Hi Bro.Michuzi!

Habari za huko kwetu. Kwanza kabisa ninatoa salamu kwa watanzania wenzangu wote popote pale walipo wapenzi wa blog hii.

Nimefurahishwa na jambo moja, hapa Italy: Ni kwamba mwanasiasa mmoja maarufu nchini hapa jina ni PAULO BONAIUTI alikuwa akiongea kwenye vyombo vya habari nchini hapa, na kusema usemi usemwa Tanzania: "Usimwamini hata kidogo simba ambaye kalala" (Mai fidarsi del leone dormiente).

Nilikuwa nafuatilia kipindi fulani kwenye TV, ndipo nilipomsikia jamaa akiongea huo usemi wa Tanzania, na baadae nimeona kwenye magazeti mbalimbali ya hapa wameandika, mojawapo ni hicho kipande nilicho tuma akiwepo na yeye, huyu jamaa BONAIUTI ambaye ni katibu wa Berlusconi wa chama cha Forza Italia.

Aliwatahadhalisha wenzake wa chama hicho wasijiamini kuwa watashinda kiulaisi, bali wakaze uzi, ndipo akasema usemi huu, akitoa mfano.

Je usemi huu upo kweli Tz? Au ni kamba zake tu huyu jamaa. Maana kwa sasa wanasiasa wapo kwenye kampeni za uchaguzi ambapo hapo mwezi wa 4 kutakuwa na uchaguzi kutokana na serikali ya bunge na mawaziri kuvunjika, kutokana na kujihuzuru kwa aliye kuwa Waziri wa sheria, ambaye alituhumiwa na kashfa mbaya hasa mke wake, kuingiza ndugu na jamaa zao kwenye vitego maalumu pasipo staili, na wala kuwa na elimu yoyote.

Salamu sana Tanzania!

Ni mimi Mdau B. F.Chibiriti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Bwana Chiribiti kweli sasa umeonesha ukomavu kwa kuamua kabisa kuweka picha ambayo wadau watashindwa kusukutulia...

    kuhusu mada yako hapo juu naweza kusema kuwa simba aliyelala kwetu Tz hana madhara makubwa manake unaweza mwenyewe kuona wanasiasa wetu wa upinzani wasivyo na msimamo. Leo yupo Chadema kesho amehamia CUF mara masalhi hayapo anarudi CCM.

    ReplyDelete
  2. jamani,mnaokijua kiswahili vizuri,naomba mututafsiriye,mimi sijamuelewa kabisa chibiriti

    ReplyDelete
  3. chibiriti...chibiriti... umerudi tena? mi sisemi kitu subiri waoshavinywa waamke utakipata unachokitaka maana naona hukomi tuu, huruma jamani hurumaaaaaaaaaaaaa chibiriti...........................

    ReplyDelete
  4. we Chibiliti kama unasomeshwa na hla za wavuja jasho ni bora ukarudi nyumbani hizo hela zikaenda kununulia vyandarua kwenu Mtimbira huko!!!

    Huna hoja sasa kutajwa Tanzania tuu kwako ni ajabu? we unawaona waitaliano watu wa maana mjomba kaa uzuri huko wenzio wengi huko wameishia kuwa...(huku anakot0ka Mh Pius Msekwa, kunaitwaje tena...?). hawafai hao, Ohoooo

    ReplyDelete
  5. Mimi huwa nikiona tuu salamu kutoka kwa Chibiriti najikuta nacheka mwenyewe sijui kwanini. Teah Bwana chieriti sasa ndugu yangu hicho Kiitaliano sisi tutakisomaje? Tutafsirie basi story nzima ndugu yetu Chibiriti kisicho na Njiti?

