Habari bwana Michuzi,

Mdau hapa, naomba uitwange hii katika blog yetu ya jamii uone watu walivyo serious na mambo ya sheria.


Kisa chenyewe ni kua kuna jamaa ameiuzia serikali taarifa za kibenki ambazo zilikua zinaonyesha watu wanaokwepa kulipa kodi. Serikali ilizifanyia kazi na kuweza kurudisha pesa kutoka kwa wakwepaji.


Uchunguzi mwingine bado unaendelea, ila taarifa za jamaa ni za kweli na ameshakula mshiko wake wa Euro million 4.2. Tatizo ni kuwa jamaa alizipata hizo taarifa kwa wizi (aliibia benki), kwa hiyo wananchi wamechachamaa kua serikali ifunguliwe mashtaka kwa kumlipa mtu ambaye ni mhalifu (mwizi wa taarifa za kibenki) hata kama taarifa hizo zimeisaidia serikali kuwapata wakwepa kodi.

Wadau imekaaje hii kama ikitokea hapo bongo?????

Kwa taarifa kamili gonga hiyo link


Kapongola,
Germany

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HII KALI UKIFUATILIA MAMBO YA KALUMEKENGE KUKATAA KWENDA SHULE MPAKA ALIPOCHAPWA NA FIMBO ILIYAKIKIMBIA MOTO AMBAO UNGEZIMWA NA MAJI AMBAYO MBUZI ILIKUWA BADO KIDOGO AYANYWE NDIO HAYO NAONA.INAONEKANA SHERIA INATUMIKA KUFICHA UVUNJAJI WA SHERIA. KUNA HAWA WATU WANITWA MALOBYST HAWA NDIO WANAGHARAMIA CHAGUZI ZA WATUNGA SHERIA KWANI HUWA WANAAGENDA ZAO ZA KUJILINDA.

    ReplyDelete
  2. ndugu yangu, hii bado too advance for us. hatuna system ya kodi kamili na hatujui nani anapata kiasi gani kwa mwaka na nani analipa kodi kwa mapato halisi. hivyo hata mwizi wa habari akiiba hawatajua kuwa kaiba information kwa nani,

    na ujue sheria yetu ni ile sijui tuiite isiyofungamana na upande wowote...lol....sheria zipo lakini hazifuatwi na malawyer hawana saying

    umeshaona search warrant bongo?
    umeshaona umesomewa your rights bongo? no ...wakitaka watasearch bila warrant na hizo evidence zitatumika mahakamani.

    kwa hiyo hayo mambo ya kumchukulia sheria mwizi wa information zilizosaidia kubaka walaji haziwezi kuapply nchini kwetu...

    Ila kwa kujibu hayo mambo ya huku..hata kama ameisaidia govt yao kufumbua wakwepa kodi lakini alivunja sheria...lazima wamshughulikie...la sivyo wengi watavunja na kutumia mfano wake. Ndio maana wao wanakwenda na sheria na sio kubadili sheria kwa umuhimu wa jambo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...