naibu waziri wa habari na michezo mh. joel bendera akiwa na uongozi wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa dar (rba) pamoja na maafisa toka kampuni ya bia, tbl. toka kushoto ni mdau wa chama hicho, katibu mkuu cheyo meneja wa bia ya kilimanjaro oscar shelukindo, mh bendera, rais wa chama hicho msofe, mpishi mkuu wa tbl gaudence mkolwe, na mkurugenzi mtendaji mbaga mwamboma. hii ilikuwa jana wakati wa ufunguzi wa michuano ya kili super cup uwanja wa ndani wa neshno. michuano hiyo inashirikisha timu sita bora za wanaume zilizofanya vyema mwaka jana kwenye mashindano ya mkoawa dar. nazo ni mabingwa watetezi jkt, mabingwa wa mkoa mwaka huu vijana city bulls, savio, oilers, udsm outsiders na chang'ombe boyz. bingwa atalamba milioni milioni 6 na laki 5

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...