
shirika la ndege ATC limeanza kuota mbawa zake lenyewe baada ya kuwasili ndege moja kati ya mbili ilizonunia kanada kwa jumla ya dola milioni 16.2. ya kwanza ilowasili leo ni aina ya Bombadier Dash 8 Q300 yenye kubeba abiria 50. Jumapili inawsili Bombadier Dash 8 Q400 yenye kubeba abiria 74.
kwa mujibu wa bosi wa atc ambaye alianza kushika nafasi hiyo mwezi february mwaka jana, ndege hizo zitaanza na safari za ndani kwenda kigoma, tabora, shinyanga, zanzibar na dar na baadaye ziteenda dodoma, songea na sumbawanga.
mataka amesema lengo la shirika ni kuwa na ndege 9 zake lenyewe ifikapo mwaka 2012, ikiwa ndege tano kubwa kwa safari za masafa marefu na nne ndogo za masafa ya kati. hivi sasa shirika lina boeing 737-200 mbili za kukodi, na inatarajia kukodi zingine mbili mwezi ujao kwa safari za dubai kupitia muscta na sauzi, pamoja na china.
LoI inaitwa Air Tanzania Corporation ATC sio Atc inaleta other meaning na sio kanada ni Canada au jamani nani anaedit hizi up dates kabla ya kuzileta hewani masudi nini?
ReplyDeleteMichuzi na wewe muoga wamekutishia wasijua kitu hapo na wewe ha well its true sky hawakurudia ila news zote kuna picha hapa UK na he will be back in 9 month fully fit ila hapa mnaweza kuona huyu mjinga alivyotuumizia kifaa chetu
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=I50-TwVCQ1s
Get well soo dudu and God bless ya. wanaotaka kumtumia salam za kupona haraka waingie hapa http://www.arsenal.com/article.asp?thisNav=news&article=488082&cpid=703&title=Over+12,500+messages+of+support+for+Eduardo
salamu zitawekwa kwenye kitabu na atapewa Dudu himself
Imao
Mage umerudi tena ndugu yangu, unatafuta kitu gani hasa? wa edit kwani hili gazeti la serikali? Mbona unatukwaza? Sasa wakisha edit si ndio utamu wote utaisha? Siye tunafuata hiyo chachandu ya ndimu na pilipili humu tulie mihogo yetu ya kukaanga sasa wewe unataka mambo ya editing tena lol? Hivi ulisomaga shule gani isiyojua sense of humour jamani? Kama ukitaka edited news nenda BBC, CNN, ITV, TVT, na kwenye newspapers hili sio gazeti la serikali ndugu yangu na halina edita! Waandishi ni sisi wenyewe na mwandishi mkuu ni huyo Michuzi tunajiedit wenyewe!!
ReplyDeletejee hiyo ndege ni ya mwaka gani maana tunajua mpya kabisa haifiki 20mUSD,angalia hapo chini
ReplyDeleteBombardier Dash Q300
A 56-seat short-range passenger plant built by the Canadian company Bombardier. The plane went into production in 1986 and made its first flight in 1987. The Q300 model is part of the Dash 8 series, which includes the 37-seat Q100, the 29-seat Q200, and the 78-seat Q400.
Its maximum takeoff weight is 19.5 tons, and it has a cruising altitude of 528 kmph. The Q300 has a range of approximately 1,500 km (with modification, it can reach 2,000 km) and is powered by two Pratt and Whitney PW123B turbojet engines. Its wingspan is 27.5 m and its length is 25.7 m.
To date, the company has taken approximately 220 orders for the Q300 (overall, 740 planes have been ordered from the Dash 8 series). One Q300 jet costs around $17 million.
Haiwezekani!!! hiyo ndege au kipanya cha bombom-kijiwe samli! mbona viti vyake vidogo na vifupi kama vigoda!!! Mh, labda macho yangu tu ila all in all hongereni kwa kuwa na ndege zenu wenyewe, nafahamu hata mtoto huanza kwa kutambaa, hutembea na mwisho hukimbia.
ReplyDeleteMweeh! We Michuzi!
ReplyDeleteMbona rangi zake ni tofauti na zile ulizowahi kuonyeshaga siku za nyumba kwenye Mchoro wa Nembo ya ACTL?
Au wamebadili tena?
Hongereni ATC kwa kuwa na chenu!!But kitadumu
ReplyDeletekaka michu.. hiyo ndege ya ATC imeletwa na capt nani? si mtuwekee humu globuni picha yake..au ni mzee checks?.. hongereni ATC, kwani haya ni maendeleo kwa taifa lote.
ReplyDeleteeline
Aaaah... hivi bado hizi ndege za propeller zipo?? Mi nilidhani tuko kwenye era ya Jet.
ReplyDeleteMichuzi:ATCL website yao haifunguki yapata kama miezi mitatu hivi(Najua wadau wengi hawaingii kwenye hii website yao),wanao wanai-restructure kutokana na 'rebranding ya shirika.
ReplyDelete2:Kama kuna mdau wa ATCL atasoma hii comment awapeleke kilio ofisini kwao.KUNA TATIZO LA USAFIRI KWA WATANZANIA WALIOKO DRC,JIRANI ZAO WANATESA KWA KWENDA MBELE.ANGALIA HII(Mfano)-ILI UTOKE LUBUMBASHI KUJA DAR,INABIDI UPITE NAIROBI.WANATURUSHA JUU YA ARDHI YA TANZANIA HADI NAIROBI,TUNNAIONA MIKOA YA SINGIDA,ARUSHA,KILIMANJARO!.HALAFU NDIYO WANATULETA DAR!!MBAYA SANA WAKIVUKA ANGA YA TANZANIA KUINGIA KENYA,WANASEMA HIVI"SASA TUNAINGIA KWENYE ANGA YA KENYA,UKIANGALIA KULIA KWAKO UTAUONA MLIMA WA KILIMANJARO"!!Kwa heri kwa leo.
Nje kidogo ya mada samahani sana michuzi.Community airlines kuna nini au mkwara wa mrisho umewashtua(Ama biashara au Siasa,siyo vyote kwa pamoja!!)
ReplyDeletehee ndo Captain mswati(CAPTAIN JAFARI LILLA)alienda kuichukua hiyo..huyu captain bwana maana kila akiongezwa cheo anaoa,waswahili bwana.
ReplyDeleteWakati majirani zetu Kenya na Ethiopia wanakimbizana na world-class airlines, sisi tunahangaika kuweka "vipanya" hewani, LOL! Afu tunajisikia faraja wenyewe, aibu bwana tusidanganyane hapa.
ReplyDeleteKama vipi vipige ruti za Mwenge -Posta, au mpya ya Feri - Kigamboni...
Salut Misupu!
Captain Lilla alienda kuichukua
ReplyDeleteinatosha kabisa kwa safari za nchini, itasaidia kufungua utalii na usafiri kwa mikoa muhimu kama vile Rukwa,Kigoma,Bukoba,Mwanza n.k. lazima tuanzie mahali,chote chote kile kitasaidia kufungua nchi mahiri kama bongo,nadhani hatutarudia makosa ya miaka 1980s, ndege mbovu zilinunuliwa wananchi wakaambiwa ni mpya, wafisadi augustine mwingira!!!!
ReplyDelete