NAPENDA KUBANDIKA PICHA HII YA MTO RUVU UINGIAPO BAHARINI KAMA ISHARA YA KUTOA SALAMU ZA MSIMU KWA WADAU WOTE WA GLOBU HII NA KUWATAKIA IDD EL HAJJ NJEMA PAMOJA NA KRISIMASI NA MWAKA MPYA. PIA NAKARIBISHA PICHA NA SALAMU ZA MSIMU TOKA POPOTE DUNIANI ILI KUTAKIANA HERI.


NAWASHUKURU WADAU KWA USHIRIKIANO MNAONIPA KWANI NAJIHISI NINA DENI KILA NIAMKAPO. NAAHIDI KUENDELEZA LIBENEKE KAMA KAWAIDA NA BILA KUCHOKA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi,
    Kwa wanajiografia, hii ni zawadi muhimu. Kwa kiingereza mto ukifanya mizunguko ya aina hiyo huwa wanasema "The river is Meandering". Tunashukuru kwa kututoa tongotongo nakutupa zawadi hii halisi.

    Merry Xmas

    ReplyDelete
  2. Sawa. Ila mwaka ujao jitahidi UBADILIKE.
    Tabia yako ya kubania koments za watu bila sababu za msingi sio nzuri na haikubaliki kabisa na jamii ya watu waungwana.
    ACHA hizo mwaka ujao!

    ReplyDelete
  3. Sawa. Ila mwaka ujao jitahidi UBADILIKE.
    Tabia yako ya kubania koments za watu bila sababu za msingi sio nzuri na haikubaliki kabisa na jamii ya watu waungwana.
    ACHA hizo mwaka ujao!

    ReplyDelete
  4. Amaaa!!! huu sio Rufiji???

    ReplyDelete
  5. aah hpo kwenye river meander, deposition ya organic materials/debris ikifanyika inatokea Ox bow lake.
    Eid alhaji,X mas & new year njema wadau wote.
    Nawatakia afya njema na kila la heri kwenye shughuli zenu.
    Tupendane

    ReplyDelete
  6. Nawe pia bro.nice view inanikumbusha kabla babu hajafariki tukienda mashambani msambiazi tulikua tunakatiza mito midogomidogoinayomwagwa na mto ruvu,tope kibao ndala zinatengeneza blocks za tope jekunduuuu raha sana oh Tanzania nchi nzuri sana afrika.

    ReplyDelete
  7. shukrani kwa salamu bwana michu ila mie bado nina uchungu na zile dola mia 5 zangu za man utd na arsenal....vipi tenaaa?tulishapangia budget atiiiii

    ReplyDelete
  8. halafu michu nshakushtukia watu tukicomment abt lile shindano la arsenal na man utd wazibania comment sasa ndo tujue mambo holaa ama??si utangaze tuu tujue moja?!
    na hii tena utaibania ila ujumbe si umeupata?

    ReplyDelete
  9. Sasa mto huo mbona mchafu? au hii ni hasara ya kukata miti mwituni!!!na kusababisha mmomonyoko wa udongo...simpo sayansi!

    ReplyDelete
  10. Wewe nanihii hapo juu na River meander zako..hiyo ni Geography ya form one...sasa inatusaidia nini kujua river meander, deposition na ox-bow lake kama hatuwezi hata kuyakinga hayo maji mpaka yanaishia yote baharini? Tunakufaje na ukame na mto mkubwa kama huo unaishia baharini? Nafikiri usomi wako ungekuwa wa maana kama ungezungumzia njia za kukinga hayo maji msichote maji kwa ndoo maili nzima...mshamba wewe...!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...