Ndugu Michuzi naomba nipitishe kilio changu kupitia huu mtandao wetu wa jamii kuhusu pesa zilizochotwa Benk kuu kupitia mwamvuli wa EPA.

Nimeshtushwa na taarifa ya kamati iliyoundwa chini ya mwanasheria mkuu inavyofanya kazi ya ya kufuatilia pesa zetu.Katika gazeti moja la kiswahili nimesoma habari inayosema kwamba wahusika wameanza kurudisha pesa walizochota na kusisitiza wananchi tuendelea kutoa taarifa zaidi. Mimi naona hayo maneno hayaingia katika fahamu zetu hata kidogo.
Sisi kama raia wa Tanzania tunataka kuona watu waliochukua hizo pesa wanafikishwa mbele ya sheria na sio kujadiliana nao juu ya kulipa.
Hata hivyo tunapenda kujua kama hizo pesa wanarudisha wanatumia njia gani kurudisha (payment plan). Tena tunapenda kujua hii kamati ina mamlaka gani kisheria juu ya kushauriana na wahujumu uchumi kuhusu kulipa hizo pesa nje ya mahakama. Hauwezi kwenda kushauriana na muhujumu uchumi Golden Tulip Hotel huku mnapata kuku na kinywaji.Kwa nini hii kamati inafanya kazi kwa usiri mkubwa wakati majina ya mafisadi yalishatajwa katika uwanja wa mwembe yangu na Dr Slaa wa chama cha Chadema?.
Tunaomba kamati hii iwasiliane na Dr Mwakyembe ambae ameonyesha anauchungu na nchi yake kama hawajajua cha kufanya.Inavyo onekana hii kamati bado haijajua inapaswa kufanya nini haswa ikizingatiwa baadhi ya wajumbe wake wamehusishwa na ufisadi.

Jamani kuuliza sio ujinga, kama kampuni pamoja na wamiliki waliochota pesa wanajulikana hii kamati inataka maoni gani kutoka kwa wananchi?. kwa nini isianze na hao kwanza na kama kuna vitu wanaficha kama majumba au magari ndio sisi wananchi tuvitaje kwani tunawaona wanavyoishi huku mitaani.Tunaomba hii kamati ifanye kazi ikiwa inajua sasa hivi watanzania tumebadilika,na hatuko tayari kuona tunadanganywa kama alivyofanya Karl Peters enzi za ukoloni.
Mdau
Pastor Abisalom Nasuwa
Dallas Baptisty University
U S A.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Pesa zenyewe zote walizokula ni za misaada, sasa nyinyi kinawauma nini? alafu hata kama zingekuwepo unadhani mngegawiwa?

    Ukweli ni kuwa zinge kuwepo au zisingekuwepo hakuna tofauti. Ni unafiki mtupu kwa mtu yeyote anayejitia anumia roho na si kingine.

    ReplyDelete
  2. nasema hivi ndg yangu wote washenzi majambazi wakubwa wanafichana maana ukute mpaka bwana mkubwa yumo
    ulisikia wapi mhujumu anarudisha kisiri tunataka wawekwe wazi mbele ya mkono wa sheria mbona kibaka akiiba manzese hawamwachii arudishe alichoiba na kuondoka tusifanyane wajing kabisaaaaaaaaaa
    wanaizaya wakubwa mbuzi kabisa kichefuchefu na tunasema iko siku tukichoka mtajuta

    ReplyDelete
  3. Msituchezee akili.. Nyie na sisi sote ni wasomi.

    Kitendo cha wanakamati kushindwa kutofautisha kati ya majukumu ya kamati na majukumu ya vyombo vya dola ni kuchezea watu akili. Wana kamati wote ni wasomi, hivyo kutoa hizi statements ni ukiukwaji wa ethics za taaluma zao.

    Kazi ya kamati ilikua ni ku-come up with resolutions/suggestions. Baada ya hapo, vyombo vya dola ndio vingefanyia kazi hizo resolutions zao. Kuna kitu kinataka kufichwa hapa na hawa wanakamati kwa wao kuanza kufanya kazi za vyombo vya dola.

    Tupeni majina tuwajue hao mnaowafichua. Taarifa juu ya wahujumu wa uchumi sio "classified material"..

    ReplyDelete
  4. MCHUNGAJI,
    BAADA YA MAHUBIRI HAYA YANAYOPENYA KAMA UPANGA UKATAO KUWILI, MIMI MUUMINI WA KWELI, HAKI, DEMOKRASIA NA HEKIMA ITOKAYO KWA MUUMBA, AMBAYE SISTAHILI HATA KULEGEZA KIFUNGO CHA KOLA YAKO NABAKI NIKIWASHAWISHI WADAU WENGINE.