    ReplyDelete
  6. Nashindwa hata mimi kumuelewa Chibatari wa Chibiriti, kwanza kabla hatujatoa maoni, tunaomba tuone maendeleo yako binafsi kaa ni bado una viti vya mbao au lah(JOKE), anyway...mii nadhani unataka kulinganisha kashfa ya waziri wa sheria wa Italy na bwana EL wa kwetu Tz, ki msingi na naomba sn tuangalie kwenye kupeana adhabu au uwajibikaji, so nakushauri utupe muendelezo wa sakata hilo hapo Italy ili tuwe tunalinganisha na jinsi lilivyo shughulikiwa kwetu Bongo, ahsante Chubatari wa Chibiriti, ila wadau tunaomba saana PICHA ZAKO!!

    ReplyDelete
  7. Chiribiti anauliza hivi.. Je kuna usemi au mithali ya kitanzania inayosema Usimwamini hata kidogo simba aliyelala? Hayo maelezo mengine yote ni kuwafafanulia tu kwanini ameuliza kuhusu huo msemo.

    Lilly, UK

    ReplyDelete
  8. Bwana chibiriti wewe kweli siyo mchezo na una moyo mgumu ni balaa!haya ngoja utajibiwa na wataalam wa lugha yetu ya Taifa!hivi makii hassan yuko wapi?...

    ReplyDelete
  9. Mtanashati, hakika sijawahi kuona utata au tatizo katika maandishi au picha zilizopita za ndg.Chibiriti.
    Baadhi ya watu wamekuwa wanamhukumu kwa muonekano wa mahala alipo, samani anazotumia na mambo kama hayo ambayo kwangu hayakuwa hoja.

    Kinyume chako, kama anony 15:47 alivyobaini,leo ndio namwona (Chibiriti) kutokuwa makini ama katika kuhakiki anachokiandika (maana kuna makosa kadhaa ya kiuandishi) au katika namna ya uanzishaji wa hoja.

    Ni bayana kuwa usemi unaozungumzia simba aliyelala au tamathali za semi zinazolandana na hii kama vile 'usidhani simba aliye nyeeshewa mvua kuwa ni paka' n.k upo Tanzania katika kiswahili na hata katika baadhi ya lugha mbalimbali za makabila yetu.

    Hoja isingekuwa kuwepo au kutokuwepo kwa usemi huu bali pengine kama una ukweli gani au maana gani leo Tanzania kuhusiana na .........(hapa angetoa tukio ambalo linashabihiana usemi huo)

    ReplyDelete
  10. CHIBIRITIumeitoa kagombee Ubunge kijijini kwako

    ReplyDelete
  11. Bw. Chibiriti na Anony Na.2 wa 11:47. Huo usemi dhahiri upo Tanzania isipokuwa lugha sahihi na fasaha kwa huo usemi hufahamika kama "SIMBA MWENDA POLE NDIYE MLA NYAMA" ikimaanisha kwamba "USIMDHARAU MTU HATA KIDOGO" AU kwa kimombo "DON'T UNDERESTIMATE ANYONE" kwa tafsiri isiyo rasmi lakini.

    ReplyDelete
  12. Chibiriti bin Chibatari! Balaa tupu!

    ReplyDelete
  13. bro chib mi huo usemi sijausikia ila nnaoujua mimi unaomhusu simba unafanana na huo ni:
    "usicheze na simba ukamtia mkono kinywani",
    au wa kufanana na neno kulala ni:
    "usimwamshe aliyelala ukimwamsha utalala wewe"

    bro huwa nakarahika sana mtu anapotumia silabi mbadala kwenye neno na kuharibu lafudhi ya neno au maana ya neno mf.1. wasijiamini watashinda (kiulaisi)ni "kwa urahisi"
    2. kutokana na (kujihuzuru) ni "kujiuzulu"
    pole kwa kifungu changu cha mwisho kama hutakipenda ila nafurahia zaidi kusikia matamshi murua na yanapotakikana.

