Kampeni ya kumsaka Miss Tanzania Uk 2008 yaanza

Waandaji wa Mashindano ya Miss Tanzania Uk, wamenaza kampeni yao mapema kwa kutafuta washiriki wa shindano la mwaka huu litakalokuwa la kukata na shoka.

Tayari imezinduliwa tovuti maalum ya Miss Tanzania Uk 2008, itatakayokuwa na jukumu la kuwafahamisha wadau wa urembo taarifa mbalimbali za shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

Hivyo basi kama wewe Mtanzania na mrembo unaishi maeneo , hilo kupitia
www.misstanzania.co.uk kwa ufahamisho zaidi na kujua mengi.

Kwa mujibu wa waandaaji hao wamedai wanakaribisha warembo wote wenye vigezo vinavtotakiwa na kamati ya Miss Tanzania.

Walitaja vigezo ni pamoja na mshiriki kuwa na umri uziozidi miaka 26, na haiba, kipaji na uelewa wakutosha

Zawadi kwa mshindi zitatangazwa baadae, lakini zitakuwa kubwa tofauti na mwaka jana, ambao mshindi aliondoka na kitita cha £1,000 pamoja na taji na alipata tiketi ya ndege ya kwenda kushiriki Miss Tanzania 2007.

Nyote mnakalibishwa na kutoa maoni yenu.
Asante
Mdau London

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...