
Michuzi!
hii picha mzeee ni siku nilipokuwa nimevuta nondo yangu ya masters in software engineering juzi tu. je umeoana jinsi wenzetu wanavyovaaa sio majoho mzeee! ni kimtindo mtindo tu yaani. mie hapo nimepiga kizibao na ua jekundu kama siku ya valentine nikiwa na wadau wa mataifa kibao huku trollhatan, sweden, chuoni west university.
Alphonce, Magori
Majoho yana hadhi yake.Ukipata nondo yako unavaa joho kuonyesha status yako and what you've achieved.Mimi nikiangalia picha yenu it's hard to believe umepokea nondo.Najua cheti chako ni muhimu zaidi lakini joho pia lina nafasi yake katika siku kama hii.Nchi nyingi zinataka kuanzisha hiyo system but I think it's a bad idea.
ReplyDeleteJoho ni kind of business...Mbona USA sio lazima uende kwenye commencing ceremony. Na kama huendi joho sio lazima kununua ...
ReplyDeletepeople pay so much mind juu ya majoho wakati cha muhimu ni diploma yako.
Ingawaje it is nice ukichukua nalo picha lakini pia yapo majoho ya kurent kwa picha tu...Joho bei mbaya sana mimi ninayo mawili na nimevaa maa moja tu...wastage of money...nilikua sijajua mchezo wa kurent
Hey Mr. Alphonce Magori,
ReplyDeleteMilima haikutani! Uko wapi sasa aise. Hajambo mdogo wako JUSTIN MWENGELE? Nakumbuka enzi za DARUSO mazee. Tangu tuachane ROOM, HALL 5 - UDSM - 2004. Tuwasiliane mzee kwa anwani ya barua pepe hapa chini. Hongera kwa nondozzzzzzzz!
Tuwasiliane,
Mr. M. MWIPOPO,
makmwipopo@yahoo.com
U. S. A
WABONGO BADO WAKO KWENYE KARNE YA KUJALI UMEVAA NINI NA SIMU YAKO NI AINA GANI, KAMA UNA KITAMBI MAMBO SAFI, KAMA UKO FIT MWEMBAMBA UNAAMBIWA VIPI NJAA? SASA UKIWAONYESHA JINSI WATU WALIVYO SIMPLE HAWAWEZI KUAMINI!
ReplyDeletehongera sana ndugu Magori kwa kujipatia nondozz.
ReplyDeleteLakini naomba kuuliza, unaposema "wenzetu" wanavyovyaa unamaanisha nani? Waswede? Kwani wao ndio standard ya uvaaji katika gradu? Au unamaanisha wenzetu kwa maana ya wazungu? Sio kwamba kwasababu waswede (or for that matter wazungu in general) wakiamua kutovaa majoho ina maana na sie tusivae majoho. Isitoshe, kuna vyuo vingi duniani vikubwa na vyenye umaarufu na heshima kimataifa kuliko University West - Startsida, ambavyo huvaa majoho mzee.
Hayo maoni yangu binafsi tu mzee. Once again, hongera sana.
hii nadhani ilikuwa semina ya kuboresha mazingira si mnaona kila mmoja na kauwa chake mkononi?hapo hamna nondoz wal;a nini
ReplyDeleteYou got it Mtatifikolo!
ReplyDeleteSuala la Majoho limejadiliwa sana katika anga mbalimbali. Mimi sipendi ile mitazamo miwili ya ki-akademisentriki isiyo na kiasi (extremes)ifuatayo:-
1.Wale ambao sasa wakiona mtu hajavaa joho popote kama wao wanasema kuwa hakupata nondo au kwamba nondo za huko ni feki. Hawa huweza kugubikwa katika suala la majoho kiasi cha kukosa kuweka nguvu katika mambo mengine pia mfano uboreshaji wa uthamani wa elimu yenyewe inayotolewa.
2. Wale ambao wakiona wengine wamevaa majoho wanasema huo ni ushamba na kutafuta sifa na kutokuwa wa kisasa. Hawa pia huweza kuhukumu wengine kuwa si wachumi kutokana na matumizi mabovu ya fedha katika kununua au kuazima majoho.
NISEME KUWA, UVAAJI AU KUTOKUVAA MAJOHO WAKATI WA GRADU NI SEHEMU YA DESTURI MBALIMBALI ZA AKADEMIA KATIKA HUU ULIMWENGU.
NA KILA SEHEMU INABIDI WAHESHIMU DESTURI WALIZOJIWEKEA KWA KIASI BILA KUTEMBEA NA HUKUMU ZISIZO NA MISINGI JUU YA WENGINE WANAOTOFAUTIANA NAO.
Namaliza kwa kuwarushia Kituko cha Unafiki:
Kwa desturi ya nilipokuwa nasoma kuna msisitizo kuwa wakati wa gradu hakuna cha majoho maana siyo kitu muhimu. Hivyo siku hiyo wahitimu wanatakiwa kuvaa (kiheshima) mavazi yao YOYOTE wanayopenda.
Hata hivyo katika uchunguzi wangu hakuna mtu aliwahi kunijibu kwa nini sasa Maprofesa wenyewe hawaachi majoho wakati wa gradu kama si muhimu?
