Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. TULIZA BOLI KIPANYA NANA HIYO NCHI ITABAKIWA NA WENYEKITI WA VIJIJI KAMA TUKIFANYA TOTAL QUALITY MANAGMENT TQM. KIPINDI CHA MPITO JAMANI TWENDE KWA NJIA YA SEMICENTURY ANGALAU MIAKA 50.

    ReplyDelete
  2. Jamani eh! KP hapo imetulia itabidi kamati ya richmond ipewe jukumu la kufuatilia UFISADI nchini bila hivyo hatufiki.

    mdau

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza wewe fisadi au mtoto wa fisadi (fisadi mdogo)na ufisadi ndio umekukuza

    ReplyDelete
  4. Kp ingekua wewe na mimi saa hizi tungekua tunanyea kwenye debe ukonga, ila kwa kua vya watendewao viko kwao. ah! bro tutafika kweli? si tubaki na tararira labda itasaidia.

    ReplyDelete
  5. KP hapo hata mimi nakuunga mkono maana jamaa wanasema pesa zinarudishwa lakini hawasemi nani karudisha wala kiasi gani kimerudishwa mpaka sasa kama sio ufisadi juu ya ufisadi ni nini? Wataje majina na amount watu watu tuko wapi kwenye hili.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa kwanza inaelekea ana damu ya ufisadi.Anatakiwa aache kumkatisha tamaa KP ili atupatie vijineno juu ya mafisadi. Tusipoandika juu ya ufisadi, mafisadi watarudi kwa kasi, ari na nguvu mpya.
    MAPAMBANO DAIMA MPAKA TUPATE TANZANIA YENYE NEEMA

    ReplyDelete
  7. Serikali inafanya danganya toto kwa wananchi, tangu lini mwizi akaambiwa arudishe alichoiba? ingekuwa ni hivyo magereza yangekuwa tupu kwani kila mwizi anapokamatwa angerudisha alichoiba halafu basi. Serikali inapaswa iwe makini na ijue kwamba watanzania wa sasa sio wadanganyika wale wa siku zote na 2010 tutawaonyesha kwenye uchaguzi.Makampuni yaliyoiba pesa yanajulikana yote wakamatwe wawekwe ndani,hela zirudishwe na wakanyee debe segerea.Uamuzi mwingine wowote ni danganya toto.

    ReplyDelete
  8. serikali yetu kweli wasanii.sasa tutajuaje hizo hela zimerudishwa ?kazi hipo hapa

    ReplyDelete
  9. Naungana na mdau aliyenitangulia hapa juu kweli Serikali yetu ni ya wasanii tena wamekutana kwny jumba la sanaa b'moyo,eti wanatuambia wameanza kurudisha bila kuwataja ni wakina nani?Kama si kulindana ni nini?Na wakiishazirudisha then nini kitafuata?nadhani hawa wote ni wezi wamekutana kwa sababu mwizi hawezi mkataza mwenzake kuiba wakati na yeye anaendelea kuiba!Ila nimesoma gazeti moja la jana hapa Bongo Waziri wa Fedha akihijiwa na ma-paparazzi ameomba wampe wiki mbili atataja majina ya waliorudisha sasa tushamnukuu tunaye mpaka mwisho?

    ReplyDelete
  10. Hii danganya toto itakoma2010.CCMmsahau ura zetu.Jk unadhani wewe na wanaotu ndio mmesoma na mna uelewa.

    USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA 2010.

    ReplyDelete
  11. nchi yetu kwanzia mkuu wa msafara mpaka wasafiri ni full wasanii!!!nchi ina wenyewe hiyo,angalau huku ughaibuni unaweza ukalalamika ukasikilizwa,nyumbani ni impossible.watu wanagombea vyeo kwa matakwa yao,kila mtu anakula kwa uwezo wake,sidhani kama serikali hii na zilizopita ni tofauti...uzi ni ule ule,tofauti ni ugumu wake!

    ReplyDelete
  12. WADAU UGHAIBUNI NAMBA ZA SIMU HIZO HAPO.

