habari kaka michuzi,Ni kweli kabisa JOHN MJEMA amefariki baada ya kujichoma kisu cha shingo. nimezipokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa sana ukizingatia kwamba MJEMA alikuwa rafiki yangu mkubwa sana. Nilimwona mara ya mwisho nilipokuja bongo mwaka jana mwezi wa 7, kwa kweli hali yake ilinihuzunisha sana kwani kwa mtu aliyekuwa anamsikia tu na kumwona kwenye tv angekataa kuwa ni john mjema.
Kaka michuzi, najua kuwa wengi wataandika na kusema mengi juu ya kifo cha hayati Mjema bila ya kuangalia ni sababu zipi zilizopelekea yeye kujiua. Sikubaliani na adhabu aliyojipa ya kujiua, lakini nahisi vitu alivyokuwa anawaza kichwani bila ya kupata msaada wa kimawazo na ushauri wa waliokuwa marafiki zake wa karibu ndio iliyopelekea leo hii tumpoteze John.
Hali ya john alianza kama utani kubadilika. Kwani mara baada ya babaake mzazi kufariki John aliniambia kuwa ''nilifiwa na mamaangu mzazi mikononi mwangu na leo baba amenifia mikononi mwangu''.
Baada ya kumzika babaake, John alianza kubadilika tabia. Akaanza kuvaa nguo za ajabu ajabu tofauti na jinsi alivyokuwa smart. Watu walikuwa wanamchukulia kama msanii na wengine wakawa wanaseama jamaa ni shushushu kwa kuwa alikuwa anafanya kazi IKULU. Kumbe mwenzetu ndio alikuwa anaelekea kuchanganyikiwa.
Muda si mwingi John akawa anafagia nyumbani kwake akiwa uchi wa mnyama na watu wakimuuliza kwanini unafanya hivyo; alikuwa anasema yupo nyumbani kwake. Kipindi anafanya mambo hayo mimi nilikuwa nimeshasafiri kuja UK.
Hali yake iliendelea kuwa mbaya. Ndugu zake wakawa wanajitahidi kumtibia ila kama kawaida yetu waswahili wakaanza kusema kuwa John kalogwa (sitaki kuelezea hapo kwani sina hakika)wengine wakasema unga,wengine bangi. Basi mradi kila mtu alisema lake.
John alipelekwa Lushoto kutibiwa na inasemekana alipona na kurudia hali yake ya kawaida...Hivyo nilipopigiwa simu muda mfupi baada ya Jo,hn kujichoma kisu nimekaa na kujiuliza vitu vingi nilivyokosa majibu. Lakini nimegundua kuwa kitu kilichomchanganya john na kufikia hatua aliyofikia ni:
(1)Kukosa msaada wa mawazo mapya kutoka kwa watu aliokuwa anawaamini yeye. Mfano wasanii wenzake, maDJ, na baadhi ya watangazaji ambao walikuwa marafiki zake, kwa sababu john alianza kulalamika kuwa anabaniwa katika suala zima la muziki. Babaake akawa analalamika kuwa John anapoteza pesa zake za mshahara kwa kufanya muziki ambao haumlipi. Hivyo aliamua kuachana na muziki akiwa na album ndani, ambayo wahindi waliikataa kwa shinikizo la mmoja wa watangazaji wa ***** Fm!
(2)Akiwa ktk hali ya kuchanganyikiwa na muziki wa bongo flava, akafiwa na babaake mzazi
(3)Alipokuwa ktk hali ya kuumwa nadhani alipoteza kazi
(4)baada ya kupona na kutambua hali aliyokuwa nayo wakati anaumwa na mambo ya aibu aliyokuwa anayafanya kuna uwezekano kuwa alikosa councelling - hivyo kuona njia pekee ya kuondokana na adha na aibu aliyoipata ni bora KUJIUA.
Naamini kabisa kuwa ugonjwa wa john wengi walikuwa wanauelewa lakini wapo baadhi ya wasanii ambao walikuwa karibu nae walikuwa wanafanya siri, kwa kuona labda wanamshushia heshima mshikaji. Kumbe wanamwangamiza.
Hivyo ombi langu kwenu wasanii na maDJ mliopo Dar, mwende Mtoni Kijichi karibu na shule ya NELUKA ambako ndiko nyumbani kwa JOHN MJEMA, mkashiriki ktk kumzika rafiki yetu mpendwa Ni mimi rafiki wa JOHN MJEMA.
MOLA AIWEKE MAHALA PEMA ROHO YAKE PEPONI - AMINA
INNA LLILLAH WAINAH.................
