TIGO WAMEKUBALI KUFADHILI ZAWADI YA MDAU ATAYEKUWA WA MILIONI 3 AMBAVYO NDIO KUSEMA DOLA 500 KWA MDAU HUYO POPOTE ALIPO DUNIANI NOTI HIZO HAPO JUU NI ZAWADI YAKE. KAZI KWENU WADAU WATUKUFU...

BURUDIKENI BASI NA NGOMA HII YA AKUDO TOKA KWA MDAU PIUS MIKONGOTY KWA KUBOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. mr michuzi kipato kitatoka au itakuwa kama ile habari ya washindi wa mpira?anyway hongera kwa yoote !hapa kwenye site yako wanapitia watu zaidi ya hio hesabu yako kwa kua ni nzuri sana.

    ReplyDelete
  2. Duuh hii kali dollar 500 ndio milioni3 ya tz mimi naona michu umekosea mahesabu dollar 500 hata milioni 1 ya kitz haifiki labda umepiga hesabu ya franga ya congo.

    ReplyDelete
  3. infamoustz@gmail.com, najua nitaibuka kidedea, kwa hiyo KUMBUKA HIYO EMAIL !

    ReplyDelete
  4. Asante sana tigo, mimi lazima nishinde huo mshiko.

    ReplyDelete
  5. Ni veme kusikia tigo wamefadhili zawadi nzuri kama hiyo. Waambie tunawashukuru. Na Michuzi pia kuonyesha shukrani hilo tangazo lao hapo juu li link na website yao maana limekaa kama picha tu.

    E-Adverts allow users to interact. Hili mbona haliko active au bado liko under constraction?

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi,

    Habari kutoka Gwangju, Korea ya Kusini. Wadau wa huku walikuwa wanakumbushia kuhusu kalenda ya mwaka 2008 kama iko tayari na imebaki kwenye mgao.

    Wassalaam,
    Omar.

    ReplyDelete
  7. Michuzi mimi ndio mdau wa million 3 hapa ISIMIKINYI@YAHOO.COM

    ReplyDelete
  8. Watu wengine bwana,

    Yan hata hawasomi msg izuri na kukurupuka kujitia kujua na kujibu jibu wasivyoulizwa,

    We mdau wa Friday, January 18, 2008 12:54:00 AM EAT, Wapi michuzi aliposema olla 500 ni sawa na Mil 3???,

    Inaelekea hata ujui kinaendelea nini. Halafu ndo unaota ndoto za kuibuka mshindi, thubutu.

    Hiyo ngoma inaenda kwa shqeir81@hotmail.com

    ReplyDelete
  9. kila la heri kwa wadau wote, na mimi nikiwemo!!

    ReplyDelete
  10. Samahani kwa kupindisha maada halisi, lakini hii kitu hapa chini imetulia sana. Wakina dada zetu wote mngekuwa na guts kama hivi, mngefurahisha sana.......

    Amng`ang`ania mbakaji hadi alipokutwa na polisi

    2008-01-18 08:56:15
    Na Aisha Hamza, PST Arusha


    Msichana mmoja ambaye anadaiwa kubakwa na dereva wa teksi, juzi alifanikiwa kumng`ang`ania mtuhumiwa wake hadi polisi walipofika eneo la tukio na kumtia mbaroni.

    Msichana huyo (jina limehifadhiwa), mwenye umri wa miaka 19, anadaiwa kubakwa na watu wawili akiwemo dereva wa teksi aliyokuwa amekodisha.

    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Basilio Matei alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku na kwamba msichana huyo ni mfanyakazi katika kiwanda cha A to Z kilichopo Kisongo, jijini hapa.

    Akisimulia mkasa huo, Kamanda Basilio alisema msichana huyo alikodi gari hilo lenye namba za usajili T 490 AGJ aina ya Toyota Mark II ili limpeleke nyumbani kwake.
    Alisema ndani ya gari hilo, kulikuwa na dereva pamoja na mwanaume mwingine.

    Alisema walikwenda umbali kidogo na makazi ya watu na ndipo dereva huyo na mwenzake, walipomgeuka msichana huyo na kuanza kumbaka kwa zamu.

    Hata hivyo, alisema kwa ujasiri mkubwa, msichana huyo alishikilia usukani wa gari hali iliyosababisha liingie katika mtaro.

    Kamanda Matei alisema baada ya tukio hilo, mmoja wa wanaume hao, aliamua `kulala mbele\' huku akimuacha msichana huyo akiwa ameng`ang`ania shati la dereva.

    Alisema akiwa katika hali hiyo, kwa bahati nzuri polisi walitokea eneo hilo na kumtia mbaroni dereva huyo.

    Kamanda Matei alimtaja dereva huyo kuwa ni Jackson Simon (32), mkazi wa Kijenge.

    ``Kwa hakika msichana huyo alikuwa jasiri sana kwani juhudi zake za kuushikilia usukani, ndizo zilizowezesha gari hilo litumbukie mtaroni na kukamatwa kwa mmoja wa watuhumiwa hao,`` alisema Kamanda Matei.

    Alisema msako mkali unafanywa na polisi kuweza kumkamata mtuhumiwa aliyekimbia na kwamba dereva huyo yupo chini ya ulinzi kwa mahojiano na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

    Katika tukio lingine, mtuhumiwa Kalili Saloya (26), mkazi wa kijiji cha Kisangiro (Digodigo), wilayani ya Ngorongoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) ikiwa na risasi 20.

    Kamanda Matei alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya mchana eneo la Oldonyosambo, ambapo polisi walimkamata mtuhumiwa akiwa na bunduki hiyo yenye namba MZQ-A 526352 anayosadikiwa kutumika kufanyia uhalifu.

    Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na raia wema kutoa taarifa polisi.

    Hata hivyo, alisema mmoja wa watuhumiwa hao alifanikiwa kukimbia na polisi wanaendelea kumtafuta.

    ReplyDelete
  11. Aisee Michuzi, naiwania sana hiyo dola 500; naona nimeishaipata tayari, Amina!!!!

    kashooke@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  12. Asante kwa kazi nzuri Michuzi! Safari iliyopita nilikosa kidago sana. Nilikuwa miongoni mwa zile email mbili zilizoambatana na mshindi. Nadhani safari hii itakuwa yangu. rdor7819@hotmail.com

    ReplyDelete
  13. hongera kwa kazi nzuri kaka!!

    ReplyDelete
  14. Kaka heshima yako. samahani sana kwa kuingilia utaratibu lakini nina shida ya kupata email ya Pius Mikongoty naomba kama kuna uwezekano umpatie address yangu. ndaniyaluv@yahoo.com. usishtuke haya yalikuwa mabo ya mr paul nipo ndani yaluv miaka ileeeee ya Zewena. Mr Paul. Sydney, Australia.

    ReplyDelete
  15. $ 500 hii hapa mazee...Chomeka email hiyo,

    samchom@gmail.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...