Kwa niaba yangu binafsi na wananchi wote wenye uchungu na taifa lao na haswa wale ambao wamekuwa wakiomba usiku na mchana juu ya nchi yetu,ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Dr Mwakyembe na kamati nzima ya bunge kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuweka ukweli wa ufisadi unaofanywa na viongozi wetu ambao tuliwapa dhamana ya kutuongoza.
Nimeipitia ripoti ya Dr Mwakyembe kama ulivyotuletea katika mtandao wako kwa makini sana. Katika ripoti hii nimehuzunishwa sana na jinsi ambavyo baadhi ya viongozi wamekuwa mstari wa mbele kukataa kutoa ushirikiano kwa kamati halali iliyochaguliwa na bunge kufanya kazi hiyo huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kubwa.
Kwa miaka mingi kanisa limekuwa likimuomba Mungu awafichue hawa watu wanaotafuna mali ya taifa letu bila huruma. Ninafuaraha kubwa kuona sasa Mungu anajibu maombi yetu wazi wazi.
Kwa niaba ya wapenda amani na haki ya taifa letu Tanzania,tunamuomba Raisi wetu mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete achukue hatua za haraka ili kututhibitishia anayonia ya kweli ya kupambana na rushwa kubwa kama hizi.
Mapendekezo yote ya kamati ayafanyie kazi mara moja kikao cha bunge kitakapo maliza mjadala wa hoja hiyo. Kwa kuwa mambo yanoyosubiri kauli za Raisi yanakuwa mengi kila siku,ninamshauri Raisi apunguze msongamano wa mambo ambayo wananchi wanahitaji majibu yake kama ifuatavyo,moja kutueleza aliyekuwa gavana wa benki yuko wapi na kama yupo Marekani kwanini hajachukua ushauri wa balozi wa Marekani nchini Tanzania wakumrudisha nyumbani kwa ajili ya kesi.
Mbili, majina ya vigogo wa madawa wa kulevya yako wapi mbali na viongozi wa dini kama Bishop Mokiwa na viongozi wengine kuomba yatolewe hadharani.Tatu kama mbunge wa Karatu Dr Slaa anatoa habari za uongo juu ya mafisadi,kwanini asifikikishwe katika mkono wa dola! na kama anayosema ni kweli kwanini wahusika hawa wajibiki kwa kuachia hizo nafasi wanazozisimamia na kufikishwa katika mkono wa dola.

Ninapenda watanzania ambao tumewapa dhamana ya kututawala wajue kanisa halitalala, litakesha katika maombi mpaka kila moja ambae amechukua haki zetu anakutana na mkono wa Mungu.Kanisa litahakikisha hizo mali walizoiba hazitawasaidia wao,watoto wao na hata vitukuu vyao.

Mungu ibariki Tanzania,

Mungu bariki viongozi waadilifu.
PASTOR ABISALOM NASUWA
DALLAS BAPTIST UNIVERSITY,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mwambieni huyo Pasta, katika hali ya kawaida huwezi ukasema "kwa niaba yangu mwenyewe", wakati unayesema/zungumza ni wewe mwenyewe.
    Huwezi kuwa na niaba yako wewe mwenyewe.

    ReplyDelete
  2. Kifimbo hako kastaili ka kusema "kwa niaba yangu binafsi" kalikuwepo miaka ya tisini hususani kwa wanasiasa na watu wa kada mbali mbali wakati wa kutoa shukrani.

    Naona huyu Pastor aliondoka Bongo siku nyingi na bado anakaendeleza

    ReplyDelete
  3. WAZIRI MKUU EDWARD LOWASSA AMEJIUZULU, AMEACHIA NGAZI HUREEEEEEEEEE. SASA ANA JINA JIPYA ''ALIYEKUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA.....NDUGU LOWASSA'' BWANA ASIFIWE SANA.

    ReplyDelete
  4. Kwa waombaji wote waaminifu, tunawaomba wote tumwombee ulinzi Dr. Harrison Mwakyembe ambae ametoa taarifa nzito sana bungeni. Ulinzi wa Dr H. Mwakyembe utaweza kusaidia hata wale amabao wameteuliwa katika kamati za kuchunguza mikataba yenye hitalafu na kuzuia rushwa wawe na moyo, ari na nguvu ya kuweka mambo hadharani.

    Mbarikiwe wote.

    ReplyDelete
  5. Swali hapo au msaada kwenye tuta kaka michuzi je aliyekuwa waziri mkuu ataingia bungeni kama mbunge wa kawaida kuwakilisha wananchi wake wa monduli au huko nako ataachia kamba? nasikia kaka michuzi ni mwandishi wa habari hebu dodosa hilo utusaidie. Au atajiuzuru na ubunge,tujiandae kumuaandaa mtoto wa marehemu sokoine akagombee. i cant wait utamu kunoga yiiihaaa

    ReplyDelete
  6. Nakuunga mkono Pastor, Kamati hii inastahili kupongezwa na kutangazwa kuwa ni mashujaa wa wakati huu. Ni vyema vijana walio Tanzania waandae maandamano ya kuipongeza kamati. Kusiwe na maandamano kwa kulalamikia tu serikali bali pia wakati pongezi zinapostahili tuandamane kwa kutoa pongezi...zemarcopolo

    ReplyDelete
  7. Kifimbo na anon wa pili huwa nafurahi sana nikiona mtu anajali sana na kuchagua maneno fasaha wakati anapoongea hasa kuandika, pia nafurahi sana ninapoona watu wanakuwa waangalifu wanaposoma matamshi yasiyohitajika katika sentensi inapoongelewa na kutoa msaada, hukarahika sana pale mtu anapoweka herufi m-badala kwenye sentensi na kuharibu maana ya neno zima au huleta maana tofauti kabisa m.f bakola, zalula, maadiri, samani na thamani nk.
    naamini kuna wengi wanajifunza maneno magumu humu kwenye maongezi yetu ya hapa na pale, na wengi wanajikumbusha maneno ya zamani wanayokuwa wakiyakosa kwa sababu ya kuwa mbali na waongeaji wa lugha yetu.

    Mchungaji, asante kwa paragraf ya nne hapo umetuwakilisha vema mungu akubariki.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  8. Pastor, asante kwa ujumbe wako mzuri. Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  9. Huyu jamaa huwa anapenda kuonekana kama na yeye yupo, kwa "niaba yangu binafsi" namshauri asitafute umaarufu kwa njia hii.

    ReplyDelete
  10. PASTOR NASUWA WEWE MMACHAME?nina ndugu wa jina kama lako..mdau norway

    ReplyDelete
  11. Pastor,

    Huu ujinga wote unaoendelea Tanzania na Africa NI swala la utamaduni. Msaada, mafunzo na muongozo wa dini utatusaidia sana katika kuokoa jahazi.

    Ni tatizo litakalo chukua vizazi ili liishe na ni nyie viongozi wa dini mnaotakiwa kuhubiri ubaya wa ufisadi na kuwashauri waumini wenu waupige vita ufisadi kwa hali na mali.

    Ahsante sana kwa mchango wako Pastor.

    ReplyDelete
  12. Kwa kweli huyu Pasta nawaswasi kidogo na yeye mwenyewe binafsi, nakukumbuka kuna wakati huyu jamaa (pasta Nasuwa) alikuwa anagombana na pasta mwenzake kuhusu $ na uaaminifu kwa ujumla, jee yeye ameshajirekebisha? nakutumia kanisa sioni kama ni suala la maana hapa tupo kutoa mchango kwa nchi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...