    Mawasiliano pia yanaweza kufanywa na namba zifuatazo: 0713 223362, 0784 998841, 0784 213928 na 0784 785722.

    FEDHA ZA EPA ZAZIDI KUREJESHWA
    2008-02-28 10:36:52
    Na Mwandishi Wetu


    Timu iliyondwa na Rais Jakaya Kikwete kufanya uchunguzi kuhusu matumizi ya fedha za EPA imetoa taarifa ya kwanza rasmi inayoonyesha kwamba kazi yao inaendelea vyema na watu wanaotuhumiwa kulipwa pesa za umma isivyo halali wameanza kuzirejesha na wanaendelea kufanya hivyo.

    Taarifa ya timu inasema kwamba wahusika wengi wametambuliwa pamoja na mali zao na kwamba zoezi la kuhakikisha kwamba hasara ambayo taifa lilipata inafidiwa linaendelea vyema.

    Aidha timu hiyo imewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao, na pia imetoa namba za simu kwa yeyote mwenye habari zinazoweza kuisaidia zaidi timu hiyo apige.

    Taarifa ya timu ya Rais kuhusu uchunguzi unaoendelea wa fedha za EPA

    Ndugu wananchi, kama mtakavyokumbuka, mwezi mmoja umepita tangu Timu ya Rais ya Uchunguzi kuhusu matumizi ya fedha za EPA tulipotoa taarifa kuhusu kuanza kazi.

    Katika taarifa hiyo, tuliwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi.

    Tuliomba mtupatie taarifa muhimu kuhusu suala hili mlizonazo. Aidha, tuliahidi kuendelea kutoa taarifa kwenu kuhusu maendeleo ya kazi.

    Kwa kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali imeonyesha jinsi baadhi ya malipo yaliyofanyika katika akaunti hiyo ya madeni ya nje isivyo halali, katika utendaji kazi wake.

    Timu imekuwa ikifuatilia jinsi watu na makampuni mbalimbali yalivyohusika katika malipo hayo, uhalali wa kisheria wa kila malipo yaliyofanyika, na kufuatilia fedha, mali na wahusika popote walipo.

    Tunapenda kuchukua fursa hii kuwaarifu wananchi kuwa hadi sasa, kazi ya Timu inaendelea vizuri. Kutokana na ushirikiano mzuri ambao tumekuwa tukiupata kutoka kwa wananchi, fedha zilizolipwa isivyo halali zimeanza kurejeshwa serikalini.

    Pia jitihada za kufuatilia mali za watu wote waliohusika zinaendelea. Mali zao nyingi zimetambuliwa na kufahamika, iwe zile zilizopo nchini na hata zilizopo nje ya nchi.

    Timu imejipanga vizuri kwa ajili ya kuhakikisha kuwa fedha zote zilizolipwa isivyo halali zinarejeshwa serikalini ndani ya kipindi kilichowekwa.

    Timu inapenda, kwa mara nyingine, kuitumia fursha hii kuwashukuru kwa dhati wananchi wengi waliojitokeza kutoa taarifa mbalimbali kwa Timu. Kila tunapopewa taarifa zozote, tunazifuatilia taarifa hizo kwa makini kabisa.

    Taarifa hizo zimekuwa ni za msaada mkubwa kwa Timu na msingi wa mafanikio yote tunayo yapata hadi sasa.

    Hivyo, tunawaomba wananchi wote waendelee kutupatia taarifa muhimu na kushirikiana nasi katika jukumu hili zito la kulinda mali na hadhi ya nchi yetu kwa kupitia namba za simu tulizozitoa katika taarifa yetu ya kwanza.

    Mawasiliano pia yanaweza kufanywa na namba zifuatazo: 0713 223362, 0784 998841, 0784 213928 na 0784 785722.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  13. NINASIKIA HIZO PESA ZINAZODAIWA KURUDISHWA ZINACHOTWA NDANI YA BOT KUTOKEA MLANGO WA NYUMA NA KURUDISHWA KUPITIA MLANGO WA MBELE NDIO MAAN HAKUNA ANAYEKAMATWA. sasa sijui na hili litaundiwa tume?

    ReplyDelete
  14. we meneja we!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...