Kaka Michuzi habari za kazi,

Haya ona mambo ya Machame hayo ... ukitaka kuoa huko lazima uwe na pickup ya kubebea majani. Imagine imefulisha mzigo kiasi hicho alafu haina breki, yaani walipofanikiwa kuiweka sawa barabarani wacha irudi rivasi... wacha kidaladala tulichopanda dereva aanze kuhaha manake tulikuwa nyuma ya hiyo pickup. lakini bahati tulisevu, lakini we acha tu...yaani!

haya siku njema wawekee wadau wasiojua mambo ya wachaga

byeee

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Kwa madhumuni ya ze-comedy au kuandaa nyenzo ya kufundishia yenye kichwa cha habari ' NGANO ZA MAKABILA YA TANZANIA' inafaa sasa.

    Lakini kama umeandaa kuonyesha uhalisia wa leo katika ndoa na ushauri kwa vijana wa karne hii, basi mashua imekuacha!

    Watu siku hizi hawaowi HUKO (kama ulivyosema), wanaoa MTU!
    Tafakari tofauti zilizopo.

    ReplyDelete
  2. Uchagani tunaamini akili ni kitu kinachoonekana.Huwezi kusema una akili uchagani wakati huwezi onyesha vitu ambavyo akili yako imezalisha kama vile gari,nyumba,friji ,tv,biashara,pesa n.k.

    Mchaga haamini kuwa mtu mwenye akili ni yule tu mwenye marks za juu darasani lazima uonyeshe vitu.Ndiyo maana ukija uchagani kuoa lazima uhojiwe kama una vitu ili tujue kama una akili kusudi isije kuwa binti anaolewa na jitu jinga ati ambalo litazalisha binti mitoto mijinga.

    Na uzuri wanawake wengi wa kichaga hupenda kuolewa na wachaga wenzao sababu wanajua midume ya kichaga ndiyo yenye akili kuliko midume ya makabila mengine.

    Wachaga tuna akili siyo mchezo.ndio maana hata Machame kuna pickup za kubeba majani na siyo mikokoteni au watu kujitwika majani vichwani.

    ReplyDelete
  3. aisee umesema kweli. akili siyo darasani ni lazima uweze kukabiliana na maisha kama hao jamaa ili uweze kusavaivu. Ndo maana hawajamaa wanaendelea wanachapa kazi kama wachina. watanzania wote wangekua hivyo mbona tungekua first world!

    ReplyDelete
  4. Situsifii bure lakini jamani Machame ni kuzuri watu wanachapa kazi, life standard on average ni nzuri. matajiri kama akina nanihii wapo na wakawaida wamejaa. Kuna mzungu amekwenda huko bado hajarecover from the shock. Vijiji vingine tanzania muende mkaulizie siri ya urembo

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza nyakatulile umechapia, au either wewe ndio mashua imekuacha... bado sana vitu hivi vinaangaliwa may be not direct!! Lakini kila mtu anataka kuoa au kuolewa mahali ambapo pako stable financially.

    Nakubaliana na wadau wa pili na wa tatu kuwa akili sio darasani tuu, ni kugundua vitu kama hivi..hahhahhaaa

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli wadau wachaga mmenikosha haswa na maoni yenu. Kuwa mchaga sio shule ni akili ya kuishi maisha bora. Mchaga sio mtu wa kupenda sifa kama kutaka cheo. Wewe mpatie nafasi yeyote yeye atakula Mfano nenda moshi kijijini ndio kumejengeka na ndio kuna maisha bora naomba makabila yote yafuate mfano wa wachaga.By Mangi

    ReplyDelete
  7. Mchaga ni mtu anaeweza kuishi sehemu yoyote ile na pakawa na maendeleo. Mfano maendeleo ya Bongo Dsm ni wachaga. kwa hiyo usishangae hiyo pick up.Nenda Moshi kuna 4x4 zina engini ya 504 na kuna benz zina taa za 109.

    ReplyDelete
  8. Mfano mzuri ni biashara ya chuma chakavu hiyo biashara moshi ilifanyika miaka ya 70. leo hii hakuna chuma chochote ndio miaka hii imeingia dsm. hii ni kujua tu wenzetu wameamka mapema zaidi.

    ReplyDelete
  9. Makabila mengi yamegundua kuwa kuoa mwanamke wa kichaga ndio mafanikio ya maisha. mifano Inaeleweka. Viongozi wengi wao wake zao ni wachaga.

    ReplyDelete
  10. Poa, lakini mkiwa katika kula lile tunda wanawake zenu wanatulia tuli huku wanasema "ukimalisa funika"

    ReplyDelete
  11. "Akili huwa inaonekana kwa macho", Mzee wa machame nakukubali kwa point yako.

    Ila issue namba mbili, kuwa "kuoa kwa wachaga, wakwe huwa wanadai kabati ya mbeho(friji),umbe wa malela (ngombe),pick-up nk"c kweli mheshimiwa. Hizo kwa kizungu huwa zaitwa "myth".