(USITOE EMAIL YANGU)
nenda http://www.eastafricantube.com/search/John/ umsikilize na kumuona Marehemu John Mjema
RIP John.to other fellas jamani stop smoking this thing inaua ubongo na ukichanganya na matatizo ya Dunia ndio hivyo tena like britney lk other folks.Tanga kuna hospitali za kichwa na Dom yeye alipelekwa tanga akapata nafuu ila ndio hivyo tena.sio uchawi wa kugombania mali
ReplyDeleteLoh, jamani poleni sana kwa msiba huu. Mie kwa kweli simfahamu marehemu wala kuwahi msikia, lakini story aloandika rafiki yake hapo juu imenisikitisha sana.
ReplyDeleteJamani watanzania huwa twapenda kufagilia wakati wenzetu wako kwenye shida, na kama anavyosema rafiki yake hapa ni sahihi, basi jamani tuwe na upendo na huruma kwa wengine.
MUNGU AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU. AMINA.
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.
ReplyDeleteRIP kaka John, I dont know him, but he is in better place right now. No more pain tears, mateso na ufisadi kashakwepa.
ReplyDeleteKwako unayejiita rafiki yake wa karibu, where were you hadi akafikia apa! kama rafiki wa karibu what did you do to help him? ulimsaidia kimawazo? kumhimiza aende kwenye counseling, au ulikuja toka Ulaya ukamwangalia anavoteseka ukaishia zako UK! Shame on you kuja kulia lia apa baada ya mauti kumfikia, why didnt you do something! I have a feeling kwamba wala humfahamu wala sio rafiki yake wa karibu ni kuonyesha tu unajua kila kitu kumbe hujui! I remember Chifupa alipofariki kuna mbwiga mmoja alijitokeza akasema yeye alikuwa rafiki yake wa karibu na amina alipokuwa ana depression alimsaidia kimawazo and bla bla! apo ukute hata hawakuwa wanafahamiana, ni kutaka kupata umarufu tu. Ushauri, kama una rafiki yako wa karibu ana shida msaidie, huwezi msaidia moja kwa moja mshauri cha kufanya au pa kupata msaada, usingoje afe ndo uje utueleze mlivokuwa mmeshibana, thats crap, and nonsense.
RIP kaka wa watu! too young to die, but what can we do, what is done is done. He is in better place if he believed in LIFE AFTER DEATH! nawakilisha.
MASIKINI INATIA HURUMA SANA UNAJUA STRESS INAUWA WATU UNAJUA WATU TUMEZOEA KUSEMA TU Iam stressed honestly we dont know what stress it is I have seen my self my close relative who died for stress
ReplyDeleteMhn, mi nafikiri hili neno la nyeti za nanihiiiiii, umelitumia vibaya hapa kutokana na upeo wangu wa lugha ya Taifa, ktk miaka ya 90 tulikuwa na maana ya sehemu za siri, lakini wewe naona unazungumzia habari ya kusikitisha kwa kumpoteza mwenzetu haya!!!!!!!!!!!!. Mungu amlaze pema peoponi kamanda, wote tu njia moja
ReplyDeleteHalafu we Michu hii lugha umetumia ina utata, mimi nilidhani "sehemu zake za siri" (Nyeti za Mjema).
ReplyDeleteJamani inasikitisha lakini kupoteza kijana kama yule.Poleni sana wanafamilia na wapenzi wote wa music wa ubongo wa fuleva..
Mungu akusamehe yote John Mjema.wote njia moja
Nasema kwa familia ya marehemu na marafiki zake wote ukiamo wewe mleta taarifa pia kuwa poleni sana.
ReplyDeleteNanukuu
"..nimezipokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa sana ukizingatia kwamba MJEMA alikuwa rafiki yangu mkubwa sana..."
Mdau mleta taarifa, nashukuru kwa ufafanuzi wako ingawa umeniacha mimi na maswali mengi kuliko majibu.
1. Mimi sijui wewe ukiwa na sifa iitwayo RAFIKI YAKE MKUBWA SANA ulitoa ushauri gani maana hujatueleza hapa na umejaribu kutueleza kuwa kukosa ushauri nasaha wakati wa shida zake ndio inawezekana kuwa sababu ya kufikia kujiua.
2. Kama unasema wengine 'walifanya siri' juu ya ugonjwa wake kwa nini wewe 'hukufanya wazi'kama unafikiri hiyo ingesaidia? Ulisubiri afe ndio leo ufanye wazi au?
3.Mbona bado nawe unaendelea kufanya siri juu ya huyo Mtangazaji fisadi mwenye roho ya dhuluma kwa kumwita 'wa ....FM'? Huoni kuwa unazidi kumpa ukimbizi mtu huyo aendelee kuwaumiza wasanii wengine ambao nao wanaweza kujiondoa kwa staili hiyo?
