JK akiagana na msuluhishi wa Mgogoro wa Burundi Bwana Charles Nqakula ambaye pia ni Waziri wa Usalama wa Raia wa Afrika ya Kusini muda mfupi baadaya kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam
JK leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, Charles Nqakula.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Nqakula ambaye ni Waziri wa Usalama wa Raia wa Afrika Kusini, alimweleza Rais Kikwete juu ya maendeleo ya mazungumzo hayo.

Waziri Nqakula alimweleza Rais kuwa mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na kuna dalili kuwa yanaweza kufikia mwisho wake katika wiki chache zijazo.

Naye Rais Kikwete alimshukuru Waziri Nqakula kwa kazi nzuri na kubwa ambayo waziri huyo ameifanya katika kufanikisha mazungumzo hayo.

“Asante sana kwa kazi nzuri hata kama ilikuwa ngumu. Nchi ya Burundi inayo hadithi kubwa ya kuieleza dunia,” Rais alimweleza Waziri Nqakula.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camilius Membe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. warundi nao wengine, wivu pia kuingilia mambo ya watu, bora sisi watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...