Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemaliza mkutano wake na Kiongozi wa Chama cha ODM, Bw. Raila Odinga. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Grand Regency Mjini Nairobi.
Mkutano huo ulikuwa mzuri na wenye manufaa, na Rais Kikwete anaendelea na majadiliano na pande zote zinazohusika katika mgogoro wa kisiasa nchini Kenya. Baada ya kuwa amemaliza kukutana na Bw. Raila Odinga, Rais Kikwete aliondoka kwenda kukutana na Rais Mwai Kibaki ofisini kwake katika jengo la Harambee.
Rais Kikwete ameridhishwa na kazi ya upatanishi iliyofanyika mpaka sasa, hata hivyo Rais Kikwete anaamini kwamba bado kuna kazi zaidi ya kufanywa. Rais Kikwete vilevile ana imani kwamba hakuna jambo lisilowezekana, na kuwa matatizo ya sasa ya kisiasa ya Kenya yatapatiwa ufumbuzi..
Upatanishi katika mgogoro wa kisiasa wa Kenya unaongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dr. Kofi Annan. Pamoja na Dr. Annan, katika kundi hilo la upatanishi la AU, ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa na mke wa Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Mama Graca Machel.
Rais Kikwete aliwasili mjini Nairobi jana jioni ili kuongeza nguvu katika upatanishi wa mgogoro wa Kenya unaoendeshwa chini ya usimamizi wa AU. Jana hiyo hiyo Rais Kikwete alikutana na Dr. Annan pamoja na Mzee Mkapa katika mkutano wake wa kwanza. Mashauriano yanaendelea.
Na
Salvator Rweyemamu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais na Habari,
NAIROBI,
Kenya.
27 Februari, 2008
27 Februari, 2008
JK bwana ya kwake yanamshinda ndani anakimbilia ya nje.Watu wanataka watuhumiwa Hosea na Mwanyika awatoe katika kamati yake ya uchunguzi EPA hajaamua chochote sasa yeye anataka wenzake waamue tena kwa haraka ama ni labda kwa vile watanzania utashi wao wameupeleka kwa kelele na sio kiphyically kama jirani zetu?Rais anapaswa kuelewa kuwa vita ni mapambano yawe ya kimyakimya ama pysical kama yanyotokea kenya.Hivo na hapa kwetu asizibe masikio kwani anapoziba masikio ndio mwanzom wa dalili za kutoka ukimyani kwenda uphysicakoni.Tatua yaliyokwako ili uwe picha ya haki na wengine watakuiga.
ReplyDeleteHuyu JK hadi leo hajamaliza ya CCM na CUF anataka kurukia ya Kenya.
ReplyDeleteMbona anakuwa kama Dully Sykes -AKA Misifa!!