JK leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, Charles Nqakula.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Nqakula ambaye ni Waziri wa Usalama wa Raia wa Afrika Kusini, alimweleza Rais Kikwete juu ya maendeleo ya mazungumzo hayo.
Waziri Nqakula alimweleza Rais kuwa mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na kuna dalili kuwa yanaweza kufikia mwisho wake katika wiki chache zijazo.
Naye Rais Kikwete alimshukuru Waziri Nqakula kwa kazi nzuri na kubwa ambayo waziri huyo ameifanya katika kufanikisha mazungumzo hayo.
“Asante sana kwa kazi nzuri hata kama ilikuwa ngumu. Nchi ya Burundi inayo hadithi kubwa ya kuieleza dunia,” Rais alimweleza Waziri Nqakula.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camilius Membe.

warundi nao wengine, wivu pia kuingilia mambo ya watu, bora sisi watanzania.
ReplyDelete