    KWAMBA, JUU YA KAULI HII YA KINABII TUNAYOIHUHUDIA KATIKA SKIRINI KUPITIA VIDOLE VYA MPELEKWA NASUWA,
    'WATU WOTE TUSEME AMINA!'

    ReplyDelete
  5. MIMI PIA JANA NILITOA MACHOZI YAANI WATANZANIA TUMEFANYWA MAZOBA SO PAINFUL.

    ReplyDelete
  6. Kwa wale wanaojua au kuweza kusoma barua ndani ya bahasha bila shaka wanajua ni kitu gani kinacholengwa. Ni wazi kwamba kuna mambo yanafichwa na viongozi wetu ndio maana wanaolipa hawatangazwi, pia kamati haitaweza kutoa duku duku la wananchina mwisho wa siku tutaambiwa fedha zimerudi na mambo kuishia kama kawaida yetu. Kwanza tujiulize hii tume inao uwezo wa kufanyakazi ya kiadilifu na kuaminiwa na wananchi? maana kuna wajumbe tayari wametuhumiwa ktk tume ya Dr. Mwakyembe na mapendekezo wote tunayajua ikiwa ni pamoja na mambo mengi tunayoendelea kuyasikia kuhusu wajumbe hawa! tusitegemee maajabu kutoka tume hii.

    ReplyDelete
  7. MZEE TULIZA BOLI NDIO KAZI IMEANZA HIVI UNAFAHAMU KWANINI MAWAZIRI WA MAMBO YA NDANI SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI WANASEMA JAMANI HEE WALE WOTE WENYE SILAHA ZA KUTUMIA RUISASI ZA MOTO "WANAOMBWA WAZISALIMSHE KWENYE VITUO VYA POLISI KUANZI TAREHE FULANI HADI .....TUNAWAHAKIKISHIA HATUTA WAFUNGULIA MASHTAKA. HII INAITWA KIPINDI CHA DIRISHANI YAANI WINDOW PERIOD. MAANA YAKE KAMA KUNA MOTO SIO ULAZMISHE KUPITA MLANGONI. MARA NYINGI KESI KWA KIPINDI HIKI CHA MWAZO ZINZSABABISHWA USHAHIDI KUKIMBIZWA HOFU KUZIDI PIA HATUTAKI KUWAPOTEZA MASHAHIDI KWA SHINIKIZO LA DAMU. TUWE NAO TUWAPENDE WATUBU KWA HIARI TUSONGE MBELE.HII TANZANIA UNAYOOMBEA KILA SIKU IKO NJIANI USIHOFU VITUKUU VYETU WATAFIKIA HAPO.ASLIMIA ZAIDI YA 95 KWA HISIA ZANGU TULIKAA MKAO WA WAPI TUTAPATA DEAL TUJIKWAMUE NA UMASIKINI NA AINA YA MADEAL NDIYO HAYO HAYO WENZETU WAMETUWAHI. SASA TUAMUE KUANDA KIZAZI CHA KUISHI KWA MAADILI LAKINI SIO HICHI KIZAZI CHETU KILICHO JAA MAPUNGUFU AMBAYO SIO NIA YETU KUWA NAYO,
    TUMAINI GEOFREY

    ReplyDelete
  8. Sikiliza Pastor,

    kabla ya kukujibu nikuulize kwanza mara ya mwisho we kua huku bongo ilikua mwaka gani??

    Nahisi ilikua kipindi cha Nyerere maana hueklewi kabisa bongo inavyokwenda,

    Kwa taarifa yako ile ni Kesi ya nyani kapelekewa tumbili,

    Huyo Mwanasheria mkuu unaemsema ana ma-skendo kibao kuliko hata hao anawaowachunguza,
    Yaani leo wao kesho yeye.

    Pia ufahamu tu kua Hao jamaa walioiba na wanajua wezi wenzao waliobaki serikalini hivyo wakiwabugudhi basi watamwaga mchele kwenye kuku wengi,

    kama umenisoma basi ni hayo tu

    ReplyDelete
  9. DAA!!EBWANA NIMEAMINI KUWA WATU WANAJUA MAMBO,NDIO MAANA HUWA SIACHI KUPITIA BLOG HII,TUMAINI GEOGRE UMENIFURAHISHA SANA NA POINT ZAKO,ILA UNAONEKANI NAWE NI MMOJA KATI YA HAO NDIO MANA UMEZUNGUMZA LUGHA YA KUTETEA MAFISADI.

    NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  10. Hint! Michu waambie vijana kuwa mwizi wa cash huwa vigumu kumuweka ndani esp kama aliiba dollars. Ukimfunga kwa kosa la kuiba, then ukamfunga miaka kadha., what if y those $$ amezichimbia kwenye ukuta au chini ya godoro? Hii itakuwa ni hasara zaidi kwani by the time anatolewa lupango, purchasing power ya hiyo $$ itakuwa imepungua sanaa unless aliziweka kwenye banki fulani.
    On that note, if they are returning the $$, wacheni kwanza warudishe then tuwaanzishie zari kwa pilato.

    ReplyDelete
  11. Pastor nakubaliana na wewe asilimia 100, aliyesema hayo ni Mh Mkuro( waziri wa Fedha. Swala hilo limeonyesha dhihaki kubwa sana kwa watanzania, Mh waziri wa fedha ameonyesha dhahili kuamini kwamba sisi Watanzania wote hatuna akili na ni mazezeta.

    Vile vile, muheshimiwa amesahau kwamba wananchi ndio waajiri wake, na sisi walipa kodi ndio tumeibiwa. Ni ufahamu wangu ya kwamba serikali inahofia kwamba baadhi ya pesa zilitumika katika maswala ya CCM, na kama sio kweli basi ni kwa nini zisianikwe adharani?

    Nimewaomba viongozi wote wa upinzani na viongozi wa dini kufunga na kumuomba mungu atusaidie kwani baraza jipya linataka kuturudisha mwaka 2006, mwaka ambao Tanzania imeibiwa kushinda miaka yote.

    Watanzania wenzangu, tupinge maamuzi ya waziri wa fedha, tuombe kwa pamoja majina ya watuhumiwa yavikishe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
    Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa
    Mdau wa USA

    ReplyDelete
  12. NASHUKURU MDAU KWA COMENTS ZAKO,ZINANIPA NGUVU. MIMI INABIDI NIKITOA MAONI NITAFUTE MLANGO WA KUTOKEA .

    ReplyDelete
  13. Tumaini mtoto wa fisadi, au mjomba wako ndio fidasi vile, au shangazi yako vile, ha hizi pesa za ufisadi ndio zimemfikisha hapo alipo, wewe kweli FISADI KIWEMBE maana unakata kwa pande zote i.e huku na huku.

    ReplyDelete
  14. Wallahi kaka michuzi,mie sijawahi ona Hii Nchi dah!ndo yamekuwa hayo eti wanarudisha pesa!mbona kuna watu wamo ndani walitaka kugushi tu hata mdhamana hawapewi maana hata sent tano hawakuwahi kuiba lakini wamo ndani mfano kuna kesi ya wafanya biashara maarufu hapo Dar wamo ndani si haki!kuna walakini lakini iko siku !

    ReplyDelete
  15. Mchungaji mi nasema kiwazimu, kama watarudisha hata kwa siri ni vema ila zoezi liende kwa uaminifu mpaka senti ya mwisho kisha ule usemi wa kelele za mlango zisizomzuia mwenye nyumba kulala ziendelee tuone kama watapata usingizi kama jasho la mtu laliwa. hapo tukishapata angalau albaki ndo tupige kelele za kuwatia neti.

    ReplyDelete
  16. Mimi nasema hivi, bila 'Ze pipoz pawa' hakuna kitakachoendelea zaidi kuhusu haya yaliyoanzishwa juu ya ufisadi. Balali hataonekana, EL ataendelea kujisifia kwamba kang'atuka kishujaa (maana hakuna mtu wa kumfilisi), NK ataendelea na shughuli zake k.k! Sitarajii katika watu walioko kwenye system kuna mtu wa kumnyooshea kidole mwenzake. They have been doing it together! Kitakachoendelea hapa ni mchezo wa kuigiza!
    Tatizo hapa ni umma wa wa-tz unakubaliana na hali hii. Ufwisadi haujaanza leo tz and yet we re-elect the same people to lead us into the endless pit of poverty.
    Tatizo kubwa hapa kwetu ni kwamba wadau wengi wa nchi hii ambao ndiyo wenye kuamua nani awaongoze wako tayari kumchaguwa mtu kwa sababu tu wanapenda hata rangi ya mavazi ya chama chake. Wengi wao hawawezi kutofautisha kati ya umaskini na utajiri. Mimi nafikiri watu ambao hawakuogopa umande kwenda shule, kama wadau wa globu hii, ndio watu wanaoweza kuleta mabadiliko. Tukiwaachia watu walioko Namtumbo, Chikanamulilo, Nyakitonto, Nshamba, Mlowa, Mamba Myamba, Misigiri, Kiagata, Bereko,Tinde n.k, n.k kwamba wataleta mageuzi ya nchi hii kwa kura/kula yao tunajidanganya!

