Salaam Bwana Michuzi,
Hongera sana kwa kazi njema sana ndani ya ukurasa wako. Wewe ni mtanzania mchapa kazi hasa, hongera wewe na timu yako.Lengo langu la kuwasiliana nawe ni kuomba msaada wako.
Mimi naishi na kufanya kazi katika jiji la Leicester hapa UK. Ni teaching assistant katika Taylor Road Primary School. Nimeombwa na uongozi kutafuta mashule kutoka Afrika mashariki yatakayopenda kushirikiana na shule yetu ambayo sifa yake moja ni kwamba ina wanafunzi kutoka nchi mbali mbali, zikiwemo zinazozungumza Kiswahili.
Kwa sasa tunazo karibu lugha arobaini hivi miongoni mwa wanafunzi wetu!Kwa kupitia blog yako, tafadhali shule zinazopenda kushirikiana na shule yetu ziwasiliane nami. Wanaweza kuwasiliana nami, nami nitawaunganisha.
Ahsante sana Sheikh Michuzi.
Mdau Leicester


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...