    ReplyDelete
  14. Jamani wadau ni hivi, kiukweli kabisa mimi huwa nasoma tuu salamu za bwana Chibiliti, nami nikiona tu kichwa cha habari huwa nacheka sanaaaa yani siku yangu nzima huwa imejawa na furaha, this man is brightening my day

    pls pls pls wadau mi namfurahia sana bwana Chibiliti pls nawaombeni sana mumuache aendelee kutuma makala zake hata kama anakosea isiwe tabu,

    somo ninalopata hapa kwa huyu bwana ni kutokata tamaa hata kama dunia yote inakugeuka

    BWANA CHIBILITI... TAFADHALI USIWASIKILIZE WATU WE TUMA TUU MAVITU BABAKE

    CHIBILITI HOYEEEEEEEEEE...........

    NA UKURUDI BONGO GOMBEA UBUNGE MSHKAJI WANGU EBWANNA NDIO.........

    ReplyDelete
  15. BWANA CHIRIBITI ANATAKA UMAARUFU KWA KILA NAMNA UMEJITAHIDI ANYWAYYYYYYY

    ReplyDelete
  16. 1.Mimi binafsi ninapata matumaini kwamba angalau sasa tz inajulikana. Miaka michache iliyopita ilikuwa ukitaja tanzania kwa nchi za wenzetu pamoja na kwa mdau Chibiriti watu walikuwa wanapekuwa ramani kuona kama kwenye tufe la dunia hii kuna nchi inaitwa hivyo. Lakini kama imefikia hadi kwa wanasiasa kujinadi kwa misemo ya tz, basi, ni hatuwa.
    2. Tulipata shida pia miaka michache in the past kutangaza utalii wa tz kwa sababu kama hizi. Ilikuwa ukisema Serengeti iko tz unaonekana muongo maana ilishavuma kwamba Kilimanjaro na Serengeti ziko Kenya. Lakini sasa naona mambo yanakuwa rahisi kwa sababu nchi hii sasa inaweza kusimama kwa bendera yake.
    3. Kinachotakiwa sasa tujitahidi tusijulikane kwa semi, methali na nahau tu bali tutumbukie ndani ya teknolojia tuvumbuwe chochote kizuri ili siku moja (si ndoto ya mchana) waitaliano wasimame na kusema 'mkinichaguwa mimi nitahakikisha kifaa (fulani) kilichogunduliwa tz kinaingizwa italia bila kodi' tehe tehe!
    4.Kuhusu usemi wenyewe inawezekana aliedit kidogo. Anons wengi wemechangia misemo inayorandana. Lakini kwa ufahamu wangu ni kwamba simba akiamka kutoka usingizini huwa aktivu wakati huo huo, hana hang-over(ili ileleweke kwa urahisi) ya usingizi. Kwa hiyo nadhani mwanasiasa huyo alikuwa anamaanisha hata kama vyama vingine vinaonekana vimelala vinaweza ku-bounce back immediately kama ambavyo Kp jana alitowa mmaasai mmoja akisoma 'bounce back' by jacob zuma!.....

    ReplyDelete
  17. SIKUBALIANI NA WATU WANAOSEMA CHIBILITI ANATAKA UMAARUFU WA NINI? IKIWA MTAKUBUKA VIZURI MARA YA KWANZA KUTOKEA HUMU KWENYE BLOGU CHIBILITI ALISEMA YEYE NI MTANZANIA ANAYEISHI HUKO CESSENA KAMA SIJAKOSEA HILO JINA, PEKE YAKE. HAKUNA WATANZANIA WENGINE KATIKA MJI WAKE.

    MIMI NAFIKIRI HII NI NJIA YAKE YA KUONGEA/KUWASILIANA NA WATANZANIA WENGINE. NAKUSIFU KWA HILO CHIBILITI OTHERWISE UNGEZIDI KUJIONA MPWEKE, ENDELEA KUWASILIANA NASI KWA KUTUMA PICHA KULETE MAKALA KAMA HIZO.

    KUHUSU METHALI KUNA YA SIMBA MWENDA POLE NDIYE MLA NYAMA. ILA HUYO PENGINE AMECHUKUA SEMI ZA MAKABILA NA KUNA SEMI NYINGI TU HATA ZA KISWAHILI KAMA VILE USICHEE SHARUBU ZA SIMBA ALIYELALA! N.K.

