CCM London yampongeza Kikwete kwa uteuzi wa Pinda, na kuwa mwenyekiti wa AU

Na Juma Pinto, London

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Uingereza kimempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi wa Wazir Mkuu Mpya, Mheshimiwa Bw. Mizengo Pinda na kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja wan chi za Afrika (OAU).

Hayo yalisemwa na mgeni rassmi wa shughuli hiyo na ndio mlezi na muhasisi wa tawi la CCM London, Bw. Sharrif Maajar wakati wa sherehe za kusheherekea kwa CCM kutimiza miaka 31 zilizofanyika Reading na kuhudhuliwa na halaiki ya kuwa ya wanachama wa CCM wakiongozi wa Balozi wa Tanzania, Bi Mwanaidi Maajar aliyemsindikiza mumewe.

Bw. Maajar alisema Rais Kikwete ametumia hekima zake kumteua Mheshimiwa Pinda kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuridhia uamuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu baada ya kuhusishwa katika kashfa ya mkataba wenye utata wa Richmond.

“Kweli ni mwana CCM mwenzetu ni mtu mwadilifu wa kusimamia haki, kwa hili sote tumefarijika sana. Tunampongeza Rais Kikwete na sisi wa huku ughaibuni tutampatia ushirikiano wa kutosha,” alisema.

Bw. Maajar alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Kikwete kwa kuteuliwa kwake kuwa mwenyekiti mpya wa OAU,hatua ambayo imetokana na uongozi wake shupavu, hali iliyofanya viongozi wenzake wa Afrika kumkabidhi kijiti cha uongozi wa OAU.

Mlezi huyo wa CCM London alisema Mheshimiwa Rais ameonesha kukubalika kwake hata na mataifa ya nje, hivyo kuna kila sababu ya wana CCM na Watanzania kwa ujumla kujivunia mafanikio makubwa ambayo Tanzania inayapata kupitia kwa Rais Kikwete.

“Kweli amekipata heshma kubwa sana Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo nawaomba wana CCM wenzangu tuendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika juhudi zake za kuleta amani Afrika na maendeleo ya Tanzania,” alisema Bw. Maajar.

Awali mwenyekiti wa CCM London, Bw. Maina Owino alisema tawi lake la Uingereza linaandaa mikakati mikubwa ambayo itatakayokuwa na faida kwa CCM Taifa ikiwemo kuwaanda wana siasa wachanga ambao wako masomoni huku Ulaya ili waweze kukiendeleza chama.

“Kazi kubwa ambayo sisi kama chama ni kuwashawishi vijana kujiunga na chama ili warudipo nyumbani waweze kukijenga na kukiimarisha chama, hivyo tutajitahidi kadri tuwezavyo kulifanikisha hili,” alisema Bw. Owino.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwapa pole raia wa Kenya ambao walialikwa katika sherehe hizo kwa matatizo ya kiaisia yaliyotokea nchini na kusababisha mauji ya halaiki kubwa ya watu wasiokuwa na hatia na kuomba kuwa a subway wakati suluhisho la amani linatafutwa chini ya msimamizi, Koffi Anan.

“Tunawaomba wenzetu kuwa na subira katika wakati huu mgumu kule nyumbani Kenya, lakini tunaamini matatizo ya huko yataisha na Kenya yetu kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Bw. Owino.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Osango, Maina,Maira, Dada Tuli ukivaa tenge!!.....Kidumu Chama cha Mapinduzi

    ReplyDelete
  2. Kujigonga tu, toweni maelezo ya maana sio ooh tunakupongeza. Toweni mampendekezo ya kimaendeleo. Acheni yes sir, yes sir.Toeni maelezo ya umuhimu

    ReplyDelete
  3. ccm london mbona wakenya watupu, kwani wabongo hamna? osango, maira, maina....kajiungeni na kanu au odm, msitafute umaarufu kwa watzee, tunapenda amani na hatuchomani mishale

    ReplyDelete
  4. This is a bullshit! mambo ya kupenda sifa tu, nashangaa hata Mh. balozi anaendekeza ujinga huu ambao ni utengano kwa jamii ya watanzania wote walioko ughaibuni. Kwa nini CCM london? yeye anawakilisha watanzania na sio ccm. Naomba ujumbe huu umfikie Mh. Maajar asifadhili upuuzi wa namna hiyo...kusiwe na kitu kinaitwa ccm london bali kuwe na kitu kinaitwa watanzania london!

    ReplyDelete
  5. ccm tawi la uingereza?? hiyo haiji kabisa. yani bado tu watu wanajipendekeza na ccm hata huku kwa mama??mmh, bora mrudi bongo kama mnakipenda sana hicho chama. huku tunataka chama cha watz waliopo uingereza na sio ccm.igeni mfano wa marekani. hawana vyama vya kisiasa bali vyama vya kuunganisha watz katika states walizopo.