    ReplyDelete
  17. KUTOKANA NA MAONI YENU INAONESHA JINSI GANI SISI WANANCHI WENYEWE TUMEGAWANYIKA KUHUSU SWALA LA MAFISADI.KUNA WALE WANAOWAUNGA MKONO MAFISADI KAMA MDAU MICHAEL JUU NA WALE TUNAO PINGA.WANAUNGA MKONO NI KWAMBA WAO WASHA KATA TAMAA NA MAISHA YA MTANZANIA.NA WOTE HAWA NI KWAMBA WAO WANAJIANGALIA BINAFSI KWAMBA MAISHA YAO YANAENDA VIZURI KWAHIO KILA KITU POWA KWAMBA HAMNA TOFAUTI MAFISADI WANGEIBA AU LA.SASA NAWAAMBIA HAKI INAYOTETEWA HAPA SIO TU KUJIANGALIA BINAFSI WEWE PIA YULE MTOTO KIJIJINI ANAYETESEKA SHULENI KUSOMA KWA KUKAA CHINI,YULE MTOTO NA WAZAZI WAKE KIJIJINI AMBAO HAWANA MAJI MASAFI YA KUNYWA,KUPIKIA WALA KUOGEANA KUFULIA.NI WALE WATOTO VIJIJINI NA ZAHANATI ZAO AMBAZO HAZINA UMEME WALA MADAWA YA KUWATIBIA WAGONJWA.WADAU TUKUMBUKE KWAMBA TANZANIA SIO DAR ES SALAAM PEKE YAKE.TUKO HAPA TUNAANGALIA JINSI GANI HIZI HELA ZILIZOCHOTWA BILA HURUMA ZINGEWEZA KUWASAIDIA WATANZANIA WENZETU AMBAO HAWANA UWEZO.NA MDA KAMA HUU TUUTUMIE VIZURI TUKIPATA NAFASI KUTOA HOJA SIO TUNALETA UTANI KILA WAKATI KWANI NJIA YA RAIA KUWASILIANA NA SERIKALI NI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI,TUKIENDELEA HIVI SIKU MOJA TUTASIKIKA TU.SERIKALI NAYO IKUMBUKE PAMOJA NA MAFISADI WAKE KWAMBA
    CHOZI LA MNYONGE MALIPO KWA MUNGU NA KAMA HAWAMUOGOPI MUNGU WAACHE KULA VIAPO KWA KUTUMIA VITABU VYA MUNGU WAKIWA WANAAPISHWA.

    ReplyDelete
  18. Kaka Nasua ni wewe uliekuwa JKT Tabora? tuwasiliane.

    ReplyDelete
  19. Hivi hizi comment ni kweli michuzi huwa ana soma au ? Manake kila comment zangu zenye maana bila kuwa na tusi hata moja aziwekwi au kwa vile zina uchungu mno na zinaweza kuwasisimua wadau? Lakini sio mbaya najua kaka michuzi utakuwa unaogopa swala kama la jambo forums lilowatokea nitakochokuwa nafanya nitakuwa naunga mkono wale wako na mawazo sawa na mimi kama john paul.

    ReplyDelete
  20. KUNA RESEARCH INAONYESHA HALI HII TANZANIA ITAENDELEA TU, VIONGOZI KUFANYA WATAKAVYO, WANANCHI WAMEKAA KIMYA.