4.Duh! sikujua kuwa Tanzania eti bado tuna Wahindi fulani maalumu ambo ndio wao pekee wenye monopoli ya uproduza au uuzaji wa kazi za wasanii? Kama ilikuwa ni kazi nzuri, hivi kweli ungemshauri kuwaona watu wengine nje ya hao Wahindi maalumu hiyo kazi yake isengekamilika na kuuzika kama za wengine?
Namaliza kwa kusema kuwa sina haja ya kuwa na wasiwasi juu ya sababu ulizozitoa zilizosababisha yeye kujiua maana inawezekana. Hata hivyo nikukumbushe kuwa unastahili kuisaidia umma na polisi katika uchunguzi wao ili sheria ichukue mkondo wake kama mtu atatiwa hatiani kwa kutenda au kutotenda jambo ambalo alipaswa kulitenda ambalo limesababisha John kujiondolea pumzi ya uhai.
NAPENDA KUMPONGEZA HUYU RAFIKI JASIRI WA MAREHEMU AMBAYE KWA TAARIFA YAKE HII AMEOKOA MAISHA YA WATU WENGI AMBAO WAMEPATA BAHATI YA KUSOMA HABARI HII.MSONGO WA MAWAZO NI KATIKA MAGONJWA AMBAYO BINADADAMU TUNAWAKATI MGUNU SANA KUUPATIA MATIBABU. KWASABABU HAUSABABISHI NA UPUNGUFU WA VITU KAMA VITAMINI AU VIRUTUBISHO MWILI VYA AINANA YEYETO. MWANASAYANNSI WA KIJERUMANI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SIGMUND FREUD ALIPENDEKEZA TIBA MBADALA ISIYOHUSIHDA MADAWA IITWAYO PSYCHOANALYSIS. TIBA HII ILIKUWA NA KUSUDIO LA KUPAMBANA UGONJWA WA ASILI KWA KUKUNG'AMUA MOJA KWAMOJA CHANZO WAZO LILILOTIBUA AKILI YA MUHUSIKA.LAKINI KUTOKANA NA KUKOSEA TIMING NI VIGUMU KUSHIRIKIANA NA MGONJWA KUJUA HASA TATIZO LILIKUWA NINI NINI, TUKIANGALIA MCHAKATO WA MFIWA YEYOTE AMBAYE AMEFIWA NA MTU WAKE WA KARIBU KUNA KITU KINAITWA UVUMILIVU WA KUFIWA AU LOSE AND BEARVEMENT, KATIKA HILI LINA MIGWAYANYO WA AWALI ,WA KATI NA WA MWISHO, WA MWISHO NI ULE ULIOSHINDIKANA KWAMBA MUHUSIKA ANAKUWA MKIWA KWA MUDAA MREFU WA MAISHA YAKE.LAKINI CHANZO KUKUBWA KABISA KWA WATU AMBAO HAWAAMINI KWAMBA WANAWEZA KUPATA MATATIZO HAYO NI HILI SWALA LA MTU KUKATATA TAMAA BAADA YA MAJARIBIO YA MUDA MUREFU KUJIKWAMUA KIMAISHA. SASA KATIKA HAYO MAISHA KILA MTU ANA KIWANGO CHAKE INATEGEMEA NINI KITAMRIDHISHA KATIKA MAISHA AONE KAMA AMEFANIKIWA, SASA HAPA KILA MTU ANAKUWA NA MTU AMBAYE ANATAMANI ANGEKUWA NA MAFANIKIO KAMA YEYE. KITU MUHIMU HASA WATU KAMA SISI WATANZANIA TUWE NA MISINGI YA KUKIDHI MAHITAJI MUHIMU NA VINGINE NAONA VIWE VYA ZIADA. VIKIWEPO SAWA TUSHUKURU MUNGU TUKIKOSA TUSHUKURU VILELEVILE HUENDA KUNA SABABU . KUWA NA RAFIKI AU MARAFIKI WA KARIBU WANANAOKUFAHAMU KULIKO UNAVYO JIFAHAMU NI VIZURI SANA KWANI HAO NDIO WATAKAO KUSAIDIA KUKUWEKA SAWA PINDI MAMBO YANAPOENDA MRAMA. HAMNA KITU KIZURI KAMA KUJICHUNGUZA KILA WAKATI KWAMBA RAFIKI ZAKO WANAKUONAJE NA UBADILIKE NINI ILI KUDUMISHA MAHUSIANO AMBAYO YANAFAIDA KWA PANDE ZOTE.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.
