waziri mkuu mh. mizengo pinda akipeana mikono na mbunge wa monduli mh. lowassa siku alipoapishwa kuchukua nafasi hiyo. mh. lowassa amevunja ukimya na kuongea juu ya maswahiba yaliyopelekea yeye kujiuzulu wadhifa wake na kueleza nini kilichosibu.


Kwa aliyeikosa na angependa kusikiliza aliyosema, bofya hapa http://nukta77.com/yaliyojiri.aspx


Ni mahojiano/mazungumzo ya kama dakika ishirini tu hivi yalirushwa hewani na tvt siku ya Jumamosi 23 Februari 2008 saa tatu usiku majira ya Afrika Mashariki.
Subi'
------------------------------------------------------
Aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa amepata nafasi ya kuzungumzia kujiuzulu kwake kufuatia kuhusishwa kwake na kashfa ya Richmond kufuatia ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dr. Harrison Mwakyembe.
Title: KLH News Episode: Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa akijieleza TVT

Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. ukiweka audio link akikisha inafanya kazi

    ReplyDelete
  2. Nimekiangalia hico kipindi - ntakaco weza kusema ni kwamba huyu jamaa haendi popote na anajiweka sawa huyu kuwania uraisi na si ajabu 2010! CCM itayumba ile mbaya uchaguzi huo, aiseee!! Huyu anao watu wake ndani ya CCM watakaomsaidia manake inaonekana itakuwa vita huko Chamwino uchaguzi ujao!

    ReplyDelete
  3. KWA TAMADUNI WA WAZUNGU, ANAYEONEKANA MUWAZI ZAIDI KATI YA HAWA WAWILI NI EDWARD LOWASA. KWANINI? KWASABABU WAO MTU USIPOMWANGALIA MWENZIO USONI NI MNAFIKI, MWONGO NA HUAMINIKI KWA UTAKALOSEMA. LAKINI INAWEZA KUWA SI KWELI, KWA UTAMADUNI WA KIAFRIKA.

    HATA HIVO SIJUI KAMA NI SAHIHI KUANGALIA PEMBENI WAKATI MNAPEANA MIKONO NA MWENZAKO. KWA UFINYU WA FIKRA ZANGU NI KAMA TU UNAFICHA "HONESTY' YAKO.

    Mdau.

    ReplyDelete
  4. Anony wa kwanza, mbona mimi ninaisikia labla settings zako zinablock hiyo audio kwani iko kama pop up.Fire wall zingine zinaiblock mpaka uiruhusu.

    ReplyDelete
  5. Ukweli ni vita ndani kwa ndani CCM wenyewe na watendaji wavivu ndani ya Serikali. Mkataba wa Richmond hauna tofauti kati ya mikataba mingine yote ya IPP (Indipendent Power Producers) Lowassa alionekana anakuja juu na anakuwa popular na anajiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Na ni kweli hana makosa. Mwenye makosa ni huyo huyo Msabaha ni mbishi na hashauriki na ndio maana rafiki yake kapata kazi Dowans baada ya kustaafu Tanesco.

    Kosa la EL ni kumwamini na kuwaamini hao manyang'au ya Madini na Nishati. Mikataba yote inayotuumiza nchi hii iko huko Nishati kuanzia hiyo ya Umeme na ya Madini. Tatizo lingine ni wanasheria wetu uchwara walioko ofisi ya mwanasheria mkuu. Mikataba inatengenezwa na Investors au Wawekezaji, badala ya ofisi ya mwanasheria mkuu kuandaa mikataba mbadala halafu wakakaa mezani wao wakiwa na alternative contract ndio wanegotiate na wawekezaji wawo wanajadili hiyo hiyo mikataba inayokuja kutoka nje. Hilo ndilo tatizo kubwa lazima waache kudesa na uvivu wa kufikiri nje ya box ili kulinusuru taifa letu. Ama sivyo yeyote atakayeingia madarakani will face the same problem. Waache kudesa watengeneze mikataba yenye manufaa kwa nchi yetu wawekezaji wakute tuna mikataba yetu ndipo tujadiliane nao kwa kutumia mikataba tuliyoiandaa. Kama marekebisho basi wao watumbembeleze sisi kurekebisha ili tuwe kwenye win win situation. Sio hali ilivyo sasa, sisi wenye mali ndio tunawambembeleza wao. Hapa ni tatizo pia la mfumo mzima wa elimu yetu hakuna critical thinking and analysis katika mitaala yetu! Matokeo yake unatoa wataalamu ambao ni yes yes kila kitu.

    I was dying to know which sect Pind is now I know Kurasini mioyo itawatua sasa!

    ReplyDelete
  6. Hata mimi sisikii hiyo sauti, sijui ni tatizo la PC yangu au vipi?? nimpeni ushauri nisikilize ili ni comment hapo

    ReplyDelete
  7. HUYU WAZIRI MKUU WETU MIZENGO PINDA..SAWA TUMEKUBALI LAKINI..INABIDI TUONE UTENDAJI WAKE UNAOFUATIA ..MOST OF US (80%) WE DON'T KNOW THE GUY KIUTENDAJI..NGOJA TUONE KAMA ATAREKEBISHA/FIKISHA MAHAKAMANI/SHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE KWA "..WALIOKUBALI.." KUHUSIKA NA WIZI UFUATAO..

    1.ENERGY (Ufisadi RICHIMOND)

    2.UDHIBITI WA FEDHA NA BAJETI (Ufisadi BoT)

    2.MALIASILI NA KILIMO (WIZI WA MADINI, MISITU YA MBAO NA WANYAMA PORI)

    3.BIDHAA BANDIA KUTOKA (INDIA) NA KWINGINEKO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...