Wadau,
SisiMizi Tanzania Ltd. kwa kupitia SisiMizi International ya New York, inapenda kuwakaribisha watanzania wanaoishi Marekani kwenye "VideoConference Seminar" itayofanyika Dar-es-Salaam, TZ na Washington, DC -USA sambamba tarehe 14 mwezi huu wa 12, 2007 asubuhi saa 2 mpaka saa 3, WorldBank HQ- Washington, DC.
Viti ni vichache, atakaye wahi ndiye atakayepata nafasi.
Wako katika kulisukuma libeneke.
Michael T. Mwakilasa


We Michuzi wewe, we mkubwa sasa. Sio unakuwa kama hawa waandishi wa kizazi kipya.
ReplyDeleteTupe taarifa kamili na sio nusunusu.
Marekani wako nyuma kwa masaa 8 ukilinganisha na Tz.
Sas hiyo saa 2 mpaka 3 ni kwa saa za huku Bongo au Marekani, mbona hujafafanua!?!
We vipi wewe!?!
Na mimi nauliza semina ya nini?
ReplyDeleteNiya lishe bora, ukimwi, online scammers, retirement au...?????Tungeomba maelezo kamili ili niwe na motisha wa kusoma hata hizo link zilizowekwa...
Haya sasa opportunities hizo za kujikwamua kwenye umaskini. Ukijua unataka kufanya nini na hao wakakupa mwanga wa jinsi ya kuexport hizo bidhaa zako naona tutatokal. Mie nafikri wangetangaza kwenye magazeti kuna wakinamama wengi wajasiriamali na bidhaa zao zimekuwa na ubora sasa kuliko mwanzo wanaweza kupata soko huko marekani japo kwa kuanza kidogo kidogo.
ReplyDeletesomeni link mtajua whats all about na time i believe ni New York time (Eastern)
ReplyDelete