    ReplyDelete
  18. kwa mimi naona maana yake simba alielala hua analala macho yake lkn pua zake hazijalala na sisi binaadamu hrufu zetu ni kama mahanjumati kwa wanyama...

    ReplyDelete
  19. Bwana Chibiliti, kwa kweli nikiona jinalako tu huwa najawa na furaha saaana!
    Usipotee sana bwana wee, tunahitaji sana michango yako kwenye blog hii kaka. Hayo maneno ya watu kuhusu wewe wala usimind kawaida yetu watanzania kwani watanzania wote ni watani hivyo endeleza mambo kaka.
    Sasa Chibiliti mbona kapicha hujakabandika( Uliyovaa shati la kitenge)
    CATEL (NAGOYA JAPAN )

    ReplyDelete
  20. acheni ujinga wadau inamaana upeo wenu wakuelewa ni mdogo kiasi cha kwamba mmeshindwa kumuelewa jamaa.jamaa kaona swala ambalo limemgusa huko alipo na kaweza kuliunganisha na hali alisi tanzania.kama amuelewi jamaa anacho kisema tafuta mtu yoyote karibu na wewew akueleza zaidi ambaye unamujua ana uwezo wa kufahamu zaidi yenu.

    ReplyDelete
  21. Jamani hata Paulo Bonaiuti mu-Italiano anatutoa ushamba hatujui Kiswahili chetu wenyewe?'Usimwamini Simba alielala hata kidogo',ni kweli usemi huo upo katika lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.Simba ni Simba.Usije ukamuona kalala ukamchezea chezea au hata kujisogeza akasikia harufu yako.Lolote laweza kukutokea.Big Up ndugu yangu Chibatari oops no Chibiriti!Hapa nimeongeza word power yangu ya Ki Italiano,'Mai fidarsi del Leone dormiente'Safi sana hiyo.Tanzania jamani inatambulika.Bali sisi wenyewe Watanzania totoro!Nafikiri umeipata.Tuletee nyingine Chibiriti.Walioka kwenye Vyama vya Siasa,kaeni chonjo,msije mkadanganyika na kulala kwa Simba.Huenda ni usingizi man'gamung'amu liko lake jambo,na tumesha anza kuyaona!Mwenye macho haambiwi tazama!

    ReplyDelete
  22. CHIBIRITI THE GREAT

    ReplyDelete
  23. Kibiriti juuu juuuu juuuu zaidi kibiriti oyeeee oyeeeee.Nakuhakikishia bwana ukienda bongo kugombea urais utashinda tu.Kwani mwanzo watu walikusema weeeee lakini sasa wengi wao wametokea kukupenda.Na hii blog ya michuzi inasomwa na watu wengi wa kitanzania waliopo katika nchi tofauti tofauti hapa duniani.

    ReplyDelete
  24. Wadau ambao hawajamuelewa muheshimiwa chibiriti naomba musome comment ya JOHN PAUL kafafanua vizuri sana.kuhusu chibiriti anavyoshambuliwa kutokana na jinsi anavyosjiwakilisha nitawakumbusha kidogo tu " do not judge a book by its cover".chibiriti endelea kuwa wewe ( do you) nautafanikiwa kutimiza malengo yako.sisi watanzania tunashindwa kujua mda wa utani na mda wakuwa makini tunapo toa hoja .pia kuna kitu kingine kwamba ukatishaji wa tamaa kwa wenzetu.sasa watu wanajaribu kumshambulia chibiriti kila anapotokea hapa huku wao wenyewe wana skeletons hidden in their closets.

