Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. michuzi naomba kuuliza hapo, wakati edward sokoine aliacha uwaziri hapo kwa msuya, aliacha kwa sababu gani na alikuwa anafanya nini kwa kipindi hicho? sababu inaonyesha alisimama uwaziri mkuu kwa muda then akarudia tena!

    ReplyDelete
  2. Michuzi angalia vizuri hizo tarehe. Mfano Sumaye na Lowassa hawakupokezana siku moja. Kwani Sumaye uwaziri mkuu ulimalizika Kikwete alipoapishwa na sidahni kama alimtangaza Lowassa siku ileile alipoapishwa.

    Inatia shaka hata hizo tarehe nyingine kama tuziamini au ndo hivyo tena.

    ReplyDelete
  3. No offence for the new PM kawa vile hata simfahamu lakini I wish JK angependekeza mwanamke kwa mika hii iliyobaki.

    Yaani mpaka leo hamna mwanamke anayeweza kuwa PM? Give us a chance and see our things.

    ReplyDelete
  4. Anony 7:54 pm

    Yaani Zakhia Meghji ndo kadhihirisha kwamba wanawake bado hawajawa makini katika uongozi, tumewapa wizara ya fedha tu,mnasema eti mlihadaiwa mka sign malipo ya pesa isivyo halali (BOT), sasa tukiwapa uwaziri mkuu hao akina mohammed GIre (richmond) sindo wata wahadaa muwape nchi yote kabisa. Bado sijaona sura ya mwanamke anaefaa kuwa waziri mkuu, wizara yenu ile ile ya jinsia na watoto (ha ha ha ) kikwete akiwanyima basi andamaneni,au basi awape na wizara ya afya maana is reasonable! Huku kwengine , mambo ya nje, fedha, elimu ya juu, miundombinu,kilimo-mfugo,madini- nishati na ulinzi tuachieni kuna hitaji wanaume zaidi.

    ReplyDelete
  5. Si Mchezo kwanza Waziri Mkuu Wa nini Tanzania. Serikali wachague moja kati ya Waziri Mkuu Au Makamu Wa Raisi. Issa Michuzi naona CCM wanachukuwa Ubingwa tu hapo toka TANU waachiye Ligi. Alafu nchi yetu tunamsahau sana Marehemu Sokoine R.I.P. mungu amlaze pema peponi. Wa Africa tunakumbuka viongozi wa nje kuliko Barani kwetu Africa Kama Lumumba kafa kwa utatanishi hakuna mu Africa aliyesema ngoja tuchunguze wazungu walimuulia wapi. na hakuna aliyesema wazungu ni magaidi sie tukienda kinyume na wao viongozi wetu wanaitwa magaidi.

    ReplyDelete
  6. Kwenye hiyo listi jamani...mbona Waislamu wawili tuuu???duh kupambanua mpaka kiama!!!

    ReplyDelete
  7. Hii orodha ndefu kwa nchi kama yetu. Wote hawa wanahudumiwa na pesa ya walipa kodi hadi wafe kama katiba inavyosema? Kama ni hivyo J.K apunguze mawaziri by half nchi iweze kuwapa hiyo huduma. Pia JK aachana na marafiki, wanamwangusha lakini wananchi wako pamoja nawe.

    ReplyDelete
  8. Hili swala la PM mwanamke ni tete,

    Meghji kweli kachemsha, hao sophia simba, Nagu, mama sitta wako too soft ie hawako firm kuweza kuzibiti mafisadi na huo mtandao ambao ulinyemelea kwa baraza letu la mawaziri.

    Labda.... huyu anne kilango, anaonekana ni mkali, ana emotions na machungu ya nchi yake, inawezekana ni changa la macho maana sijui past history ya utendaji wake katika uongozi, Hana kashfa?

    Hivi huyu mama asha rose migiro mbona hasikiki kabisa huko UN? Au na yeye kachemsha? Ametusaidiaje sisi kama watanzania mpaka dakika hii

    ReplyDelete
  9. wewe unayelalamika kuwa hiyo listi ina waislamu wawili nadhani una akili za kuku.Mbona hatujawahi kusikia mkristo analalamika kuwa Rais na makamu wa rais wote ni waislamu?Na upendo wetu kwa Jk ni sawa na upendo tuliowapa MKapa,Nyerere,Mwinyi na kiongozi mwingine yeyote alishika nyadhifa kubwa serikalini.
    Inaelekea wewe ni wale wajinga-wajinga mnaoshinda chini ya mwembe mkicheza "bao",draft,karata na kupiga porojo,hakuna cha elimu wala ujuzi wowote ni kulalamika tu.
    Prof.Juma kapuya alivyowaambia Mpe mtoto elimu,siyo tende.Rudi shule na usomeshe watoto wako kwa hali na mali wafanikiwe maishani siyo kuwang'ang'aniza kwenda madrasat(kupata elimu ya dini) tu na kutojali elimu ya kawaida.Nielewe sipigi vita elimu ya dini(kiislam),nachosema elimu ya dini(kikristo,kiislam,nk) haiwezi kumsaidia mtu maishani.

    ReplyDelete
  10. Wewe Anony 7:54pm huwezi kuchanganua mambo. Aidha elimu yako duni au we ni wa kale. Unahitaji elimu ya jinsia kwa sababu umekandamizwa na mfumo dume. Wanaume unaodai wanaweza uongozi, ndiyo wanaongoza kwa ufisadi na kukandamiza wanyonge. Hizo wizara unazotaka wanaume waendelee kuwepo ndizo zimetufikisha hapa tulipo leo na tutaendelea kila siku kupiga kelele za ufisadi. Wanawake wanaweza uongozi, akiharibu mmoja haimaanishi wote hawawezi.

    ReplyDelete
  11. Asha Migiro ni deputy secretary general wa tatu UN, hao waliomtangulia uliwasikia au hata kuwajua unawajua?. Anafanya kazi yake vizuri na hahitaji kujitangaza. Wanaomtathmini wanajua anachokifanya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...