

Baada ya kila mmoja kujaribu kuendelea na maisha yake,wote (Tausi na Mwalimu Adam)wanagundua kila mmoja bado anacho kitu anachohitaji toka kwa mwenziwake.Kila mmoja anakuwa kujitolea muhanga kuhakikisha anakipata alichokipata kwa bei yeyote.
Je, nani atafanikiwa na nini kitatokea na kubadili mfumo mzima wa maisha ya wawili hao pamoja na wa wote walio wapenda na kuwajali? Haya ndo baadhi ya maswali katika filamu mpya ya Muhanga wa Mapenzi iliyotengenezwa na Nassir Mohamed na iko tayari kuingia mitaani.


Hivi hizi filamu sasa mbona inakuwa balaa, nyie waigizaji mnapata muda kweli wa kukaa chini na kutafakari kweli ah! this is 2 much, kwa soko lipi? hebu tulieni mcheze senema za kueleweka. Tumechoka sasa. Hamkuangalia 'zecomedy' tunataka viwango bwana. wewe ucheze maigizo, wewe ucheze zidi ya senema moja kwa wakati mmoja, wewe mwenyewe uwe director, dereva, mtunzi, meneja wa sakafu, meneja mavazi, masoko khaa, mwee inawezekana kweli kukawa na kiwango hapo? au ndo mnaganga... soo mmezidi mnooo kutukamua kwa visenema vyenu michosho BASI SASA.
ReplyDeleteanon wa hapo juu kweli umechemsha ndugu yangu soko buria siku hizi kama wewe hutaki wenzako wanataka na ukumbue kuwa bla hizo filamu utitili hakutakuwa na maendeleo ya kutengenza filamu kwani hiyo ndio njia moja wapo ya kujifunza na kupata maoni ya watu. kiuwezo bado tuko nyuma na quality watu hawaangalia kwani filamu zenyewe ni low budget haswa. Tutafika mwanzo mzuri taratibu watu watajifunza na kusonga mbele hata mtoto ananza kwanza kutembea mmojawpo akiwa wewe mwenyewe sasa umekuwa unaweza pambanua kipi kizuri na kipi kibaya.
ReplyDeleteNa laiti kama msingekuwa mnabeba kiukoo basi hata hao wasiokuwa na uwezo wangepata hizo nafasi wakasome ili watengeneze filamu nzuri ila sasa undugunaization aliokataa nyerere umezidi wajinga wajinga ndio wanapewa nafasi hizo na wenye vipaji wanazidi kutoweka.
Keep up Nasir najua utafika tu kwani unajuhudi na moyo wa kujituma na usisikie la mtu kwani wabongo dharau ,kejeri,maimango jadi yao hata sikumoja hatawamsifia mbongo mwenzao hata ufanye vizuri au ujitahidi kuonyesha njia wao watasema negative tu Na ndio maana hatufiki popote kwa sababu ya ujinga wa kukandiana na kusiribana.
Mungu ibariki Tanzania
Mzalendo
Nani anakulazimisha kununua.Unataka waombe ruksa kwako wakitaka kutoa filamu.Watu wengine bwana.
ReplyDeleteTuleteeni vikota, misosi na mademu uchi tuu...ngono tupu tuu...mengine tuyaache!!!
ReplyDeleteWewe anon wa kwanza unataka wanunue za Kinaijeria ambazo hata hawaelewi zinasema nini? Hata huko Nijeria, Bollywood na Hollywood kuna sinema zenye standard tofauti kulingana na bajeti.
ReplyDeleteHayo ndio mazoezi yenyewe wacha sinema za kiswahili zimwagwe angalau tupunguze hilo soko la sinema za nigeria, wengine hatuna uwezo wa kwenda jumba la sinema kila siku au kukaa kwenye viti virefu hizo hizo ndio kiburudisho chetu.
Ungewashauri wajifunze zaidi na watengeneze sinema nzuri sio kuwakatisha tamaa eti waache wakiacha watapataje uzoefu au watajifunzaje?
Mcheza kwao hutuzwa na sio kubezwa!
Hiyo ni filamu au mchezo wa kuigiza?
ReplyDeletekaka michu nitumie basi ikitoka..namkumbuka huyu dada aliigiza kny filamu ile ya fungu la kukosa,na kwa kweli namkubali...nitumieeeeeeeeeni basi ikitoka..
ReplyDeleteNey-Bham.