    Kwa uzoefu nilionao, mahari kuoa mchaga ni Pombe (mbege) debe kadhaa,maziwa kwa kina bibi,blanketi kwa baba na mama,mbuzi,mkungu wa mchare na miguu miwili ya ngo'mbe mnono na ileri(fweza kidogo).

    Nafikiri Mchaga wa machame umenipata hapo.

    ReplyDelete
  12. Mimi sio mchagga lakini naishi uchagani hakuna wachapa kazi na watafutaji kama wachagga.Nimefunguka macho sana kuishi na kufanya kazi nao.

    ReplyDelete
  13. wachaga ni watu wenye wivu sana na roho mbaya sana,mfano kuna mdada mmoja kaolewa na family isiyo ya wachaga kawagombanisha wote na family haina tena mshikamano na upendo yeye katulia anaangalia.nimeshaona wengine wanauwa mpaka waume zao ili wachukue mali,na pia siwapendi sababu kabila lingine wanaona kama si watu, i hate wachaga uchapa kazi ni hulka ya mtu na si wachaga tu.

    ReplyDelete
  14. WE ANONYMOUS TUESDAY FEB 5..2:41PM..ACHA UJINGA..KAMA UNAMAINDISHA MAMBO HAYO SANA TAFUTA MWANAMKE ATAKAYE KUFAA..ILI USHUGHULIKE KWANZIA ASUBUHI MPAKA JIONI AFU WATOTO MTAKAOZAA WAPATE MARASMUS..NA MKEWE AWE GOAL KEEPER TU..NDIO MAANA WANASEMA THA BED OF AN AFRICAN MAN IS VERY FERTILE AND HIS TABLE IS VERY EMPTY..TUNGEKUWA TUNASHUGHULIKA KAMA HAWA NDUGU ZETU LABDA TZ TUNGEKUWA MBALI KIMAENDELEO..KWASABABU WATU WANGEKUWA WANAFIKIRIA ZAIDI JINSI YA KUJIKOMBOA FROM UMASKINI ZAIDI KULIKO KUENDELEZA MAMBO YA UNYAGO!!!.

    ReplyDelete
  15. na ni kweli jamani wanawake wao wanawapenda waume zao zaidi kuliko ..other guys frm other tribes!!! isnt it ovious?

    ReplyDelete
  16. Hahahahahahahahahaha! Ndio maana naihusudu blog ya Michuzi, siwezi kukaa masaa matatu kabla sijaja safisha macho humu.
    Jamani am so proud of being Mchagga. Maana tangia utoto wangu nimekuwa nafundishwa jinsi ya kutafuta pesa. Nimeolewa (MACHAME) still mume na wakwe zangu ndio wananipa darasa la PHD ya kutafuta pesa, yaani hatulali njaa hata siku moja. Na uzuri kwenye biashara zetu tunaajiri watu wengine,kwahiyo akili zetu wachagga zinawapa ajira watu wamakabila mengine ambao bado hawajachangamka.Hata wanangu ukiwapa pesa za matumizi shuleni wanabakisha chenji wanasema, wanajiwekea savings ili na wao waje kuwa na maduka kama ya mama.
    Wachagga noma....... wapo kila kona.Ukiangalia kati ya watu 10 wenye maendeleo lazima 7 watakuwa wachagga?? Je nimekosea wana blogu???prove me wrong, nimewaachia jamvi!!!!

    ReplyDelete
  17. anonymous hapo juu nakuunga mkono, umenifurahisha sana.Kama huna mke nitafute chemba nikupe binamu yangu.

    Tunawapenda sana waume zetu, hata madungayembe yakijaribu kujiingiza kwenye ndoa zetu, wataachwa kwenye mataa tu maana watawalaza waume zetu njaa bureee.Hawajitumi kama sisi wala uvumilivu haupo. Ukitaka mwanamke wa kukuvumilia na kukunyenyekea u know where to go........ kamata uda mpaka Moshi (Tena kipindi cha x-mas) utajiopolea mtoto safiiiiiii hana gharama, mafuta ya Mgando tu mwilini anaridhika sio lotion za mamilioni.

    ReplyDelete
  18. Anony uliyenitaja sijachapia bali nawe unaungana na mtoa hoja kuendelea kuchapia zaidi.

    Sikiliza mada hapa haikuwa AMA WACHAGA WA MACHAME NI WACHAPA KAZI AU SI WACHAPA KAZI AU MTU KUOA AU KUOLEWA NA 'FINANCIALLY STABLE MAN/WOMAN'. HIYO SASA NI TOPIC YAKO MPYA UNAYOTAKA KUIANZISHA.

    NIKUREJESHE KILICHOSEMWA NA MLETA MADA,
    Nanukuu,

    "..ukitaka kuoa huko lazima uwe na pickup ya kubebea majani.."