    ReplyDelete
  6. HAWA JAMAA WANAJISAU WAKATI FUTURE YA CHAMA NA WATANZANIA NI KUWAUNGANISHA WANANCHI ILI KUUJENGA UMOJA WA NCHI HASA KWA WANANCHI WALIO NJE YA NCHI HAWA WANAFIKIRIA KUWAGAWA WANANCHI WALIONJE YA NCHI KICHAMA.. WOTE WANAONEKANA NI WAOTA FADHILA YA KUTAPA NAFASI YA KUONEKANA KUKIDUMISHA CHAMA NJE YA NCHI. HASA WAKIFIKIRI WAKIJA KUOMBA KURA NDANI YA CHAMA WATASEMA WALIJIHUSISHA KUHAMASISHA CHAMA NJE YA NCHI. WATANZANIA SASA HIVI KUJUMLISHA NA JIEGRAFIA YAO YA MSINGI WANAIJUA DUNIA HUWEZI KUAMINI. WANAWEZA WAKAKUHESHI MU TUU LABDA HANA HAKIKA WA KUPATA MLO WAKE WA SIKU LAKI VICHWANI MWAO KAMA AKIWA NA UHAKIKA WA MLO NA MALAZI KAMA KWA MWAKA HIVI UTASHANGAA UWEREVU WAO. NNABIDI MJIHARIFU WENYEWE MAANA UMOJA WA TAIFA NINI. KAMA ILIVYO VUMISHWA HIVI KARIBUNI MZEE ALIKUWA TAYARI KUTOA UWAZIRI KWA WATUNGA SHERIA KUTOKA UPANDE MWINGINE ILA KILICHOENEKANA NI KUTOKUWA TAYARI KWA UPANDE MWINGINE KUHISI KWAMBA RUNGU LAO A KUKOSOA MAOVU LITAPUNGUA HASA WAKATII HUU AMBAO SERIKALI IMEKEMEA MAOVU BILA WOGA , KWA HIYO WALIHISISI JOTO LITAPUNGUA NA UPANDE MWINGINE ULIHISIWA KUWA NA HOFU YA YA KUTOKUWA NA MUDA WA KUREKEBISHA MAMBO PINDI IKIWA WATAANZA KUSHAMBULIWA KWA MAMBO YANAYOONEKANA KABLA HAWAJA YAFANYIA KAZI. USHAURI WA BURE KWA CHAMA TAWALA INABIDI KIWE KINA SEMA MAOVU BUNGENI WASIJE BAKIA KUGOMBANIA ALITOA HOJA WA KWA NZA KWA WANANCHI.ILA KATIKA VIKAO VYAO WANAAMINI KABISA KWAMBA UKITAKA UPATE UBUNGE INABIDI UWE CHAMA TAWALA. INAWEZEKANA ISIWE KWELI KWANI INAWEZEANA CHAMA TAWALA KIKAKUPITISHA LAKINI VILE VILE CHAMA KIKAKUONA HAUFAI ILA WANANCHI WAKAPEWA RUNGU WAKAKUPIGA CHINI. KAENI MTULIE FIKIRINI MNATAKA KUWASAIDIA WANANCHI AU MATUMBO YENU. NAJUA MKIRUDI NYUMBANIA KIAPATO KINASHUKA SASA MSIJARIBU KUOTA KWAMBA SIASA NDIO ITAKUWA MKOMBOZI WENU YA MATATATIZIZO YA UCHUMI.KUWENI NA MIOYO MISAFI MNAPOTAKA KUWATUMIKIA WANANCHI SIA MANENO MATAMU NAFIKIRI MIOYO MISAFI HAIHITAJI MJADALA NI KUBADILIKA NDANI KWA NDANI NA KUTENDA.YOU DONT ONLY HAVE TO BE SYMPATHETICAL BUT ALSO EMPATHETICAL. YAANI SIO TUU UONE HURUMA MATATIZO YA WANANCHI INABIDI UBEBE MZIGO WA MATATIZO YAO

    TUMAINI GEOFREY

    ReplyDelete
  7. Duh...yanga tupu hapo jamani...

    ReplyDelete
  8. Kama hao CCM wa London wana uchungu na nchi, kwa nini hawakumpongeza Dr. Slaa alipoanza kuwafichua mafisadi? Hao mafisadi wamestawi chini ya utawala wa CCM, na wamelindwa muda wote na hii hii CCM, na katika watuhumiwa wakuu, CCM wamo. Akina Dr. Slaa walipoanza kuwafichua, wabunge wa CCM waliwadhalilisha hao akina Dr. Slaa. Je, wanaCCM wa London kwa nini hawakutamka lolote? Hongereni sana wanaCCM wa London. Zidumu fikra zenu.

