alama ya mahali alipouliwa olof palme
jumba la sinema alilotoka na mkewe akiwa hana bodigadi
mtaa ambao olof palme aliuwawa
mie na mh. ndunguru tulibahatika kupaona mahali ambapo waziri mkuu wa sweden olof palme alipigwa risasi na kuuwawa siku ya ijumaa februari 28, 1986 huko stockholm, sweden. alipigwa risasi wakati yeye na mkewe lisbet palme walipokuwa wanatoka kuangalia muvi katikati ya stockholm kwenye kona ya mtaa uitwao Sveavägen.

miaka miwili baadaye jamaa mmoja, Christer Pettersson, alikamatwa kuhusiana na mauaji hayo na alipatikana na hatia, hata hivyo mahakama kuu yalipindua hukumu hiyo jamaa akaachiwa. inasemekana mwaka jana pettersson, ambaye alifariki mwaka 2004, aliungama kitendo hicho katika barua alizomwandikia mwandani wake. hata hivyo wataalamu hawana uhakika kwamba kuungama huko kulikokuja baada ya miaka 21 kutasababisha kufunguliwa upya kwa kesi hiyo ya mauaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mi ni mpenzi mkubwa wa kipindi cha forensic files, kuna cku walionyesha peterson amabaye alikuwa mtuhumiwa wa mauji hayo ya waziri mkuu. baada ya kuachiwa huru alihamia marekani na huku akawa anatembea na mke wa mtu na akapigwa risasi na huyo mume mtu. na mwili wake ukatupwa porini lakini ulipatikana!
    Shuk,Texas.

    ReplyDelete
  2. hizi story za sweden zinatuhusu nini sisi wabongo
    tupe news ambazo zitasaidia kuleta maendeleo bongo badala ya hizo za waziri mkuu wa sweden aliuawa mtaa huu alitoka jumba hili la sinema alikaa kiti hiki
    sisi wabongo hazitatuletea maendeleo yoyote

    ReplyDelete
  3. Hii ni kama Kibatari bin koberiti! Kumbe wako wengi tu!

    ReplyDelete
  4. hii comment imeniacha hoi ..."hizi story za sweden zinatuhusu nini sisi wabongo
    tupe news ambazo zitasaidia kuleta maendeleo bongo badala ya hizo za waziri mkuu wa sweden aliuawa mtaa huu alitoka jumba hili la sinema alikaa kiti hiki
    sisi wabongo hazitatuletea maendeleo yoyote"

    Sidhani kuna lolote baya kujua kuna nini kilichowahi jiri miaka ya nyuma/nchi za watu. Mbona wafuatilia FA cup/Premier league, Kenya Violence, Election in America, Ze Commedy n.k bila kijiuliza mbongo inakusaidia nini.

    "Panua" mawazo kaka ( if you are a kaka by the way.

    ReplyDelete
  5. Hivi Michuzi Umetembe Anchi ngapi?
    Mi naona ungetumia Muda mwingi kuwafahamisha watu ulichojifunza katika matembezi yako hayo ingekuwa powa.. Sio kama hao viongozi wenu wanaokuja Ulaya na marekani kila siku lakini hata kuiga kujenga vituo vya mabasi wanashindwa kazi kununua maVX tu. JK nimeona ana VOLVO YA AJABU. Ile aliyokuwa anatumia raisi mstaafu ilipigwa mnada au ALIONDOKA nayo?
    Nadhani Magari ya maraisi yagekuwa yanapigwa Mnada Serikali ingemake hela nyingi sana. na zingeweza kusaidia sekta nyingine Kibao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...