MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM MHESHIMIWA BENEDICT NANGORO AMESHINDA KATIKA UCHAGUZI HUO MDOGO ULIOFANYIKA JANA WA JIMBO LA KITETO KWA KUJIPATIA KURA 21,506 DHIDI YA MPINZANI WAKE WA KARIBU MH. VICTOR KIMESERA WA CHADEMA ALYEPATA KURA 12, 561, KWA MUJIBU WA HABARI TOKA HUKO KITETO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Mi ni mmoja wa watu waliopinga/kutombendezwa na uteuzi wa Andrew Chenge kwenye baraza la mawaziri. Huyu mheshimiwa ndiye aliyependekeza sheria mbovu katika uchaguzi kama ile ya kuitambua takrima aka rushwa halali. na ile ya mgombea anayepinga matokeo kulipa 5mil ili kupata haki yake. Kwa mtaji huu wataendelea tu kushinda kwa kutumia sheria hizo mbovu.

    ReplyDelete
  2. Mwanakijiji najua habari hii sio nzuri kwako, Pole sana. nakupongeza kwa jitihada ulizoonyesha katika kipindi hiki cha kampeni. My message to you and other CHADEMA or opposition supporters is --- to a determined, there is nothing as a lost fight.Just unacomplished struggle --- keep moving.

    ReplyDelete
  3. Mwanakijiji kafanya nini? Kada Zemarcopolo hongera kwa kupata ubunge! Usinisahau tu katika enzi zako.

    ReplyDelete
  4. kidumu chama cha mapinduzi

    ReplyDelete
  5. HELICOPTERSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS!!

    Watu wanataka maendeleo nyie mnashindana kwa magari na helicopterss!!! Dah huo mwaka 2010, tutayaona mengi mradi msitoane macho tu! He kumbe na nyie wavulana wa Mzumbe ni wanachama wa Chademaaa!! Uuwii Yesuu na Maria sikujua kama ni nyie ni memba babaangu eeh!

    ReplyDelete
  6. Michuzi hizo namaba umetoa wapi au na wewe unataka kuwa Kivuitu?

    ReplyDelete
  7. Mimi nachukia sana tu Tanzania wanavolable vyama vingine kama vyama vya upinzani!!!! Upinzania na nani? Mimi naona vyama vingine nikama CCM tu vyote vinasuppose kuwa na majina yao tu sio vyama vya upinzani. Kwani nani anampinga mwenzake.

    Natumaini kila chama kila stand na beliefs zake sasa kwanini kingine kiwe cha upinzani??? Kwani ukiwa hubelieve sera za CCM basi wewe ni mpinzani...why...????

    USA wana 2 major parties lakini wana kama 10 vidogodogo lakini husikii hata siku moja oh chama cha upinzani. Upinzaniana nani?


    Hii kasumba ya TZ ibadilike hamna anayempinga mwenzake ila kila mtu anastand na believe zake...Sijui za CC ni zipi?

    Naomba kuwakilisha by the way mimi sina chama hivyo msiiniite chadema hapa...

    ReplyDelete
  8. "Chama chetu cha Mapinduziii chajenga nchiii(Itikia Michuzi kada mkubwa wee),Nyereree..aaaaah,....aaaah.