    KWA NINI?? HAMNA SHIDA TANZANIA, KWA HALI NGUMU WATU WANASURVIVE.KWANZA MALIASILI YAISHE, IWE KUWA KAUNA TATIZO AMBALO KILA MTANZANIA LINAMUUMIZA.WATAUNGANA NA KUONA UMUHIMU WA KUWA NA VIONGOZI SERIOUS.IFIKIE KIPINDI NAULI IPANDE NA ROBO TATU YA WAKAZI WA DSM(MFANO) WANASHINDWA KWENDA WANAKOTAKA KWENDA, HAPO NDIPO WATU WATAAMKA.SASA HIVI NI POROJO.MNAMSUBIRI BUSHI AJE MUONEKANE MNAONGEA.....ACHA WALE...ACHA WAFENYE USANII....SHIDA HMANA TZ, INGEKUWEPO TUSINGEANDIKA KWENYE BLOG AUTOMATICALLY TUNGEPIGANA.TUNGEKUWA SERIOUS KUCHAGUA VIONGOZI, WALIOAMKA NA WANAOLALAMA PENGINE NI WALIOSOMA, WANGAPI HAO?? WANGAPI HAWAJASOMA TZ..LOWASA KAPOKELEWA KWA SHEREHE..AKINA NAI WAMEMPOKEA WANANCHI.TENA WATAMCHAGUA AWE MBUNGE WAO!!!!TUFANYEJE SASA, TUTALALAM WE, WAKATI WANANCHI WA HALI YA CHINI NDIO WANAOUNGA MKONO HALI HII.PENGINE HAWAPENDI LAKINI WAFANYEJE WAKO GIZANI.KWETU MBEYA KIJIJINI MTU ANAWEZA ASIWE NA HATA SENTI AKAISHI,VYAKULA VIKO SHAMBANI.ATAANDAMANA HUYU.
    ACHA SHIDA IJE ITUTAFUNE PENGINE TUTAAMKA.

    VIONGOZI WOTE WAKO SAFI.KIKWETE MSAFI...!!! UNAGUNA..jamii mbovu utoa viongozi wabovu, wamefikaje pale...nani aliyewapigia kula kwa nini, nini alichokifanya kikwete zamani kilichopelekea sisi kumchagua??

    mdau-canada

    ReplyDelete
  21. Wadau kama wakina michael inatakiwa wajue wadau wengi au watanzania wengi ambao wanakemea swala la ufisadi sio kwa sababu ni wanafiki au ni wivu unawasumbua.kinachotufanya tukemee ni umaskini tuliokuwa nao unao wafanya watoto wakae chini mashuleni kisa hakuna hela ya kutengenezea madawati,hakuna hela ya kuwalipa walimu hili waweze kufundisha katika mazingira ya upendo,hakuna hela ya kujengea visima hili raia wapate maji masafi ya kunywa kutuepusha na maradhi na kupunguza vifo.hakuna hela ya kutoa huduma za afya kwenye vijiji na mambo mengi sana.huu ni umaskini unaosababishwa na watu wachache ambao hawana uchungu na hawana moyo wakuisaidia nchi bali ni kuangalia maslahi yao.cha ajabu walitumia vitabu vya dini kula kiapo cha kutumikia taifa kwa huaminifu . Siku itafika watanzania tutaweza kufaidika na utajiri wa nchi yetu.

    ReplyDelete
  22. MIE HATA SIELEWI KITU HUMU NDANI, JAMANI SI WANACHI WAMEPIGA KELELE PESA ZIRUDISHWEEEEEEEE! SASA ZINARUDISHWA AU HAMTAKI ZIRUDI.

    HATA RICHMOND WATU WALIPIGA KELELE PESA ZIRUDISHWEEE! SIJUI KAMA ZITARUDISHWA. SASA MWATAKA NINI? WAKIHUKUMIWA BILA KURUDISHA PESA TUMEPATA NINI? SI BORA HIZO PESA ZIRUDI ZOTE NA INTEREST JUU. THEN MAMBO MENGINE BAADAYE.

    vigeugeu nyie, mie siwafati tena kwanza hata kanisani sipajui!

    ReplyDelete
  23. Taja majina kwanza hukumu baadaye

    Wakirudisha bila kuchukuliwa sheria tunajua zingine wameficha.. what is the point?

    Namtaka Bush afanye safari tena bongo baraza la mawaziri litabadilishwa tena. Bila hivyo watamumunya hela zetu kiulaini sana na kutucheka kutufanya wajinga tu.

    I wish maviongozi wote wangeondolewa tuanze upya. Wote ni muozo tu ndio maana kila mmoja hawezi kumgusa mwezake kwa vile naye ana madhambi yake.

    Hao watu wanaoiongoza nchi wajue kua this is another generation. We don't play and we see in black and white not just the gray potion of the story...

    Na wewe Tumaini kama unatetea baba yako dawa yako iko jikoni. Mtatoka kuishi oyester bay/ masaki/msasani mlikokulia na soon mtaahamia kijichi ndio mtaelewa ulimwengu ni nini.

    Tumechoka kufanywa watoto kila siku wakati wengine wanaejoy hawajui ugumu wa maisha kabisa kwa kupitia politics

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...