wadau tulizeni mzuka. mjadala wa ripoti ya dk. mwakyembe unajadiliwa hivi sasa. waziri mkuu mh. edward lowassa ameshasimama na kujieleza, ambapo amedai kuonewa na kwamba hakuna kielelezo kinachoonesha alihusika katika kupitisha zabuni ya richmond. pia amesema hakuwahi kuhojiwa ama kupewa nafasi ya kujieleza na kusikika upande wake.

mmoja wa wajumbe wa kamati teule, mh. seleli alisimama na kupinga hoja hiyo na kusisitiza kwamba mh. waziri mkuu alihusika katika kufanya zabuni ya richmond ishinde.

mh. anna kilango malecela naye alisimama na kumwaga cheche kwamba hata kama itamgharimu ataiunga mkono hoja ya ripoti hiyo. alizua kichekesho kwamba hana urafiki na mtu katika kulinda maslahi ya nchi, hata kama mtu huyo atakuwa ni mh. john samwel malecela.

waziri wa nishati na madini mh. karamagi amesimama sasa na anakana kwamba hahusiki kuandaa ama kuongoza mkataba, na kwamba aliingia wizarani wakati mkataba una umri wa miezi 6 mwezi oktoba.

anasema alipoingia umeme ulikuwa umeshuka sana toka gridi ya taifa na ungezima. swala la kwanza linalosema yeye alishiriki kushinikiza tanesco kufuta mkataba na richmond ili kuweza kumpata mzabuni mwingine na kunusuru nchi katika giza (makekele, na mh. karamagi anamwomba spika amlinde).

inaendelea...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ndugu wadau wenzangu mliobobea kweny masuala ya sheria
    Huku ng'ambo kuna mashitaka ya abuse of power
    ambapo adhabu yake ni kurudisha mshahara woot tuliomlipa au kufilisiwa kiki ambatana na kifungo jela
    sasa hili suala mnalionaje kwani ni wazee wetu ndio wanaoumia mpaka sasa kwa ufisadi wake

    ReplyDelete
  2. Shemeji vipi tena...hapa mzuka hautulii wala nini,tushachukia sana hapa wengine hata kazi leo hatujatulia kufanya mpaka tunataka fukuzwa kwa ajili ya kufatilia sakata hili la rushwa..acha kabisa wewe..acha watu watoe madukuduku yao bwana..we tulia bora watu hawajatukana kwenye blog...
    Jipu limetumbuka...

    ReplyDelete
  3. Ukweli ni Kwamba wakati umefika, viongozi lazima watambue kuwa kuongoza inamaanisha kuwa mtumishi wa wale waliokuthamini kukupatia nafasi hiyo, ambayo kwa upande huu ni wananchi. Lakini viongozi wetu wemejisahau na kudhani kuwa kuongoza ni kujitajirisha kwa gharama za wananchi. Ukweli ni kwamba kuwajibika peke yake sio njia pekee ya kidemokrasia, ni lazima wote waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hii. Kwani kuachia ngazi kila mtu anaweza kufanya hivyo mara aonapo amesha jiibia vya kutosha lakini kama sheria ni ya kweli basi iwawajibishe wahusika wote kama inavyotakiwa. Na Kwa Dereva Wetu JK huu ni wakati muafaka na muhimu kuweka misingi ya nchi ili kuhakikisha kuwa upumbavu na udangayifu na ukacholi wa watu wachache wanaojidai kuwa viongozi hutaendele tena nchini kwetu. Tuna kila sababu kuwa na maendeleo ya hali ya juu, lakini kwa sababu ya wacheche wasiokuwa na vision wala busara wanadhani ni haki yao kuiua nchi yetu kwa manufaa ya wao wenyewe.
    Na KWA WAPIGA KURA WOTE NDANI NA NJE, YOTE HAYA NI SABABU YA NJAA ZENU. MNANUNULIWA KWA VIHELA VIDOGO NA MNACHAGUA WALE WEZI KILA SIKU. WAKATI HUU NI WAKATI WA MAPINDUZI, KILA MPIGA KURA LAZIMA AJUE HAKI ZAKE KWA KILA HONGO UTOAYO NA KUMCHANGU MTU UNAUZA UHAI WAKO NDIYO MAANA TUMEJAZA MAJAMBAZI, NA WALAFI PAMOJA NA WAJINGA AMBAO HAWAJALI MASLAHI YA NCHI BALI YAO. NI LAZIMA UWE MJINGA KAMA UNASHINDWA KUELEWA KUWA HII NI NCHI YETU HATUNA BUDI KUIENDELEZA NA SIO KUIIBIA. PEANENI TENDA LAKINI HAKIKISHA WANAOPEWA TENDA WANAUWEZO WA KUFANYA KAZI WANAZOPEWA. TUMIENI KURA ZENU KUCHAGUA VIONGOZI HALALI NA MUWAJULISHE KUWA YOU MEAN BUSINESS, WAKILETA UJINGA UJINGA MSIWACHAGUE TENA HATA KAMA WANAIMBA NYIMBO GANI NZURI. For the break, lets build our country so we can be happy of our home. Lets end this stupid saga and get to build the country. Na kama JK akishindwa kufanya kazi naye hana budi kuwekwa kando katika uchaguzi ujao. Tunataka viongozi wanadhamini kazi zao na sio marafiki au mashogo zao. Mpe shoga yako kama anaweza kufanya kazi, lakini kama haweze wate watu wenye ujuzi sahihi katika kazi hizo. Tusipeane peane tu, hayo tuwaachie machangudoa kwani wao ndiyo wanapenapeana na wateja wao kwa kiasi kidogo.

    ReplyDelete
  4. Wakati umefika, tuanze kuwajibika lakini na vyombo vya sheria lazima vifanye kazi zake za kuwawajibisha watuvu wote wa nidhamu kama sheria na uthibitisho unavyoonyesha. Tumechoka na UPUMBAVU wa wachache wakati wengi wanapata taabu, ni wakati wa kuweka mambo sawa na kuwaondoa wale wote walio na kasoro na wasiojali maendeleo ya wananchi. Nadhani tuache kuoneana AIBU na tufanye kazi kama tunavyotegemewa, si wakati wa kuonyesha uzuri bali ni wakati wa utendaji wa kazi na kuleta mafanikia ya maana katika nchi yetu. Tujifunze kutoka kwa majirani zetu Kenya, Uganda, na wengineyo wengi. Sababu ya ujinga wa wachache waliodhani sheria ni za kwao wanasababish vifo vya wengi nchini mwao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...