    ReplyDelete
  9. Binafsi sikufurahishwa hata kidogo kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi Kiteto.Siyo kwamba naichukia CCM au kwamba naushabikia upinzani au ushindani.Hata kidogo.Kinachonitia simanzi ni jinsi Watanzania tunavyo endelea kutoa mfano mbaya kwa nchi zingine za Afrika katika masuala ya uchaguzi wa kidemokrasia.Bila shaka wenzetu Kenya walikuwa wakifuatilia kwa karibu sana ili waone jinsi uchaguzi huo mdogo utakavyo endeshwa liwe kama funzo kwao katika matatizo ya kisiasa yanayo wakabili hivi sasa.Kwa jinsi uchaguzi huo ulivyo endeshwa Kiteto, ni kitu gani ambacho Wakenya na Waafrika wengine wataweza kujifunza na kuiga katika mifumo yao?CCM wamekuwa wakisherehekea ushindi huo.Kuna nini cha kusherehekea katika uchaguzi wa Kiteto?Iwapo CCM ingepoteza jimbo hilo tu moja kwa kuhakikisha kweli uchaguzi katika jimbo la Kiteto umeendeshwa kwa wazi na haki na kwa kuzingatia misingi yote ya kidemokrasia bila ya kusababisha vitisho na hofu miongoni mwa wapiga kura yote hayo kwa manufaa ya chaguzi zijazo,sifa hiyo ingemwendea nani kama siyo CCM pamoja na kulipoteza jimbo hilo,mathalani?Tusingekuwa tumeiosha Tanzania machoni mwa Mataifa mengine barani Afrika kwa mfano mwema?Watu waliojiandikisha kupiga kura Kiteto(2005) ni 74,626.Waliopiga kura ni 35,261 sawa na 47% ya wapiga kura wote.Hii ni chini ya asilimia HAMSINI ya wapiga kura wote.Pamoja na matumizi ya Helikopta zote hizo,Mashangingi kadhaa na pesa chungu nzima bado waliopiga kura ni chini ya nusu ya wapiga kura wa jimbo la Kiteto.HAWA WAPIGA KURA WENGINE 53 PER CENT WAMEHAMA JIMBO LA KITETO AU VIPI?Je, hii inawezekana?Na kama wapo TUELEZWE NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA KWA NINI HAWA ASILIMIA 53% HAWAKUPIGA KURA?Je,Kura zao ziliibiwa?Au WALIGOMA KUPIGA KURA KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI,zikiwemo vitisho au rushwa au wizi wa vitambulisho vya kupigia kura?Je, hii ni demokrasia kweli tuliyo dhamiria kuijenga hapa nchini?Mshindi wa uchaguzi huo ambaye tuna ambiwa katoka CCM amechaguliwa na ASILIMIA 29% TU YA WAPIGA KURA WOTE.Huyu Bungeni atakwenda kuwawakilisha wakazi wa jimbo lote la Kiteto kwa kupewa DHAMANA HIYO na wakazi wa jimbo hilo(wapiga kura) wapatao asilimia 29% TU?Je, hiyo ndiyo Demokrasia tunayo taka kuijenga hapa nchini?Yaliripotiwa matukio kadhaa ya ukiukwaji wa taratibu zilizowekwa katika kufanikisha uchaguzi ulio huru na wa kidemokrasia.Komba aliyepaswa kuwa kiongozi katika kuonyesha jinsi demokrasia inavyo paswa kutekelezwa kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla,alionekana kupitia vyombo vya habari akilazimishwa kutelemka chini ya jukwaa kwa kuvamia eneo lililopaswa kutumika na chama cha Chadema kwa ajili ya Kampeni zake.Kuna vijana waliopigwa na kuumizwa vibaya wakati wa Kampeni.Kumetokea madai ya wapiga kura kadhaa majina yao kuto onekana katika orodha ya wapiga kura.LAKINI BAYA KULIKO YOTE,IWEJE KATIKA JIMBO MOJA TU NA DOGO KAMA KITETO ZAIDI YA NUSU YA WAPIGA KURA WANYIMWE HAKI YAO YA KUMCHAGUA MBUNGE WALIYEMTAKA?Huu ni uchaguzi katika jimbo moja tu na hayo yametokea.Je,mwaka 2010 uchaguzi utakapo fanyika katika majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima ASILIMIA NGAPI YA WAPIGA KURA WOTE WATANYIMWA HAKI YA KUMCHAGUA RAIS WAMTAKAYE na Wabunge watakostahili?There is nothing to celebrate here.In fact,if Um to be frank to myself,to CCM and infront of the almighty GOD,if future elections are going to be held like Kiteto,CCM will be destroying itself!Dunia hivi sasa iko wazi mno.Kila kinachotendeka watu wanaona na bahati nzuri kuna watu wenye akili mno nje ya ulingo wa kisiasa ambao wanayafanyia tathmini matukio kama haya ya Kiteto.Tuweke misingi ya Kidemokrasia kwa faida ya Watoto wetu na kizazi kijacho cha Bara la Afrika kuliko kuendekeza ulafi na uchu wa madaraka!Bob Marley alitukumbusha katika moja ya tungo zake,kwamba 'YOU CAN FOOL PEOPLE ONLY ONE TIME,you can not fool all people all the time'.ZINDUKENI VINGALI MAPEMA.Hapatatosha hapa nawaambieni,shauri zenu!

    ReplyDelete
  10. CCM kwa majini ya kuiba kula tu siwawezi! Zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakuona majina yao, duh!

    ReplyDelete
  11. NYIE JF, HUMU HASOMI MTU HAYO MAGAZETI YENU NENDENI MKAYATUNDIKE HUKO HUKO JF. MSITAKE KUTULETEA VURUGU KAMA ZA KENYA HAPA!

    ISITOSHE WENGI WENU BADO WADOGO MMESEMA WENYEWE MMEMALIZA SEKONDARI HUKO MZUMBE MWAKA 2003 WENGINE 2005. HATA HAO VIONGOZI WACHADEMA WENYE HEKIMA ZAO WAMEKUBALI MATOKEO HEBU ENDELEENI KUSOMA MKIMALIZA MTAUONA UTAMU WA SIASA KAMA MTAKUWA NA MUDA WA KUTUNDIKA MAGAZETI BADALA YA KUTAFUTA PESA YA KULA NA FAMILIA. NI USHAURI TU.

    KOSA LA CHADEMA UCHAGUZI TAREHE 24 UTAWAAMBIAJE WATU UCHAGUZI TAREHE 25? SASA NDIO MAANA HAWAKWENDA KUPIGA KURA.

    ReplyDelete
  12. Wewe ulietoa comment hapo juu 8.42 napenda kukuambia kwamba Watanzania wamechoshwa na 'CHEAP POLITICS',SIASA ZA KUCHUMIA TUMBO NA SIYO ZA KUJENGA AKILI.Kwa taarifa yako mimi niliyeandika comments za 5.47 ni mtu mzima mwenye umri unaolingana na wa Baba yako.Usidhanie wote wanao toa mawazo humu ambayo hayakupendezeshi kwa sababu zako binafsi basi ni Watoto wa Shule.Tumeyaona mengi na ndiyo maana tunadiriki kutoa tahadhari.Hao unao wakingia kifua miaka mitano baada ya sasa hawatakuwepo tena katika ulingo wa siasa,wamechoka ile mbaya.Kwa nini watanzania tukubali kuharibu FUTURE yetu kwa kuendekeza NJAA YA TUMBO?Kama unaogopa vurugu za Kenya kwa nini utoe kauli zinazo shawishi kuwepo mazingira yatakayo sababisha vurugu za kisiasa?Usifikiri kila mtoa hoja katika Blog hii ni mdau wa JF!Penye ukweli uwongo hujitenga.Na hakuna mtu muoga duniani kama mhalifu,daima hutanguliza vitisho na kukwepa hoja.Nakuhurumia sana bwana mdogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...