WIMBI LA UINGIZAJI NA UUZAJI WA VYAKULA VIBOVU ZANZIBAR
Chama The Civic United Front (CUF- Chama Cha Wananchi) kimeshitushwa na wimbi la uingizaji na uuzaji wa vyakula vibovu kwa wananchi wa Zanzibar, vyakula ambayo vinahatarisha maisha na uhai wa wananchi.Hivi karibuni mchele na unga mbovu wenye tani zipatazo 70 ziliingizwa hapa Zanzibar
CUF inashangazwa na vitendo vya wafanya biashara wasio waaminifu ambao huingiza na kuuza mchele na unga mbovu na vyakula vyengine vilivyopitwa na wakati wa wananchi, jambo ambalo ni hatari kwa afya za wananchi.
CUF tunaitaka Serekali ya SMZ kuwachukulia hatua kali wale wote waliobainika kuleta vyakula hivyo vibovu na na kuvitawanya katika baadhi ya maduka hapa Zanzibar kwa kuuziwa wananchi.
Kuchelea kutowachukulia hatua kali waingizaji wa vyakula hivyo vibovu kunahamasisha wafanyabiashara wao na wengine kuleta na kusambaza kwa wingi vyakula hivyo. Tunaamini kuwa laiti kama hatua kali zingechukuliwa kwa wale waliobainika miezi michache iliyopita kuwa walileta mchele mbovu na kama wangechukuliwa hatua kali za kisheria, tunaimani kuwa wengi wa wafanya biashara hao wangeliwacha kuleta vyakula vya aina hiyo ma moja.
CUF tunaitaka SMZ na wawakilishi wa CCM kuwacha kufanya Siasa ndani ya Baraza la Wawakilishi na kuwacha kuwa mabubu katika suala hili muhimu kwa afya za Wazanzibar na Watanzania kwani vyakula hivi husafirishwa nchi nzima, siku chache tu zilizopita kwa ukereketwa tu, mwakilishi wa CUF Mhe Haji Faki Shaali alifungiwa na baraza la wawakilishi baada ya kutowa msimamo wake katika sakata la Mchele mbovu ulioingizwa na mfanya biashara mmoja hapa Zanzibar ambaye ni mfadhili mkubwa wa Chama cha Mapinduzi.
CUF inaungana na kuwa pamoja bega kwa bega na wananchi, na kuwataka watu wote kususia biashara hizo mbovu ambazo zinahatarisha maisha ya wananchi. Pia CUF inawataka Waziri wa Biashara na Waziri wa Afya kujiuzulu mara moja kwani inaonekana kuwa wameshindwa kusimamia Biashara na Afya za wananchi wa Zanzibar
HAKI SAWA KWA WOTE
Salim Bimani
Naibu Mkurugenzi
H/Binaadamu na Mahusiano na Umma
Headquaters:
Headquaters:
P.O.Box 3637,
Zanzibar,
Tanzania.
Tel.: 024 22 37446
Fax.: 024 22 37445
Main Office:
PO. Box 10979,
Dar-es-Salaam,
Tanzania.
Tel. 022 861009
Fax.: 022 861010
Kwani wameona kwamba Unguja ndio dampo la chakula kibovu?
ReplyDeleteNa viongozi WABOVU KUTOKA RAIS MPAKA SHEHA
ReplyDeleteASANTE SANA CUF KWA KUANZA KUVALIA NJUGA MAMBO KAMA HAYA..VILE VILE BIDHAA FEKI ZINAZOKUJA NA MASHUA MZISHUGHULIKIE JAMANI ILI WANAICHI WAPATE HUDUMA BORA..
ReplyDelete