mama kikwete akisalimiana mwenyekiti mwenza wa The Universal Peace Federation Co-chairman Dr. Hyun Jin Moon
mama kikwete akiwa na bishop abel muzorewa mkutanoni


mdau freddy maro wa ikulu anatupasha kwamba mama wa kwanza jana amewasili Seoul, Korea ya Kusini, kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa amani duniani (World Summit on Peace 2008) kwa mwaliko wa Shirikisho la amani duniani (Universal Peace Federation -UPF).



Takriban wajumbe 200 toka nchi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano huo, wakiwakilisha viongozi mbalimbali wa dunia, ikiwa ni pamoja na marais wastaafu, wabunge, viongozi wa dini na jamii chini ya kaulimbiu ya “Toward a New Paradigm of Leadership and Good governance for Peace in the 21 Century”.




wajumbe wataongelea namna nzuri za kufuata katika kuleta amani duniani kwa watu wa mataifa yote, rangi zote, dini zote ili kuwafanya watu waishi pamoja kwa amani. mada zingine zitazojadiliwa ni vyanzo vya migogoro, kutokuwepo usawa, umaskini na kuelekea katika mapatano, ushirikino na ustawi kama jamii moja ya binadamu.




baadhi ya watu mashuhuri wataokuwepo mkutanoni na ambao wameshawasili Seoul ni pamoja na waziri mkuu wa zamani wa zimbabwe bishop abel muzorewa, waziri mkuu wa zamani wa guyana hamilton green, na imamu mkuu sheikh assane cisse ambaye ni rais wa taasisi ya kiislamu ya waafrika-wamarekani ya senegal, pamoja na rais wa zamani wa sierra leone, alhaji ahmad tejan kabbah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mama yetu kapendeza kweli hapo.Hongera mama wape pointi hao.

    ReplyDelete
  2. Jamani myonge myongeni haki yake mpeni!!mama wa kwanza kapendeza..hongera mama yetu uu mzuri kwa kweli..

    ReplyDelete
  3. mama yetu wa kwanza yupo very cute halafu amependeza sana.keep it up mama,mpambe wake wa mavazi nae anastahili pongezi.

    ReplyDelete
  4. Walah huyu Mama ana maji ya nguo....

    ReplyDelete
  5. Ujumbe umefika, Mama!

    Wakikuuliza wajibuni, "Tanzania ni Nchi ya Tatu Afrika kwa Dhahabu!"

    Kumbe Kasisi Muzorewa bado yupo imara?

    Hako ka-kasisi karikuwa kakijaga hapa Tanzania kuudhuria mikutano ya kutatua mgogoro wa siasa wa Rhodesia-Zimbwabwe, na kuraraga Kilimanjaro Hoteri yetu.

    Harafu karipokuwaga kanaurizwa juu ya Nyererena Tanzania karitamkaga:

    “Nyerere is against our proposed modality of de-colonising Rhodesia-Zimbabwe based on tripartite (a White three point vote, an Asian two-point vote, and an African one-point vote) whereas Nyerere himself acquiesced with and accepted the same modality in de-colonising his Tanganyika!"

    "What can they advise us on our economic development when their top tourist hotels do not have toilet papers!”

    ReplyDelete
  6. MAMA SALMA ANA BABY FACE NA ANAJUA KUVAA

    ReplyDelete
  7. Bwana Michu,Tofauti Ilioje Hii!!

    Tz.
    Mama wetu Wa Kwanza yupo nje ya Nchi, anamuwakilisha Mumewe na Taifa letu kwa ujumla,anapendeza kwa mavazi ya Heshima kabisa,bila shaka hoja zinazozungumzwa hapo ni za Msingi kabisa.

    Kenya.
    Kwa mara nyingine tena,Mama wetu Wa Kwanza yupo ndani ya Ikulu, ndani ya vazi la Kulala(Pajamas),anawaamuru maafisa utendaji/usalama wa Ikulu wamtoe Mhe.Imanyara(Mb) kwenye Kikao kinachoendeshwa na Rais,na kisha Kumshambulia Kwa Migumi na Matusi ya Nguoni.Mhh! mama wa shoka huyu.

    **I'm sure Mr.Koffi is asking himself this Que:If you can't stop the Violence in your Own house,how about National wide?? **

    ReplyDelete
  8. Umependeza sana mama wa kwanza you rock!!!!!!!!!
    Designer wako kakusomea sana hongera for representing the beautiful women of Tanzania

    ReplyDelete
  9. mama yangu weeeeeeeeeeeeeeeeee~!! Nyu weldi oda hiyoooo!! Watu wote watasali siku moja, na atakayekaidi ni kichapo kikali!!!!

    ReplyDelete
  10. huyu mama kikwete is alyws looking hot like fire shes definately on the hot point what a beautiful mama africa queen for real love her style and keep up with da good work mama represent

    ReplyDelete
  11. Mmmh Mama anajua KUVUNJA KABATI...
    Halafu Bishop Abel Muzorewa ameweka KANTA...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...