
KALALA MBWEMBWE, MWANAMUZIKI MKONGWE ALIYEPATA KUTAMBA NA MAQUIS DU ZAIRE, SAFARI SOUND NA TANCUT ALMASI, AMEFARIKI JIONI HII HUKO IRINGA.
KWA MUJIBU WA KIKUMBI MWANZA MPANGO 'KING KIKI', HABARI HIZO, AMBAZO ZIMELETWA KWA SIMU NA KUPOKEWA NA MWANAMUZIKI KABEYA BADU JIJINI DAR, ZINASEMA KALALA MBWEMBWE AMEFARIKI WAKATI AKIFANYIWA UPASUAJI.
MIPANGO YA MAZISHI, KWA MUJIBU WA KING KIKI, INAFANYWA HUKO HUKO IRINGA AMBAKO MAREHEMU AMEJIJENGA NA FAMILIA YAKE.
MAREHEMU KALALA MBWEMBWE AtAKUMBUKWA KWA SAUTI NZURI NA USTADI WA KUTUNGA VIBAO KAMA 'FANTA WANGU' (ALIFANYA ZING ZONG), 'SAZA, MTOTO WA MAMA' (NA MAQUIZ) PAMOJA NA 'HAMISA' (SAFARI SOUND NYINGINE KIBAO.
Mola aliyemleta duniani Kalala Mbwembwe, hatimaye amemchukua.
ReplyDeleteMola ilaze pema peponi roho ya Marehemu. Amen.
Huyu Kalala Mbwembwe ndio Hamza Kalala Mbwembwe? Unatuchanganya wadau
ReplyDeleteTHANKS FOR GOOD TIMES! R.I.P
ReplyDeleteNimesikitishwa sana na kifo cha Kalala maana alikuwa jirani yangu hapo Miyomboni Iringa,akiwa anamiliki Mgahawa unaitwa Suudia karibu na Msikiti wa Ijumaa.
ReplyDeleteKweli huku ughaibuni tunamiss mambo mengi ya home.
Nimestushwa sana na kifo cha kalala.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu Amweke pema peponi. Amen
Mungu amuweke peponi amina.
ReplyDeleteMzee Michuzi unaonaje breking nyuuz kama hizi tuziite tu "brekin nyuuz" badala ya "breking nyuuuuuuzzzzz" maana brekin nyuuuuuzzzz inasound kama vile tunashangilia kitu fulani hivi!it just sounds that way to me personally, lakini kama kwa wengi inaonekana easy tu basi hamna noma tuiache hivyo tuendelee.
Bwana alitoa na bwana alitwaa jina la bwana libarikiwe,mungu alilaze roho yake mahala panapostaihili..mdau Norway
ReplyDeleteMungu Amlaze Mahali pema peponi,Ameni!Sisi wapenzi wa muziki wa dansi tutaendelea kumuombea kwa Mungu na kumkumbuka kutokana na vibao vyake vilivyoshika chati sana ktk muziki wa dansi TZ,namkumbuka sana alipokuwa akitumbuiza pale Iringa Luxury Bar akiwa na Makosa Band enzi hizo tunasoma pale Tumaini University!
ReplyDeleteNakumbuka jina la Hamza Kalala... nyimbo sikumbuki sana lakini hili jina lilikua very popular nikiwa std 1 or 2 hivi...
ReplyDeleteMay Gor Rest his soul in peace. Poleni wafiwa.
Ndugu anony,huangalii picha...huyu sio Hamza Kalala. Michuzi amesema anaitwa Kalala Mbwembwe, sasa wewe limekujia jina la Hamza Kalala, mbona halikukujia la Suleiman Mbwembwe au kwakuwa ni marehemu nae.
ReplyDeleteKaka Michuzi tunaomba uhusiano wa huyu ndugu yetu marehemu na Hamza Kalala au marehemu Mbwembwe S...plz.
Apumzike kwa amani!
Huyu si HAMZA KALALA bali ni KALALA MBWEMBWE.
ReplyDeleteMichuzi umeruka bendi moja ambayo mbali na Marquiz ni M.K Gouup ngoma za magorofani enzi zile pale New Africa iliyompa umaarufu zaidi na wimbo wake wa YU YU wakati walipo team na Kina Kasongo Mpinda, Mbombo wa Mbomboka Mafumu Bilali Bombenga marehemu SIDI MORRIS. Na kwa faida ya wadau hapo juu Kalala Mbwembwe ambaye asili yake ni Mzaire au Mcongo hana uhusiano wowote na Hamza Kalala aliykuwa Vijana Jazz ambaye ni Mbongo halisi
ReplyDeleteNimehuzunishwa sana na habari za kifo cha Mwanamuziki mkongwe mpendwa ndugu yetu Kalala Mbwebe aliyeng'ara sana alipokuwa na MAQUIS,SAFARI SOUND,MK,TANCUT ALMASI ORCHESTRE na mwishoni akiwa na bendi yake Jijini Iringa!Rambirambi zangu za dhati ziifikie familia yake Mjane na Watoto vijana wake,Wakazi wote wa Iringa,Wanamuziki wote wakongwe nchini ambao watakuwa wameguswa sana na msiba huu,Kina KING KIKI,ASSOSSA NA WENGINEO,WAPENZI WOTE WA MUZIKI WA DANSI,hatuna la kufanya yameshatimia,ndivyo Mungu alivyopenda yawe,sote tuko njiani.Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi,amen!
ReplyDeleteASANTE SANA MICHUZI KWA TAARIFA HII.
ReplyDeleteNI VIEUX WANGU HUYO.
NA NI MKASAI MWENZANGU.
LAKINI ANAITWA "KALALA MBWEBWE" SIO "MBWEMBWE".
K.
Kifo kinatisha lakini ni kawaida. Mungu ailaze maala pema roho ya marehemu. Nakumbuka kile kibao chake: "Saza ehee Mtoto wa Mama ah," Then General Nguza analiporomosha lile gitaa la nyuzi nzito, talalalala talalaa talalala...dah ulikuwa utamu kweli enzi zile.
ReplyDelete