Balozi mpya wa Zimbabwe nchini Tanzania Edzai Chimoyo akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa JK ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
JK akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Uswisi nchini Tanzania Adrian Schlaepfer ikulu jijini Dar es salaam leo asubuhi.


JK leo (Jumanne, Februari 5, 2008) amepokea hati za utambulisho za mabalozi wawili wapya ambao wataziwakilisha nchi zao katika Tanzania.
Katika sherehe fupi zilizofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Rais amepokea hati za utambulisho wa balozi mpya wa Zimbabwe, Mheshimiwa Meja Jenerali Edzai A.C. Chimoyo.
Pia Rais Kikwete amepokea hati za utambulisho wa balozi mpya wa Uswisi nchini, Mheshimiwa Adrian Schlaepfer.
Katika mazungumzo mafupi baada ya kuwasilisha hati zake, Balozi huyo mpya ambaye ni mtaalam wa jeshi na veterani wa vita vya ukombozi, alimweleza Rais Kikwete jinsi Zimbabwe inavyothamini mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Zimbabwe.
“Bila mchango mkubwa wa Tanzania, ni dhahiri kuwa Zimbabwe na kwa hakika Kusini mwa Afrika nzima, isingekuwa huru,” Meja Jenerali Chimoyo amemwambia Rais Kikwete.
Balozi huyo pia amemweleza Rais Kikwete kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwezi ujao.
Pia Balozi amempongeza Rais Kikwete kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
“Afrika ina changamoto nyingi; vita, ukame, magonjwa na kila aina ya migogoro ya kisiasa na hata kijeshi katika Somalia, Darfur, na sasa katika Kenya na Chad. Lakini tuna imani haya yote utayaweza kwa sababu ya uwezo na uzoefu wako,” amesema Balozi Chimonyo.
Katika mazungumzo mafupi na Balozi Schlaepfer, Rais Kikwete amemshukuru nchi ya Uswisi kwa misaada yake kwa Tanzania. Rais amesema kuwa misaada hiyo, imechangia mno maendeleo ya Tanzania.
Rais Kikwete pia ametumia nafasi hiyo kumwelezea balozi huyo mpya kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali juu ya malipo ya fedha za kigeni ya EPA katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Rais amemweleza balozi huyo mpya jinsi uchunguzi wa kubaini makosa ya jinai unavyoendelea kufanyika katika suala hilo, maelezo ambayo yalimfurahisha balozi huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sasa Mzee yanini unamshukuru huyo mswisisi kwa misaada yake???si wanayarudisha yale waliyoyaiba(na mpaka sasa wanatuibia)...kilichotoka bara la Afrika ni kingi kulinganisha na kile kinachorudishwa!!!Na mwambieni huyo mwakilishi wa Mugabu afunge virago na kurudi makwao kwani wanatuaibisha tu...

    ReplyDelete
  2. Braza Michu, huyu balozi wa Zimbabwe give him 3 months uje uone atakavyoanza kunenepeana. TZ asavali kuna mikate na siagi, sio kama kule Zimbabwe

    ReplyDelete
  3. mbona huyo wa zimbabwe amechoka hivyo???? inaonekana shida za uchumi wa nchi yake imemuweka katika hali hiyo.atleast atakuwa na amani hapa tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...