mkurugenzi wa twanga pepeta asha baraka akiongea na mashabiki wa bendi hiyo mara baada ya kuanza maonesho yao toka warudi safari ya muscat. amesema bendi hiyo imejipanga upya kukabiliana na ushindani wa soko ikiwa ni pamoja na kupata vyombo vipya pamoja na wanamuzikia, pamoja na kuisuka upya twanga chipolopolo katika kile alichokiita kwenda na wakati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Sasa 'chipolopolo'manaake nini???
    mbona hatuna ubunifu wa maneno!

    ReplyDelete
  2. Bwana Michuzi line kam tunavyokujua watu wa siku nyingi nilikuwa nauliza huyo jamaa mwenye shati la buluu pili au tatu kwa hesabu za kwenu wamakonde amekunywa mwarubaini uliooza au ndio pozi zenyewe, naomba nisaidieni.

    ReplyDelete
  3. WEWE MDAU HAPO JUU ACHA USHAMBA KUKANDIA WATU MAUMBILE KUNA WATU WAMENDA SHULE LAKINI HAWAELIMIKI HUJAFA HUJAUMBIKA TUMIA AKILIA MSHAMBA SAAANA.
    from MDAU DK

    ReplyDelete
  4. Afanalek... yakhe hawa ndio wanaukuwa jukwaani pale wakikata kiuno..?
    hivi wakija huku zanzibar wanakuwa wanafikia sehem gani hawa..?

    al-hajj mahfoudh.

    malindi
    zinjibar.

    ReplyDelete
  5. Nampongeza Asha Baraka kwa mafanikio makubwa alioyapata katika fani ya muziki.Lakini anakasoro moja ambayo itamshushia hadhi asipo irekebisha kabla wengi hawaja mstukia.Nayo ni ile tabia ya wazi kabisa ya kuto thamini mchango wa wanamuziki wenye asili ya Congo DRC.Kama vile anadonge fulani na jinsi watanzania walivyotokea kuupenda zaidi muziki wa wana DRC Congo pengine kuliko ule wa bendi zake za Twanga Pepeta na Chipolopolo.Mimi ningependa kumwambia Asha hivi,kwamba,Kwanza ni vyema atambue kwamba Wana Congo DRC ni ndugu zetu kabisa na utamaduni wao ni wa KIBANTU kabisa.Ngoma zao za kitamaduni au Za Kienyeji hazina tofauti kubwa na zile za makabila yetu ya hapa nchini.Na ndiyo maana utakuta muziki wa dansi utakao pigwa na bendi za Congo DRC ni ngumu sana kuzitenganisha au kuzitofautisha na ngoma za kwetu hapa nyumbani.Congo DRC pia wanazungumza lugha ya Kiswahili kama sisi.Utaonekana mtu wa ajabu leo hii ukisimama na kutamka kwamba Wana Congo DRC wasizungumze lugha ya Kiswahili.Kwanini?Kwasababu siyo lugha yao.Utaonekana mtu wa ajabu kabisa.Kama ambavyo utakavyo onekana mtu wa ajabu utakapo waamuru watanzania wasishabikie miziki itakayo pigwa na bendi za Kikongo au wanamuziki wenye asili ya Congo DRC.Tamaduni zetu zinafanana sana na ndiyo maana hata uchezaji wa Twanga Pepeta ni uleule anaocheza MPYANA JP MUKULU SHITUKA PAMOJA NA WERRASON!Au unabisha?Hii mipaka iliyowekwa na Wakoloni wakatutenganisha na ndugu zetu wa Congo DRC,Rwanda na Burundi isituzingue sana.Inasikitisha sana kauli kama hizo za kutojenga mshikamano katika fani ya muziki baina ya watanzania na wenzetu wa nchi hizo nilizozitaja sauti hizo zikitoka kwa watu wenye rika la Asha Baraka,ambaye kwa vyovyote vile bado ni kijana Na wengi watamwangalia yeye kama kiongozi.Hata juzi tu hapa alipokuwa akizikaribisha bendi zake zikitoka Ughaibuni alitoa kauli kali kuhusu Watanzania kutoshabikia miziki ya Kikongo zaidi kuliko ya kwetu Tanzania 'eti,kwasababu miziki ya Kikongo ni miziki ya kigeni'!Huu ni upotoshwaji wa ukweli.Miziki yote hiyo ya TZ na DRC Congo ni Miziki ya Kibantu na ya KIAFRIKA.Nafikiri atakuwa amenielewa na hatutamsikia tena akitamka kauli kama hizo ambazo kwa sisi watanzania wenye umri mkubwa kidogo na tunao tambua asili ya muziki wote huo huwa INATUKERA SANA.