    ReplyDelete
  9. Michuzi, naomba upunguze politics kidogo. Hiki chama wengine hatukependi so we feel little offended kukiona kila tukifungua website yako.

    ReplyDelete
  10. WADAU HII HOJA NI NZITO KIDOGO NILITAKA KUICHANGANYA NA ONI LANGU LA KWANZA ILA NIKASITA NAOMBA NI WEKE WAZI KAMA UNAKUMBUKA WAKATI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRICA NYERERE ALIKUWA ANAFUNGUA MATAWI YA VYAMA KAMA FRELIMO, PNC ANC NA VINGINE ILI KUKOMBOA NCHI KATIKA UKOLONI PIA NCHI NYINGI ZA ULAYA MASHARIKI NA ZA MUUNGANO WA URUSI ZILIKUWA NA SIASA KAMA HIZI. NIA NA MADHUMUNI NI KUPINGA SEREKALI ZINAZOTAWALA NCHI YAO. HAIWEZEKANI HATA KWA UCHAWI AU MUUJIZA UKAMUHAMASISHA MTANZANIA ALIYEENDA UINGEREZA AU NJE YA NCHI JIUNGE NA CHAMA AKIWA NJE YA NCHI(LABDA UMUHAKIKISHIE ULAJI). HAYA NI MAMBO YA WAKIMBIZI WA KISIASA NA WAPINGA SEREKALI MUWE MAKINI MSIROPOKEROPEKE NA KUTENDA MAMBO HAMBAYO HAUYANA MFANO WAKIHISTORIA. PASPORT YAKO IMESHIKILIA OMBI LA RAIS WA NCHI SIO MWENYEKITI WA CHAMA.UNATAKIWA UJUE HUKO NJE KWA UTANZANIA WAKO SIO KWA UCHADEMA.IKIWA UMEALIKWA NA CHAMA LABDA LABOUR PART KWA SEMINA YA KISIASA HAYO NDIO MAMBO UNAYOTAKIWA UWAFAHAMISHE AU UWAELEZEE WANANCHI. HILI SOMO NIGUMU SANA KWELI NASIKITIKA NAWEZA MSILIELEWE KWA VIZAZI KWA HUO MTINDO WENU WAKUSAHAU UTANZANIA WENU MKIENDELEA HIVYO ITABIDI TUWAPATIE KADI YA CHAMA KAMA HATI YA KUSAFIRIA.

    TUMAINI

    ReplyDelete
  11. Afadhali MUMEWAANGUKIA kichizi na kujipendekeza kwao.
    Ningeshangaa sana maana NDUGU yangu BARAKA KANGE mulimgombania sana nyinyi, kama mpira wa kona!
    Khaa!

    ReplyDelete
  12. Point well put,Mr Tumaini nakubaliana na maelezo yako ya pili 100%,mimi naipenda CCM unlike those who hate it lakini nafikiri tukiwa kwenye nchi za watu ni bora zaidi kujivunia Utanzania wetu kuliko U-CCM wetu haileti maana,kama umealikwa nchi ya nje kuja elezea maswala ya CCM poa lakini sio kama hawa wenzetu wanao jaribu kujipa umaarufu kupitia CCM,warudi bongo watangaze hizo siasa zao we are not interested,sisi kama watanzania tunasema hatuhitaji CCM-UK tunahitaji umoja wa watanzania UK no matter what party you support.Na Michuzi nafikiri ungejirekebisha kwa hili hizi organisation za CCM abroad zinapo kutumia picha zao na message uwafahamishe kama usingependa kuonekana una favour one particular party on your blog.I think it's enough seeing JK,Pinda and the rest of them in your blog each day,let alone adding these low life good for nothing fame-grabbers.

    ReplyDelete
  13. Wewe anon feb 14 2:30
    sasa we mbona unamfundisha michuzi kazi. Nafikiri na wewe ukituma picha zako( chadema,nccr mageuzi nk) ataziweka tu kwenye hii blog, hajasema wana ccm tu ndio watume picha zao. Kama walivyosema wengine ingekuwa vizuri kuwe na chama cha WATANZANIA) hiyo inaeleweka. Kwa hiyo Go Ahead with with your part member and send your comment and phote to michuzi ataziweka tu kwenye blog ili mladi hazichafui hali ya hewa, we will be happy to read them and give out our comment. God bless Tanzania na vyama vyake vyote

    ReplyDelete
  14. hawa jamaa hawana habari na nchi. kwanza lazima wengi wao wamejiandikisha ukimbizi toka somalia, pili wanasoma nje kwa kutumia hela walizoibiwa wananchi bongo tatu wanajipendekeza kwa ccm ili wakirudi nyumbani washikie mkanda na kuendelea ufisadi alioanza mtakatifu nyerere. yote haya hayana faida na mtanzania maskini aishie kijijini ambae toka enzi ya nyerere walikuwa wanaomba maji safi tu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...