rais mpya wa cecafa ambaye pia ni rais wa tff leodegar chilla tenga akipongezwa baada ya uteuzi mchana huu. wengine toka shoto ni makamu wa rais wa tff crecentius magori, katibu mkuu wa cecafa nicholaus musonye na makamu wa rais mpya wa cecafa fadoor hussein

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Pongezi kwa Rais wa Tff chila Tenga kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa shirikisho la Cecafa,tunaamini Tanzania itabadilika kisoka kwa kupitia changamoto la Rais wa Cecafa,tunaomba wadau wote wampe ushirikiano mzuri pamoja na mawozo mazuri jinsi ya kuleta mabadiliko ya soka ya Africa mashariki na katikati,tunaomba Tenga awe muwazi wa kutaka maoni mbali mbali ya wadau wa TZ popote walipo Duniani ili kwapamoja tuwezi kubadilisha sura ya soka ya Africa mashariki iwe na ushindani kama ile ya Africa ya kule juu kichwani na upande wa kushoto mwa Africa hasa pale sehemu ya bega la kushoto pamoja na kifuani mwa Africa ambao wameendelea kisoka,tunamtakia Tenga mafanikio mazuri,kwenu wadau

    ReplyDelete
  2. haki ya nani mimi ni nabii, manake ni siku nyingi sasa ninaona mambo yanayokuja mbele..nliona uingereza akitoka Euro, Richard akishinda BBA hata kushindwa kwa Richa kulikua uchi kwangu...na sasa hili la tenga ndo kabisaaaa limenidhirihishia kuwa mi naweza kuwa nabii flani hv...HONGERA TENGA, naiona Tanzania ikienda south kwenye world cup!!!!

    ReplyDelete
  3. Prof. Pius Yanda wa UDSM

    waTz wenzetu kuwa mshindi mwenza wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu ametoka Tanzania na anaitwa Prof. Pius Yanda wa chuo kikuu cha Dre es Salaam. Hii nondo ni kubwa ila imepita kimya kimya sana jamani. US AlGore amekaribishwa ikulu kwa Bush, tunakumbuka mapokezi wa Prof. Wangare Mathaai Kenya. Tanzania tunawaza nini jamani?,Huyu si Bongo Celebrity pia? Ni wazo tu"

    ReplyDelete
  4. Hivi wewe michuzi
    mbona siku hizi umekua mvivu hivyo?
    yaani huongezi hata picha na matukio mara kwa mara
    umeishiwa nini? picha hizo hizo for the last 24 hrs.
    changamka kaka.

    mdau canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...