Ndugu watanzania wenzangu,
Kwa niaba ya dada yetu Diana Thamage Kibodya, familia yote ya Kibodya, ndugu, jamaa na marafiki,tunauchungu mkubwa moyoni kuwatangazia kuwa Mama yake mzazi wa Diana Kibodya amefariki dunia huko South Africa.
Tunawaomba wanajumuia wote mjumuike na wenzetu kwa hali na mali, katika> wakati huu mgumu wa maombolezo. Marehemu Martha Thamage alikuwa na umri wa miaka 71.
Diana anategemea kwenda South Africa haraka iwezekanavyo ili akawahi mazishi, na mnaweza kuwasiliana nae kumpa pole yeye mwenyewe, simu ya nyumbani 413-782-6310, au wasiliana na ndugu yetu Isaac Kibodya simu 413-219-1153, kwa niaba ya wanandugu wote.
Tunawaomba wanajumuia wote tuwakumbuke wenzetu katika maombi, na kama ilivyo kawaida yetu kusaidiana katika kila hali wakati wa msiba mzito kama huu.
Mwenyezi Mungu amjalie marehemu mama, alale mahali pepa peponi, amina.> Stephen Tomi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pole sana Dada Diana. May you Beloved mother rest in eternal peace.

    ReplyDelete
  2. SASA NI WA SOUTH AU WABONGO MBONA UMESEMA WANASAFARI KWENDA SOUTH KWENYE MSIBA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...