    NA KWA KUSISITIZA AKATULETEA PICHA YA 'PICKUP' NA KARAHA ALIYOIONA YEYE.
    HIYO HAIKUWA KWA UDHAMINI WA TAMATHALI ZA SEMI BALI ALIKUWA NAMAANISHA HAKIKA ALICHOSEMA NA KUKIONYESHA!

    Sasa hiyo tungo inayosema kuwa LAZIMA UWE NA PICKUP, leo hii!! ndiyo wengine tusiyoikubali maana watu kibao tu wameoa Machame akiwemo kaka yangu lakini hakuwa na pickup na hana mpango wa kununua pickup!!!

    Mdau ndio maana nilisema kama alivyoeleza vizuri mchangiaji mwingine kuwa hizo ndizo ziitwazo myths au mimi nilisema Ngano za makabila ya Tanzania.

    Kwa kiasi kikubwa sana leo hii ndoa zinafuata mitizamo dunia (World View) na mapendeleo ya 'WANAOOANA' ndipo nikasema anaolewa/anaoa MTU kuliko utamaduni asilia wa anapotoka mwanandoa (HUKO). Kwanza jiulize kuna Wamachame wangapi wameolewa na ulinganishe na 'pick-ups' zilizoko huko halafu ndio ushuke hapa kuniambia nimechapia.

    Afterall hakuna utamaduni ulio static watu wanabadilika sana mdau angalia mashua imesha kuacha.

    vinginevyo topic hii humu imebadilishwa na kuwa juu ya uchapakazi na ujasiriamali wa Wachaga tofauti na suala la msingi ambalo kwalo tuliwekewa picha.

    ReplyDelete
  19. HEEE..SHIMBONYI SHAFO..KWA..KORA..MEKUU..HAKIKISHAHIYO NGOMBE INATOA MASIWA LITA YAKUTOSHA...LASIMA ILIPE....KABSA BABAANGU...KINDO KYAFOMBEE..

    ReplyDelete
  20. Ni kweli ni wachapa kazi tena yoyote ikiwa kushona viatu kuuza duka kuanzia chinga,duka uchwara mapaka hyper, ila ile sifa ya wizi na ujambazi mh! WAMEZIDI hapo, miaka ya 70 eee waliwika bongo kuchinja wenzao na tena anakuchinja kikatili huku anakusimanga" kufa polepole eee usiniharibie kisu changu eee.hasa hao wamachame hata wachaga wenzao wanawasifu kwa ukatili na uroho wa hela.

    Ila napenda wale wenye mapenzi mema utamkuta kazini kwake myenyekevu katika kuvuta wateja, karibu msee karibu tajiri yangu eee. Ndio maana wanafanikiwa sana biashara zao kutokana na lugha zao za kubembeleza, na hawachagui mteja wake yeyote huwa mfalme kwake ndio maana wakiuza maduka yao hupata jina maramoja DUKA LA MCHAGA .

    ReplyDelete
  21. Mimi nimetokea Morogoro. Nimeowa mchagga na nemezee nae watoto watatu, kwa juhudi na maarifa aliyo toka nayo huko uchaggani, watoto wawili wako chuo kikuu Dar na mwingine form six. Nimejenga nyumba ya matofali kijijini kwentu, Kigurunyembe. Alicho fanya mwana mama huyu kwenye shamba langu hekari 10, ni kitu cha maajabu. Tuna lima mboga za majani na kuuzia wenyeji na mahoteli. Waluguru wenzangu wana mashamba kama langu, lakini badala ya kuchapa kazi, mashamba yetu yana ota majani tu. Tatizo la wachanga, hawana mapumziko mpaka x-mass.

    ReplyDelete
  22. MIMI NI MCHAGGA WA MACHAME,NIMEOLEWA NA MUME WA KABILA LINGINE,KWA KWELI NINA SHIDA SIJAPATA KUONA KWANI NAJITUMA NIMEFUNGUA GLOCERY YA BIA NA MADUKA YA BIDHAA NDOGONDOGO,PESA NI NYINGI TUMEJENGA NYUMBA TATU,NZURI SANA MOJA AMEPANGA MZUNGU,PESA IKIPATIKANA BWANA,ANACHUKUA ANAHAMIA KWA BINTI,AKISINGIZIA KAIBIWA!!,BASI NAKATA TAMAA SANA,NA BWANA UKIMSHAURI NENDA KATAFUTE KAZI,AU SIMAMIA BIASHARA,UTAPATA LOSS KILA SIKU!!!
    NAOMBA USHAURI WANA BLOG NIACHANE NA HUYU BWANA NIFANYEJE,KWANI MIMI NINA NIA YA KUJENGA GHOROFA KARIAKOO,NA NINGEISHAFANYA HIVYO NI HUYU BWANA TU NDIO ANANIANGUSHA.NI MUME WA NDOA NA NINA WATOTO NAE 3,PIA NAMPENDA,TATIZO NI HILO TU!NIFANYEJE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...