Kutokana na uhuru huo tuliopewa na kwa kuzingatia mazoea na mapendeleo ya utamaduni wetu tuliyokuwa nayo toka katika vyuo vinavyojali majoho kwa wahitimu, mimi na rafiki yangu tuliamua kutesti litimasi.
Siku ya siku ikafika watu wengine wengi)wakawa wamevuta suti zao, wengine jeans na mashati tu, wengine majoho ya kifalme ya ki- Naijeria na wengine magauni makubwa yenye rangi za kuvutia na mishipi toka Uchina n.k
----------- baada ya muda --------
Ilipofika zamu ya darasa (course)yetu kusimama kando tayari kupokea nondo Mimi na Rafiki yangu tukatoka kidogo, kwa spidi ya 180 huko nikamvika rafiki yangu JOHO LA GRADU KAMA LINAVYOELEWEKA NCHINI KWETU NA KWA NCHI YA RAFIKI YANGU NA KOFIA YAKE YA TARABUSHI juu!
Ahstaghafullah! yaani alivyotokeza tu (akiwa na mfanano wa Maprofesa) kila mtu meza kuu (kwa Maprofesa) walianza kuhangaika na kutahamaki hususani Dean of Academics na Rector; huku ukumbi wote uliosheheneza zaidi wanafunzi ambao wengi walitoka katika nchi zenye desturi ya majoho, jamaa za wahitimu na watumishi wengine wa Chuo ukilindima kwa vifijo na nderemo!
Iliwachukuwa kama dakika kumi hivi wakuu kushauriana pale meza kuu nini kifanyike, yaani aambiwe kuvua au la. Tulisubiri hiyo amri itoke ili tuukarabati unafiki papo kwa papo lakini hekima ikawaongoza wakaendelea na utaratibu. Jamaa yangu alikabidhiwa nondo yake huku watu wengine wakiwa wamenuna.
Na toka siku hiyo, yaani graduation zote zilizofuatia, ikaandikwa kwa maandishi na kuwekwa lakiri kwamba, 'WAHITIMU WANARUHUSIWA KUVAA MAVAZI YAO MENGINE YOYOTE WANAYOPENDA LAKINI YASIWE HAYO 'MAVAZI RASMI YA KUHITIMU',
Hapo ndipo niliponyanyua karatasi ya litimasi iliyobadilika rangi kama tulivyotasnifia kuwa HAKIKA SI KWELI KUWA MAJOHO YA GRADU HAYANA MAANA PALE BALI YALIKUWA NA MAANA ZAIDI KIASI KWAMBA INABIDI YAVALIWE NA WASOMI WALIOKUBUHU MAPROF TU, VINGINEVYO KWA NINI SASA KIROHO KIKUUME WAKATI UMESEMA TUVAE VYOVYOTE NA KWAMBA HILO JOHO HALINA MAANA YEYOYE ?????????????
Kama watoto wa chekechea tu wanavaa majoho siku hiz wala sion kama kuna ulazima sana wa kuvaa hayo majoho cha msing ni kuipata degree yako thats all hongera sana mdauuuuu
ReplyDeleteHIVI MBONA NYIE MAANONYMOUS MNAMIND VITU VIDOGO?JAMAA KAPATA MASTERS YAKE AND HE IS PROUD OF IT THAT IS WHY AME POST HIYO PICHA SASA MNAVYOANZAN KUSEMA KUWA HAMNA NONDO WALA NINI MNAONYESHA JINSI MLIVYO NA CHUKI BINAFSI(HATERS!!!!)
ReplyDeleteOF COURSE BWANA MAGORI ALITAKIWA ASITUELIMISHE KUHUSU KUVAA AU KUTOVAA MAJOHO MAANA ITS NOT THE JOHO THAT MATTERS ITS THE DEGREE IN YOUR HAND AND OFFCOURSE THE KNOWLEDGE YOU GOT FROM YOUR DEGREE MAANA KUNA WENGI WENU SIKU HIZI MNA MAKARATASI LAKINI NI VIHIYO lol
ANYWAY HONGERA SANA BWANA MAGORI KAMA BADO UPO SWEDEN TUWASILIANE MIMI NAISHI HUKU NAFANYA KAZI KAMA SOFTWARE DEVELOPER NA PIA NASOMA MASTERS IN SOFTWARE ENGINEERING MANAGEMENT AT LINKĂ–PING UNIVERSITY
Monday, February 4, 2008 11:41:00 PM EAT
ReplyDeleteAnonymous said...
hii nadhani ilikuwa semina ya kuboresha mazingira si mnaona kila mmoja na kauwa chake mkononi?hapo hamna nondoz wal;a nini
AHAHAHAHAHAH, WEWE NI KIBOKO JAMANI, ULIKUWA UNAWAZA NINI?? KAZI KWELIKWELI, MIMI SIMO.
mimi nampongeza sana Magori kwa kumaliza masters yake, ni safari ngumu.Majoho huwa ni protocal tu.Siku hizi hata chekechea wanayavaa!
ReplyDeleteMasters ino kichwani(ni maarifa) na sio katika majoho.
Juma M.
Huyu kaka ana tabia mbaya sana.Akitongoza mwanamke akimtolea nje yeye hudai ameshalala nae.Yaani ana akili mbovu sana
ReplyDelete