    ReplyDelete
  6. Napenda kumuunga mkono kwa %100 mdau hapo juu,lakini na mimi naomba niwakilishe hoja yangu kwa angle tofauti kidogo,kwanza namtakia kila la kheri Da Asha kwa kuziboresha bendi zake zote mbili,pili aache kuzikandia bendi za kikongo tena namshauri aanze kuudhuria na maonyesho yao ili ajifunze na arekebishe kwake kwa sababu hao wanamuziki wa kikongo kama FM Academia huwa wanahudhuria maonyesho ya twanga pale Viongozi kilabu baadi ya siku za jpili then wanaenda kwny onyesho lao pale msasani club,muziki si uadui bali undugu.Tatu wanamuziki wa Twanga wanaringa sana siku hizi wanajiona wako juu kama Werrason au JB wakati bado sana kwa mfano show za zaki kila jpili pale voingozi kilabu huwa wanatangaza waanza kuimba saa nane mchana lakini kiukweli wanaanza saa kumi na nusu wanaimba nyimbo mbili twanga International'e na mbili Chipolopolo then wanasema tuwafuate TCC Club chang'mbe na jtatu ni siku ya kazi wanategemea sisi tunafanya kazi ya kuwafuata wao wakati wanachelewa kuanza kutumbuiza?wanasahu zamani walipoanza kupiga pale Relwe gerezani wakiwa chini wa Mafumu Bilali Bombenga kiingilio kilikuwa bure mpaka wanakuja Viongozi kilabu wakawawameanza kupata chati kiingilio kilikuwa kinywaji soda ,bia au maji,na walikuwa wanaanza saa nane enzi za kile kibao cha Kisa cha mpemba,leo hii kiingilio 2500/= wanapanda stejini saa kumi na nusu ila wanakuwepo kiwanjani tangu mchana nao wanakunywa bia na mademu zao na mabwana zao lakini kwny maonyesho ya bendi za kikongo huwezi kuna upuuzi huu nenda makumbusho,msasani club uone jinsi wakongo wanavyoheshimu kazi inayowapa kula,na naona hakuna cha uzaleno kwny burudani mimi mtanzania ila bendi yangu ya wakongo FM Academia hamna cha uzalendo wala nini.Na umwambia Da Asha najua mnaongea,tena amtibu na Aisha Madinda sio anamtumia tu akiwa mzima
    Mdau wa dansi!

    ReplyDelete
  7. DUU NYIE WADAU WA2 HAPO JUU MMENIKUNA KWELIKWELI AFADHALI MMEMWAMBIA ASHABARAKA UKWELI AJIFUNZE MUZIKI KUPITIA KWA WAKONGO FM ACADEMIA WANAJALI KAZI NAMZIKI WAO SHOO YAO HUCHOKI HAWAJAMAA MWISHOOO NIKO UNGHAIBUNI DK NAWAMISS KINOMA KULIKO TWANGAPEPETA INGAWAJE MIMI NI MBONGO NAWAFAGILIA HAWAJAMAA TANGU ENZI YAKINONDONI
    'FROM TEACHER'

    ReplyDelete
  8. Dah! nadhani meoongea hapo juu hamumtendei Da Asha haki,kuhusu wanamuziki wa Kicongo kwani ukiacha wanamuziki wa Kicongo kama vile kin Ndala Kasheba, king kiki na kasongo mpinda ambao sasa ni watanzania, plus wengine waliokuja kivyao vyao kama wale wa iliyokuwa Marquis,Yeye Asha akishirikiana na kaka yake Baraka Msiilwa ndiyo watu wa kwanza hapo bongo kuwaleta wanamuziki wa Kicongo kama expatriates na kuwaundia bendi yao ya Wacongo watupu iliyoitwa M.K.Sounds.Kwa wale wanaojua historia ya FM Academia na iliyokuwa Diamond Sounds Ikibinda Nkoi watakubaliana nami kwamba bendi hizo zote zimetokana na iliyokuwa M.K Sounds ambayo ilianzishwa na yeye Da Asha na binafsi nimemsikia Nyoshi Elsadat kiongozi wa FM Academia,kina Dodo Ala Bouch na wengine wengi waliopo hizo bendi za Ki Congo kuwa kama si Tantin(Aunt)Asha labda wasingekuwa hapo walipo. Hapa msisitizo nikutaka kuondoa dhana kuwa anawachukia wacongo kama wacongo. Labda tuseme tuu tatizo hapa linalomnyima usingizi ni ushindani wa kibiashara uliopo sasa kwani kwa muda mrefu ni ukweli ulio wazi Twangapepeta hawakuwa na mpinzani. Ni hulka ya binadamu au mfanya biashara yeyote kutaka awe juu daima. Na katika kuwathibitishia kuwa hawachukii wa congo ispokuwa yuko kwenye mapambano ya Kibiashara ndiyo maana tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa ameajiri baadhi ya Wacongo na wazambia kwenye bendi yake ya Twanga Chipolopolo wakichanganyikana na baadhi ya wabongo, ili itoe ushindani katika soko la hivi sasa, wakati huo huo akizingatia umuhimu wa kuinua vipaji vya watanzania kwa kuifanya bendi ya African Stars "Twanga Pepeta International" kubaki kuwa ya wazalendo wa kitanzania tuu.Hapa nionacho mimi ni swala la sera za kibiashara na uzalendo tuu na si kwamba hawapendi wa Congo au wageni.

    ReplyDelete
  9. Hata msemeje Twanga itabaki kuwa juu na ndiyo maana inapata mialiko ya nje kwani inaonekana kweli ni ya Wantanzania kutoka Tanzania. Sasa nyie mnataka kujikweza kwa kuwatukuza wageni ambao mkijaribu kuwatoa nje ya nchi tuu wote wanazamia. Hao Wacongo wanaganga njaa tuu kwao kukitula wanarudi. Nyumbani ni nyumbani tuu, jivunieni na wasanii wa kwenu kama kina Msondo, Mlimani,TOT, Twanga Pepeta. Hongera Da Asha kwa kukuza na kulea vipaji vya wabongo, na usije kuiharibu Twanga yetu kwa kuweka wakuja, tutakususia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...