    ReplyDelete
  25. Kwanza kabisa ninawasalimu tena sana! Jamaa wa 2:45 am, anasema nikisikia tu Tanzania basi, sina hoja, Ninapenda kuku kumbusha kuwa Tanzania ni nchi yangu, sina budi kujivunia na kuipenda kwa moyo wote. Sasa wewe unataka niisifie nchi gani? Mimi ninawashukuru ninyi nyote kwa kunijibu swali langu, maana kuuliza si ujinga. John Paul umesema kweli kabisa, maana hata mimi nilipo fika hapa miaka ya nyuma ilikuwa ni shida kumfahamisha mtu, sehemu ilipo Tz, mpaka useme karibu na Kenya ndipo wanakuelewa, lakini sasa angalau kidogo afadhali. Salamu sana kwenu ninyi wote! Ninakupenda sana tena sanaaaaaaa.......!!!!!!!! Tanzania na watu wake woteee!!!, na wala sita kusahau daima Tanzania Mia sempre nel mio Cuore!
    CHIBIRITI.

    ReplyDelete
  26. ndugu zangu watanzania sisi ni kiboko.yani baada ya kumpongeza chibiriti kwa kutuonesha jinsi gani misemo yetu inatumika duniani tunaendelea kumhukumu kutokana na picha zilizo pita? Kama mafisadi serikalini wangekuwa wanaandamwa kama chibiriti humu basi nchi ingekuwa imebadirika mno na mafisadi wangeona aibu kuendeleza ufisadi wao.

    ReplyDelete
  27. WHAT A TURN AROUND FOR MR CHIRIBITI, LAZIMA LEO MZEE UTALALA VIZURI, ANGALIA LEO COMMENTS ZILIVYO MORE POSITIVE. UMESHAKUSANYA WAPENZI KWENYE BLOG HII, YOU MUST BE PROUD OF YOURSELF. ILA NATAKA KUJUA HII METHALI ULIYO TUPA ARE YOU TRYING TO TELL US SOMETHING "POLITICIAN IN THE MAKING"

    ReplyDelete
  28. Bwana Chibiriti, ni wewe tena?! Hahahaha.... Kwa kweli mimi huwa najikuta natabasamu hata kama nipo depressed, kila nionapo posting na salaam toka kwa bwana Chibiriti. Huyu bwana huwa anaibuka pale watu wapomtarajia na akiibuka tu kila mtu analazimika kuweka comment. Huo ni mvuto wa kipekee na kwa hilo mie ninakusifu Bw. Chibiriti. Halafu hili jina lako ni la kweli au pia ni usanii wako? Haya tutaongea next time ukileta kituko kingine.

    ReplyDelete
  29. He bwana Chibiriti, umenichekesha sana. Bado upo tu!

    ReplyDelete
  30. CHIBILITI MAMBO MZEE..WAHESHIMIWA KABILA HII WAKO KATIKA JAMII UTAKE USITAKE..

    ReplyDelete
  31. BOB CHIBBY... you are my role model

    ReplyDelete
  32. AAH CHIBIRITI WEE NAONA BADO UNATIKISA KIBERITI.

    NA WADAU WAMEKUITIKIA BWANA, SIO UNAONA COMMENTS HIZO UTAFIKIRI MAREHEMU CHIFUPA AU DADA CYNTHIA VILE !!

    HEHEHEHEEEE .. :))

    ReplyDelete
  33. HIVI WEWE JINA LAKO CHIBILITI AU CHIBIRITI...
    MANAKE KWENYE HOJA ZAKO NYINGINE UNAJIITA CHIBILITI, NYINGINE CHIBIRITI...AU NI KIINI MACHO. SIDHANI KAMA MTU UNAWEZA KUKOSEA JINA LAKO UNATUMIA ALL YOUR LIFE....KUNA WALAKINI HAPA!!!!!

    ReplyDelete
  34. safi sana nchi yetu sasa inajulikana sana tunashukuru,sasa bwana chibi habari za huko kwetu italy zinaendaje nasikia sasa hivi una plasma tv unaendesha bmw kama wenzako wa ukerewe na marekani au maisha bdio vile vile kama ulivyopost tule tu fenicha twako na computer,mh chibi maisha ni magumu lkn nao kwako ni zaidi any way ndio maisha hahaaaa upweke utakuua rudi home tukutane roze garden upate rost kidogo au umeshazoea kujipikia ukitoka job?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...