ReplyDeletetumepoteza nguzo nyingine kwenye hiphop...story inasikitisha lkn sote tunatakiwa tujifunze, john ni kwasababu anajulikana je wangapi wamekumbwa na msongo huu wa maisha wakaamua icho alichoamua john??
ReplyDeleteRIP John
Wainalih-wainalihi laajun masikini kipenzi wa wengi ame2toka nilikuwa namzimia sana huyu john mjema sasa ame2acha inasikitisha sana
ReplyDeleteR.I.P John Mjema...Nimependezwa na jinsi NYAKATAKULE alivyohoji kwa huyo mleta habari..maana kama kweli ulikuwa unajua tatizo lake kwanini hukutoa msaada wa mawazo mpaka tatizo lilipotokea...kawaida binadamu tunapenda sanaa kuzungumza mambo likishatokea tukio ingawa mengine yanakuwa yapo ndani ya uwezo wetu kuzuilika..nilisikia John Mjema alikuwa milembe kwa muda kiasi..Poleni sana wafiwa...Wasanii wa bongo tuachane na majani hiyo ndo moja ya side effect zake
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi! sikuwahi kuwa na urafiki nae ila tumeshawahi kukutana kwenye harakati za kisanii,ukweli ni kwamba siwezi kusema au kuhukumu ila nachoweza kusema wasanii wa nyumbani tubadilike haswa kitabia,nimeona wengi wanavuta bangi kupita kiasi na wengine unga ,vitu ambavyo athari zake zipo wazi sana.
ReplyDeleteUnajua wasanii wengi waliokufa hapa kesi zao nyingi ni za ajali,haswa wakiwa wamelewa na ugonjwa wa ukimwi maana kwao ngono ya kuchanganyachanganya ndio burudani hivyo basi wasanii waamke wabadilike kabisa na mafanikio watayaona,ila wakiendelea hivi tutawazika kila siku.
inasikitisha kama utafuatilia mlolongo mzima wa vifo hivi utaona bangi inahusika ,pombe na madwa ya kulevya.
Swali langu muhimu ni hili,je ni lazima ufanikiwe kwa muziki ukiwa kama unahusisha hivyo vitu?
Mbona kuna wasanii wamefanikiwa bila kuhusisha?
jamani tubadilike.
Rest In Peace John Mjema.
ReplyDeleteAsante sana Solo Thang kwa habari muhimu za Marehemu.
Kwa kweli inasikitisha kusikia kuwa mtu anafikia hatua ya kujitoa roho. Ila tu naomba ieleweke kuwa hakuna binadamu ambaye anapenda kufa. Hivyo nakubaliana kabisa na mtoa mada kuwa kuna tatizo kubwa lililompelekea ndugu yetu huyu kuchukua uamuzi wa kujitoa roho. Tusimlaumu bali tujilaumu wenyewe na pia tutafakari ni nini cha kufanya ili kuondoa tatizo hili kwenye jamii yetu.
ReplyDeletePia kwa uelewa wangu nasikitishwa sana na sheria iliyopo nchini kuwa pale mtu anapofanya jaribio la kujiua basi huukumiwa kifungo. Ningeshauri badala ya kumhukumu mtu kama huyo basi zifanyike jitihada za kumsaidia na pia kujua nini kilichompelekea kuchukua uamuzi huo ili kuweza kupata vyanzo vya kujiua kisha tutafutie ufumbuzi wa kudumu. Iwapo mtu amekata tamaa ya kuishi then unampeleka jela unategemea kumjenga au kumbomoa zaidi mtu huyo hasa ikizingatiwa kuwa jela zetu zimejaa mateso ambayo ndiyo makali zaidi ya maisha huru yaliyomshinda mhusika?
Nashauri tuangalie upya hii sheria ambayo badala ya kumbadilisha mhusika inasababisha pindi anapokuwa mtu huru afikirie kujiua tena kwa kubuni mbinu madhubuti zaidi ili asikamatwe tena.
Maisha ni Magumu jamani na yanakatisha tamaa ila tujitahidi kumwomba Mungu na pia tuwe na huruma kwa binadamu wenzetu pindi tunapobaini kuwa wapo katika hali ngumu.....
Asilimia kubwa ya watu wanaochukua uamuzi wa kujiua hupata msukumo kutoka nje na si maamuzi binafsi. Kwa mfano mwanafunzi anapofukuzwa chuo ilhali alikuwa mwaka wake wa mwisho, Pale wazazi wanapokataa kumsaidia au kumuunga mkono mtoto wao katika jambo fulani au Mtu anaponyimwa haki yake ya msingi mfano kufukuzwa kazi bila sababu za msingi au kwa chuki binafsi za mwajiri wake pamoja na mambo mengine mengi tu....
