mama wa kwanza salma kikwete akifungua tawi jipya la premier lilimo katika jengo la mnara wa benjamin mkapa a.k.a mafuta house jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kwanini hawa wanawake "vingunge" wengine hawavai kama huyu mama Kikwete?

    ReplyDelete
  2. wanawake vingunge wanajifanya eti wazungu...kwa kweli Mama K ameweke precedent nzuri - "she is truly Tanzanian/african".

    ReplyDelete
  3. Michuzi,toa hiyo luhga ya Kirusi kwenye sehemu ya maoni!

    Staili nzuri! Lakini hicho kitambaa...wakati mwingine, kitenge au khanga, ni lazima kuvaliwa toka begani! Kwa nini wasijifunge kiunoni?

    Wabunifu, changanya kidodo staili ya kimono na ile ya akina mama wa Ki-Ganda!

    ReplyDelete
  4. Halafu hizo alizojitandia si kanga tu za kawaida hizo? Nyingine kajifunga kilemba. Amependeza hasa. Lakini siku hizi hata mama Lowassa naye anavaa mavazi ya kiafrika, sijui wa mama wengine mawaziri. Wao ni vioo wakivaa na wamama na wadada zetu wengine nao wataiga watavaa. Huo ndio uzalendo, na kukunwa na uafrika na utanzania wako.

    ReplyDelete
  5. kwa anonymous wa 5:48:0

    jibu la swali lako ni rahisi sana, mama Kikwete anavaa hivyo kwa vile ni mwalimu aliyesoma zamani na anayefuata maadili ya ualimu. ukiangalia walimu wanaofuata maadili, siku zote wanavaa kwa kujiheshimu sana. hata ukienda UDSM wanafunzi wa kike wanaosomea ualimu utawafahamu haraka sana kutokana na jinsi wananavyovaa tofauti na wengine wengi, japokuwa kuna wachache wanaoshindwa kujiheshimu, lakini wengi wanajitahidi.

    ReplyDelete
  6. for shizzle she looks gorgeous n marvellous.........Mama endelea hivyohivyo!!!!!
    cheers, mama maendeleo here!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Hehee umenikumbusha Tulivyo kuwa tunangolewa meno chuoni kwa wimbo wa haiba ya ualimu

    ReplyDelete
  8. Mbona mnataka akina mama wavae ki-afrika na hiyo mizee ya kiafrika mbona imejitwika mi suti kama mizungu myeusi? Na yenyewe ivae kiafrika.

    ReplyDelete
  9. Swala siyo mavazi ya heshima peke yake. Hata wazungu pia wanayo mavazi yao ya Heshima. Tunataka yawe ya heshima na pia ya kiafrika.

    ReplyDelete
  10. hayo mavazi aliyovaa hayafai ktk mazingira ya kazi ambapo inabidi uwe comfortable na flexible.

    kijijini kwetu kinamama wanapokwenda kulima hulazimika kuvaa SURUALI.

    SURUALI ndiyo vazi linalofaa kwa wachapa kazi.

    she is a 1st lady kwa hiyo she can afford kuvaa vitenge na kanga.

    ReplyDelete
  11. First lady,mama tunakufagilia waaaawaaaa uko vizuri,unajua kuvaa na tunakukaribisha sana London kwani unawakilisha vizuri wamama wa Tz.Viambie hivo vimama vinavyopenda suits hatuvipendi.tunakupenda mama yetu unavaa tunavyopenda.Keep it up,unatuwakilisha vizuri mama.well done mama kikwete.

    ReplyDelete
  12. The mamas we love u throughout ughabuini.tunakupenda sana kwani unavaa kama wamama wa kiafrika asili.Keep it up First Lady Mama Salma Kikwete,u know how to do it it the right way.

    ReplyDelete
  13. very inspiring to our mothers manake kuna wa mama wengine pajaz utakuta zote nje huyu mama anajiheshimu sana na ataendelewa kuheshimiwa.represent mama kikwete au vipi

    ReplyDelete
  14. Inavyoonekana Mama Salma is the real 'PRESIDENT'!!!

    ReplyDelete
  15. Katiba inamruhusu first lady ku-assume executive responsibilities?

    ReplyDelete
  16. we michuzi acha kutu take for granted,unasema mama anafungua tawi la premier,hiyo 'premier'ndo nini,ni tawi la benki,bima,kijiwe cha paparazi au kitu gani?fafanua mjomba tena haraka kabla hatujakufunga tairi shingoni.

    ReplyDelete
  17. Nashukuru mtoa maoni mmoja kanifurahisha kajua siri ya mama yetu.kwa sisi walimu TUNAIITA MWALIMU HAIBA.Mama kwenda ikulu bado hajaacha ualimu.watoto wake bado wanamwangalia yeye bado ni kioo tangu zamani hadi leo tungeshangaa mwalimu ambae angebadilika tu kisa kaingia ikulu.Thank you mother UNAWAKILISHA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...