatari...kaputula,viatu na hizo kamba za kujinyonga...aa sio za kwetu bwana...hapo kwetu ni ngoma chakacha cha vijiuno na mbele minazi zikijipendekeza...na hayo yote uchi kabisa!!ua vipi?

    ReplyDelete
  12. Basi niwape na angalau wimbo mmoja;

    Tenga tilela malelo
    Magunga afya mwana,
    Mwana ayii kuchihoro
    Kusoko la wahavi
    Kwa Basinyusi Ndifwa

    Ena Dadi
    Ena dadi, ena dadi nileke nakandole mawu

    Ena dadi, ena dadi nileke nakandole mawu

    (Alafu inaanza tiyara baadae lipenenga . Tiyara ni kale katarumbeta kadogo na lipenenga ni yale matarumbeta makubwa ambayo yote nanatengeneza na vibuyu)

    Sasa sijui chemi bado yupo hapo au nimemwacha hoi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...