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina
Posted Date::2/11/2008
ReplyDeleteMwanamuzi wa kizazi kipya ajiua kwa kisu Dar
Na Beatrice Charles
MSANII wa muziki wa miondoko ya Bongo Fleva, John Mjema amejiua kwa kujipiga kisu,polisi wamethibitisha jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 jioni, Mtoni Kijichi eneo la Neluka na kwamba msanii huyo alijichoma na kujichinja sehemu ya shingoni.
Kamanda Kandihabi alisema mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye alitoa taarifa kwa polisi, Michael Kassim (20) alisema mjomba wake anadhaniwa kuwa alikuwa ameathirika na ugonjwa wa ukimwi.
�Tulikuwa tikimsikia akisema mara kwa mara kuwa yeye ameathirika,� alisema Kassim.
Akizungumza na gazeti hili katika ofisi za Mwananchi jirani wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema marehemu Mjema alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na kwamba alikuwa ameanza kuchanganyikiwa akili, hali ambayo ilimfanya afikie hatua ya kuanza kuvua nguo.
Alisema kabla ya kufariki Mjema alikuwa chini ya uangalizi wa ndugu zake kutokana na majaribio ya kutaka kujiua.
�Alitaka kujiua kipindi cha nyuma, lakini siku ya tukio ndugu zake hawakuwepo nyumbani ndipo yeye akapata nafasi ya kujiua kwa kutumia kisu,� alisema jirani huyo.
Wa inna illahi rajiuun.All i can say is this-The John i knew was a very hard worker alikuwa hakwepi kazi na mwepesi kutumwa na kusaidia.Pia katika uzima wake alikuwa na nidhamu.Matatizo ya dunia yanaweza kumkumba mtu yeyote pahali popote na akabadilika msimtambue.The story is a fable...do not judge others and as humans extend a helping ahnd when hand when needed.Tusiache mwanya wakuambiwa..."You tripped me when i was falling,you kicked me when i was down.You poured water on a drowning man..."
ReplyDeleteKweli mdau kuna kipindi nafikiri inaweza kuwa ni mwaka jana mwezi wa sita au wa tano nilikuwa Mtoni Kijichi karibu kabisa na kwa kina Mjema kwa jamaa yangu mmoja mara akapita John Mjema kavaa kichupi bila shati, yaani kila mtu akaanza kuponda hawa wanamuziki umarekani huu utawaponza.Sikuelewa hali aliyokuwa nayo basi nikafikiri ni kawaida tu ya mbwembwe ya wanamuziki wetu.KUMBE ALIKUWA KATIKA HALI NGUMU.
ReplyDeletePoleni sana Mambo Jambo na wadau wote kwa msiba huu mzito.
Depresion ni hali mbaya sana ila ndugu zangu kwa wale mliowahi kukumbwa na hali hii mpo hai sasa kwa sababu mlijipa matumaini,au mliyakubali mazingira yenu. Kwa wale ambao hamjakumbana na hali hii ikiwatokea kamwe msijiue nendeni kwenye nyumba za ibada,safirini mkatembelee ndugu,jamaa marafiki au shiriki tatizo na watu wako wa karibu,au uwaone watu wa 'canceling'. Ila kumrudia mungu ni muhimu mno utapata tumaini jipya. Kwa ufahamu wangu kujiua ni kujihukumu mwenyewe na adhabu yake ni kali sana sote tunaifahamu. Dini zote zinaeleza kujiua ni kujihalalishia moto wa milele,ndugu zangu tufahamu ilo kamwe tusifichane huo ndio ukweli. Naomba radhi kwa nitakao wakera lakini kujiua ni mwanzo wa adhabu kali mbele ya mungu. Mtu aliyejiua mchungaji,padre,shekhe watu hawa huwa hawakubali kutoa ibada ya mazishi,husema hawaoni sababu kwani muhusika ameshakufa roho na mwili. Nimeumia sana kusikia John Mjema kafanya vile kwani mwisho wake ni mbaya na ndio sikitiko langu. Narudia tena wadau tuache hadi mungu atuhukumu kamwe tusijihukumu. George
ReplyDeleteRIP in John Mjema! Nakumbuka mara yangu ya kwanza kumuona na kupata kuongea na Mjema pale Diamond Jubilee aliposhusha ile classic song MIMI SIO MWIZI live. Hii stori imenistua sana, jamaa alikuwa ametulia sana kimuziki na nyimbo zake kadhaa zilikuwa kali mno.
ReplyDelete